Na pia kama kuogopa gharama basi hata wanajeshi waende likizo hadi tunapojiandaa kwa vita ndio waitweHayo ni mazoezi ya kijeshi, yana tija na ni muhimu kwa usalama wetu. Hakuna nchi isofanya vitu hivyo. Hata nchi zilizoendelea bajeti zao za mambo ya ulinzi ni kubwa sana.
mmh jamani...umeanza vizuri hoja mwishoni utumbooo. hivi nyie watanzania mtu huwezi kuongelea jambo muhimu bila kunyunyizia na umbea? yaani uwezi kabisa?
Hivi wewe unadhani Jamii Forum ni ukurasa wa wapumbavu. Una elimu gani kuhusu taratibu za urukaji wa ndege za jeshi? Kuona ndege za jeshi zinaruka unakurupuka eti mafuta kodi ya wananchi inatumika vibaya. Unajua hiyo ndege imenunuliwa na kodi hiyohiyo ya wananchi au kwa upeo wako mdogo ukajua jeshi limenunua ndege ili lichezee mafuta ya wananchi? Haya mambo sio ya kukurupuka kwenye mitandao kama hii unajiandikia tu. Kumbuka hii nchi inalindwa na wanajeshi mpaka wewe unapata jeuri ya kuongea madudu yako humu. Ndege za jeahi la wananchi katika anga hili la watanzania zitaruka mahala popote pale na wakati wowote ule na hii no katoka kutekeleza majukumu yake kipindi cha amani ili kurahisisha mapambano kipindi cha Vita.
upikie ndizi huo utumbo huwaga ni mzuri sana.
Heshima kwenu waungwana,
kwa mliopo dar wengi wenu mtakua mmeshuhudia ndege tatu za jeshi zikiwa zinarushwa kwa kufuatana kwa kasi sana angani, mimi swali langu ni je gharama zake zina faida au tija kwa taifa? Je mafuta yanayotumika sio kodi ya jasho la watanzania? Hebu tupia maoni yako hapa
Sio kila jambo linalofanywa na Serikali basi lazima upinge. Mbona hukuuliza kwanini zimenunuliwa kwa Kodi zetu???
Embu ulizia Nchi zilizoendelea harafu watakwambia wao ndege wanarusha lini hadi lini, mimi ninavyojua wenzetu kila siku wanafanya haya mazoezi tofauti na sisi mpaka sikukuu.
Kumbuka hili ni Jeshi la Ulinzi la Watanzania ambao wamekufanya wewe uwe huru muda huu kwenye Simu/PC yako unaandika vitu kama hivi.
Ivi tulishanunua ndege mpya? Au bado tuna rusha zile mig79 za kirusi tangu wakati wa nduli.
Heshima kwenu waungwana,
kwa mliopo dar wengi wenu mtakua mmeshuhudia ndege tatu za jeshi zikiwa zinarushwa kwa kufuatana kwa kasi sana angani, mimi swali langu ni je gharama zake zina faida au tija kwa taifa? Je mafuta yanayotumika sio kodi ya jasho la watanzania? Hebu tupia maoni yako hapa
tatizo unatumia ------ kufikiri,unadhan kila jambo linalofanyika lazima uone faida zake moja kwamoja,kaa na uzezeta wako,ivoivo
vita gain ya kupigana namadege sasa hivi? Adui was taifa la Tz ni ujinga ,umaskini,rushwa iliyokithiri na viongozi kusaini mikataba yenye kufilisi nchi yetu . kurusha ndege ni kupotosha malengo kama ni mazoezi waende porini . kama wanavyofanya US mazoezi wanafanyia kwenye jangwa la Nevada.Jwtz wakifanya vizuri Congo,Darfur tunawasifia. Unadhani jeshi bila mafunzo/mazoezi wanaweza kushinda vita?