Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

SEHEMU YA 23

Siku zikakatika. Kwa Fareed, maisha yalikuwa burudani lakini hakutaka kuendelea kuwa na mwanaume mmoja tu. Alitaka kila mwanaume mwenye mwili mzuri awe wake. Hakuacha kujiremba, alijipamba, alijua kujisafisha na kila alipokuwa, alikuwa akinukia maradhi ya Zenji, alijua kurembua macho, alijua kubinua midomo na zaidi ya yote alijua sana kuzungumza hasa kwa sauti ile ya kike.

Kwa wakati huo, alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda Dubai. Alikuwa akimsindikiza mpenzi wake huyo aliyekuwa akienda kwa mambo ya kibiashara. Alichukua ndege pamoja naye, alivalia mavazi ambayo ilikuwa ni vigumu kugundua kama alikuwa mwanaume, alijiremba, alivalia dela na kichwani alivalia kiremba.

“Unakwenda Dubai?” aliuliza wakala wake aliyeitwa Asteria Kimaro, mwanamke aliyekuwa akiwaunganisha wanawake na wanaume tata kwa wanaume wengi waliokuwa wakiishi Ulaya, Asia na Marekani. Alijenga nyumba nyingi, kununua magari ya kifahari kwa biashara hiyo tu.

“Ndiyo!”
“Kuna wateja wawili wanakuhitaji huko. Nishafanya mawasiliano nao, nakutumia namba zao. Wanakuhitaji sana,” alisema Bi Asteria.
“Haina shida! Ila wana hela?” aliuliza Fareed, yeye alikuwa akifikiria hela tu.

“Eeh! Mtu aishi Dubai, awe mfanyabiashara mkubwa halafu asiwe na pesa! Umeona wapi hiyo! Hao wana hela mpaka wanaumwa!” alisema Bi Asteria.
“Basi sawa.

Naomba namba zao!” Akatumiwa namba hizo. Mwili wake ulikuwa ukiwasha mno, kila alipokaa, akili yake ilikuwa ikifikiria pesa tu. Hakutaka kuona akiishi maisha ya kimasikini, alijitoa maishani mwake, hapokuwa alikuwa akifanya jambo gumu, lenye kujidharirisha lakini hakuwa na jinsi, hayo yalikuwa maisha ambayo aliyachagua na alipaswa kuishi katika maisha hayohayo.

Walipofika Dubai, wakateremka ndani ya ndege, haikuwa mara yake ya kwanza, alikwishawahi kufika mara kadhaa hapo, wakatoka nje na kuchukua gari kisha kuelekea hotelini. Walipofika huko, ilikuwa ni kujiachia tu, walikuwa wakiyafurahia maisha, Godfrey alisahau kama alikuwa na mke, kwake, mwanaume huyo tata alimridhisha mno.
 
SEHEMU YA 24

Usiku wa siku hiyo wakati Godfrey akiwa amelala huku amejichokea zake, Fareed akachukua simu yake na kuanza kupiga namba za wanaume aliokuwa amepewa. Alianza na mwanaume wa kwanza, huyu aliitwa Saed Al Muntazir, alikuwa mwanaume mwenye mwili uliojazia, ndevu nyingi, alikuwa mwanaume wa shoka, mweye pesa zake, kama alivyokuwa Godfrey, hata naye tabia yake ilikuwa ileile, kulala na wanaume tata kuliko hata wanawake.

“Nilipewa namba yako!” alisema Fareed, alikuwa amekimbilia chooni kuzungumza na mzee huyo.
“Kutoka wapi?”
“Kwa Asteria…”
“Ooh! Kumbe nini wewe! Hebu nitumie picha zako za utupu zikionyesha ulivyoumbika,” alisema mwanaume huyo.
Hiyo ilikuwa kazi ndogo kwa Fareed, hakutaka kuchelewa, hapohapo akamtumia picha hizo alizokuwa amekaa mikao ya hasarahasara, mwanaume huyo akazipokea, akaanza kuziangalia, mwili wake ukasisimka, hakuamini kama angekutana na mtu mwenye sura nzuri, umbo mashallaah kama alivyokuwa Fareed.

“Njoo hotelini kwangu!”
“Sawa. Nitakuja kesho asubuhi!” alisema Fareed.
“Sawa mpenzi!”
Hakutaka kukaa chooni kwa muda mrefu, akatoka na kurudi chumbani. Alipofika, macho yake yakatua kwa mpenzi wake, Godfrey ambaye alikuwa amekaa kitandani huku akionekana kuwa na hasira kupita kawaida.

Alivimba, alikuwa akipumua kwa hasira, paji lake la uso lilikunja ndita, kwa jinsi alivyoonekana, hakuonekana kuwa kwenye hali ya kawaida. Fareed aligundua kwamba kulikuwa na kitu, akagundua kwamba inawezekana mwanaume huyo aliyasikia mazungumzo yake alivyokuwa chooni, akaogopa kwani kuachwa na mwanaume huyo kulimaanisha angepoteza vitu vingi, starehe zote zingepaa.

Akaanza kumsogelea, hakuzungumza kitu, kwa mbali alionekana kutetemeka lakini hakutaka kulionyesha hilo, hakutaka agundulike kama alikuwa na hofu kubwa. Alipomfikia pale kitandani, akakaa pembeni yake na kuupitisha mkono wake katika bega la Godfrey.

“Tatizo nini mpenzi?” alimuuliza Godfrey.
“Ulikuwa unaongea na nani?” aliuliza huku akionekana kuwa na hasira kali.
“Rafiki yangu!”
“Ndiyo ukaongelee chooni!”
 
Shunie mi wacha niingie Badoo nikawatafute Kina Fareed
We mwanaume si kila siku upo huko badoo unaniaga nn me nilishakuacha sababu ya hizo mambo zako mtu unawakula mpaka wakina fareed
 
Niwekee bhanaa! Sa ntajuaje kama G alimpiga?!
umeanza najuta aiseee iceman kukufundisha kusoma story dada nikiweka nyingi kutakuwa na maarosto bado haijamaliziwa hii
 
We mwanaume si kila siku upo huko badoo unaniaga nn me nilishakuacha sababu ya hizo mambo zako mtu unawakula mpaka wakina fareed
Hapana.... Nimelazimika kwenda kule baada ya kukukuta na KIBEN10, hivyo nikaona wacha niende BADOO kupunguza Stress, yaani umesababisha niwe MUHUNI kupita kiasi
 
Hapana.... Nimelazimika kwenda kule baada ya kukukuta na KIBEN10, hivyo nikaona wacha niende BADOO kupunguza Stress, yaani umesababisha niwe MUHUNI kupita kiasi
Kila la heri baba angu na hiyo badoo yako
 
SEHEMU YA 25

“Jamani! Si mambo yetu ya kikekike mpenzi! Kama nimekukera naomba unisamehe bebi…” alisema Fareed, alizungumza kwa sauti nyembamba mno ambayo aliamini ingeufanya moyo wa mwanaume huyo kulainika, hakutaka mwanaume yule aliyekuwa akizungumza naye ajulikane, akajitahidi kuificha simu yake na kisha kuanza kumbusu Godfrey, alianzia mashavuni na kuhamia mdomoni, yote hayo ilikuwa ni kumsahaulisha na kile kilichokuwa kimetokea.

“Umekasirika mpenzi?” aliuliza Fareed.
“Usijali! Ila siku nyingine jitahidi kuwa muwazi,” alisema Godfrey na kisha wote kupumzika kitandani.
“Kesho ndiyo kesho! Ni lazima nikaonane na huyo bilionea, nimchune mpaka achunike,” alisema Fareed huku akiachia tabasamu pana, hakutaka kuwa na Godfrey, kwanza alitaka kuwa na nafasi ya kujaribu asali ya mzinga mwingine.
*
*

Akili ya Fareed ilichanganyikiwa, kichwa chake kilifikiria pesa na hakutaka kuona akiwaacha wanaume hao na wakati aliambiwa kwamba walikuwa na pesa, mabilionea wakubwa wa mafuta huko Dubai.

Alilala na Godfrey lakini kichwa chake hakikutulia hata mara moja. Asubuhi ilipokwisha na Godfrey kumuaga kwamba anakwenda kuonana na wafanyabiashara wenzake kikaoni, akaanza kuwasiliana na Bwana Saed na kumwambia kwamba alikuwa na muda, kama alikuwa na nafasi waonane katika hoteli yoyote ile.

“Unapafahamu Bavaria?” aliuliza Bwana Saed.
“Ndiyo!”
“Nenda hapo! Ukifika, waambie kwamba wewe ni mgeni wangu, utapewa chumba na nitakuja huko! Nina kikao kidogo na wafanyabiashara wenzangu!” alisema Bwana Saed kwenye simu.

“Sawa mpenzi! Ila unajua malipo yake?”
“Niliambiwa ni dola elfu moja!”
“Ndiyo mpenzi!”
“Nitakupa dola elfu tano! Kwani nimeangalia picha zako, zimenidatisha kishenzi!” alisema Saed maneno yaliyomfanya Fareed kutoa tabasamu pana.

Hakutaka kuchelewa, akaondoka hotelini hapo na kuelekea katika hoteli aliyokuwa ameambiwa. Njiani, bado alijiona kuwa na uhitaji mkubwa wa kutafuta pesa.

Alijua kwamba alikuwa akijidhalilisha lakini hakutaka kujali, alijitoa, hayo ndiyo yalikuwa maisha yake ya kila siku, alikuwa tayari kuutumia mwili wake kwa staili yoyote ya maisha lakini mwisho wa siku apate pesa.
 
Back
Top Bottom