SEHEMU YA 163
Siku ya tarehe 26.08/2016 ndiyo siku ambayo Fareed akafariki nchini Marekani huku akiwa kwenye maumivu makali. Ulikuwa msiba mzito kwa marafiki zake lakini hata maofisa wenyewe wa FBI walihuzunika, hawakutaka kabisa kumpoteza Fareed kwani aliwasaidia kupambana na magaidi kwa asilimia tisini.
Taarifa hiyo ikatolewa kwenye televisheni, mawasiliano yakafanyika na FBI wenyewe ndiyo walioshughulikia safari ya kuusafirisha mwili wake kuelekea nchini Tanzania ambapo baada ya kuwakabidhi ndugu, wakawaachia kiasi cha dola laki tano ambazo ni zaidi ya milioni mia tano kama shukrani kwa kila kitu alichokifanya Fareed kwao.
Huo ukawa mwisho wake, mchezo wa kuingiliana na wanaume wenzake ukayagharimu maisha yake, akafa katika maumivu makali.
Akaunti yake ilikuwa na pesa nyingi, zaidi ya bilioni ishirini lakini zote akaziacha kwa ndugu ambao kwenye kugawana tu mpaka wengine wakauana, na pesa nyingi zilikuwa zile alizopewa kama zawadi na Bilionea Williams ambaye alikuwa akitumia kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kuhusika na mauaji ya Bilionea Belleck.
Huo ukawa mwisho wake, marafiki zake walimkumbuka, watu aliotembea nao wakamkumbuka, aliacha historia, mbali na mchezo mchafu aliokuwa ameufanya, wema wake, ucheshi na roho yake nzuri viliendelea kuwa mioyoni mwa watu wengi.
MWISHO