Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

SEHEMU YA 150

Mauaji ya Bwana Belleck yaliyokuwa yametokea nchini Ufaransa yalimshtua kila mtu, watu hawakuamini kile kilichokuwa kimetokea, ni ndani ya siku tatu mabilionea wawili walikuwa wameuawa na kwa jinsi alama za mauaji zilivyokuwa zikionyesha, kila mtu akagundua kwamba muuaji alikuwa mmoja.

Polisi walichanganyikiwa, wakawasiliana na polisi wa nchini Misri na kuwaomba kuwatumia picha ya mtuhumiwa, hilo halikuwa tatizo, picha ikatumwa na ilipowafikia, wao wenyewe walishangaa.

Alikuwa mtu yuleyule aliyekuwa akitafutwa sana na FBI kwa kosa la kulipua kituo cha treni cha Pennsylvania. Hawakujua sababu ya mwanaume huyo kufanya matukio yote hayo.

Wengi walihisi kwamba alikuwa gaidi, lakini gaidi na mabilionea wale kulikuwa na kitu gani kilichokuwa kikiendelea?
Hakukuwa na aliyekuwa na majibu, kila mmoja alikuwa na hamu ya kumkamata Fareed na kuweka wazi kile kilichokuwa kikiendelea mpaka kufanya matukio yote hayo.

“Atafutwe kila kona, wekeni picha zake katika vituo vyote vya televisheni duniani, sambazeni kadiri mnavyoweza mpaka kuhakikisha huyu mtu anatiwa mikononi mwa poli,” aliagiza mkurugenzi wa FBI nchini Marekani, Bwana Sandal Peters.

Mawasiliano yakafanyika kwenda nchini Ufaransa, polisi wa huko hawakujua mahali alipokuwa mtu huyo hivyo kwenda hotelini kwa ajili ya kuangalia kamera za CCTV ambazo waliamini kwamba zilimnasa mwanaume huyo.

Hilo halikuwa tatizo, wakapata picha ya mwanaume huyo, wakafuatilia kumfahamu zaidi mtu huyo, picha zake zikasambazwa kwenda sehemu nyingine, walijua kwamba mwanaume huyo alivyokuwa ameingia nchini Ufaransa alipitia sehemu katika bandari au uwanja wa ndege hivyo kwenda huko.

Walitafuta kila kona, walichukua picha za wasafiri wote waliokuwa wameingia katika sehemu hizo lakini hawakufanikiwa kuipata picha yake.

Walipohamia kwa watu walioingia humo kwa ndege binafsi wakafanikiwa kuipata picha ya mwanaume huyo, maelezo yalisema kwamba aliingia ndani ya nchi hiyo kwa kutumia ndege binafsi iliyokuwa ikimilikiwa na bilionea kutoka nchini Marekani, Peter Williams.

“Is this Williams’ jet?” (hii ni ndege ya Williams) aliuliza polisi mmoja.
 
SEHEMU YA 151

“Yeah! Why did he do this?” (ndiyo hii! Kwa nini amefanya hiv?) aliuliza polisi mwingine.
“We don’t know! We have to arrest him,” (hatujui! Tumkamateni) alisema polisi huyo.

Kwa msaada wa interpool, Bwana Williams akakamatwa, akawa mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ya mauaji yaliyotokea nchini Ufaransa.

Na kwa sababu alikuwa amemsafirisha mtu aliyehusika katika ugaidi, akapewa kesi hiyo nyingine kwa kuwadhamini magaidi kulipua kituo cha treni cha Pennslyvania.

“Simfahamu kijana huyo,” alisema Williams wakati akiwa katika chumba cha mahojiano.

“Na alifikaje ndani ya ndege yako? Nani alimtafutia vibali? Kwa nini aliingia nchini Ufaransa kwa ndege yako na kuondoka kwa ndege yako?” yalikuwa maswali kadhaa ambayo alishindwa kuyajibu.

Kila mtu akajua kwamba alihusika katika mauaji ya Bilionea Belleck lakini pia alihusika katika tukio la kigaidi lililotokea hapo Pennslyvania.

**** Fareed alikuwa akilia, maumivu ya tumbo yaliongezeka, alijua kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake. Siku hiyo hakula kitu, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea tumboni mwake. Mawazo yake yakamwambia kwamba yale matunda aliyokuwa akila ndiyo yaliyomsababishia hali ile.

Siku hiyo ilipita huku akiwa kwenye maumivu makali, aliumia kupita kawaida. Usiku hakulala, alikesha akilia kwa maumivu makali, aliendelea kukohoa na kutoa madonge ya damu.

Ilipofika majira ya saa tano asubuhi ndipo kwa mbali akaiona meli moja kubwa ikielekea kule alipokuwa. Hakuwa na nguvu za kutosha lakini akasimama na kuanza kupunga mikono yake juu huku akijitahidi kutoa sauti ili asaidiwe pale alipokuwa.

Hiyo ilionekana kuwa nafasi pekee ya yeye kuondoka kisiwani pale. Meli ile ikaendelea kusogea, kwa mbali akawaona watu kutoka kwenye meli ileile wakipunga mikono kuashiria kwamba walimuona.

Vijana wawili wakafungua mtumbwi uliokuwa katika meli yao na kisha kupanda, hapohapo wakaanza kuelekea kule alipokuwa Fareed kisiwani ambapo baada ya kumfikia, wakaanza kumuuliza maswali kadhaa kuhusu sababu iliyomfanya kuwa mahali pale.

“Tumbo linauma…” alilalamika Fareed huku akilishika tumbo lake, hata maswali aliyoulizwa akashindwa kuyajibu kabisa.
 
Sitaki kabisaaa uchokozii
Nisamehe jamani
Nipe hela nkusamehe
Subiri nikadange
Usidangee
Sasa ntapata wap hela ili unisamehe
Muombe shululu
Nichune Mimi ntakupa
kumbe kudanga unajua mfyuuuuuuu mpaka ukutane na bango utajua kila aina ya kudanga
 
Back
Top Bottom