Michezo ipo mingi ila mna ng'ang'ania mpira. Kwani ndio mchezo pekee mnaoujua?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,015
12,293
Moja ya agenda za ajabu ambazo sizielewi katika taifa hili ni kuamini katika mchezo wa soka kama njia pekee ya kututambulisha kimataifa.

Hii agenda imekwisha shindwa mara nyingi hakuna maajabu yoyote yatapatikana katika mchezo wa soka katika nchi yetu.

Tubadili fikra zetu na kuamua kuuweka mpira wa miguu kama mchezo wa burudani tu kufurahisha roho za Watanzania na sio kuuchukulia serious kama mchezo pekee wa kutuvusha na kututambulisha kimataifa.

Ni wakati sasa kujitafuta katika michezo mingine wenda itatutoa na kututambulisha duniani.

Wachina wali invest a lot of money kwenye soka wakitegemea wataleta maajabu duniani lakini holaa hakuna kitu walichopata lakini sio kwamba hawana michezo mingine wanayo tamba hapana. Mchezo kama table tennis ndio mchezo wao haswa wachina na wanajulikana duniani kwa ubabe wa mchezo huo.

Wakenya wamejipata kwenye riadha na wanafanya vizuri.

Wamarekani kwenye soka wamejaribu kwa kuokoteza wazee kutoka huko ulaya lakini holaa ila wamarekani kwenye Basketball huko ndipo wanapotamba na kujulikana duniani.

Warusi, waukraine, wamexico hawa kwenye ndondi ndipo wanapo tambulika duniani.

Ipo mifano mingi ya nchi mbalimbali duniani zilizo amua kutafuta michezo mingine nje ya soka na wamejipata na wanafanya vizuri haswa.

Tubadili fikra zetu Watanzania tutafute na tuwekeze mchezo tunaoweza huko ndipo tutatokea.
 
hakuna anayekulazisha kushabikia mpira, ukitaka kashabikie taarabu, mapenzi ya mpira hasa kwa wanaume yanakuja automatically kuanzia utoto labda kwa vijana wa siku hizi wanaanza kucheza computer game ,
 
Kama kuna mashindano ya machawa duniani basi tunaweza kuonekana
 
Inashangaza...... ! Halafu Kingine cha ajabu Kuna Wachezaji wazuri wengi tu Lkn Wamewang'ang'ania Wachezaji wa Utopolo..! Wengine hawawaoni?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom