Nini faida ya mgeni rasmi kwenye mpira wa miguu?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Nianze kwa Kuwasalimu, Naamimi Mko salama na Mnaendelea Vizuri Kusubiri Weekend Hii kuona Timu zetu Za Tanzania Zitafanya nini Katika Michuano Ya Kimataifa.

Kwa Miaka Kadhaa Sasa vilabu vikongwe vya Tanzania Vimekuwa na Taratibu za Kuwatumia Wanasiasa Katika Michezo Yao na Kuita kile Wanacho Sema Kuwa NI MGENI RASMI katika Mchezi Fulani. Huu Utaratibu kwangu mimi nimeona Ukiwa unafanyika sana Tanzania, Kuwatumia Wanasiasa Kama Wageni Rasmi Katika Mechi Za Kimataifa au Zile Mechi Kubwa Zinazo Vuta Hisia za Wengi.

Hii haijawa Kwenye Mpira wa Miguu tuu hata Michezo Mingine Wanasiasa Wamekuwa Wakijiingiza katika michezo kwa Mgongo wa Mgeni Rasmi. Kwangu Mimi Ninaona Huu ni kama utaratibu wa Kuwatumia na kuwanufaisha wana siasa huku Ndio watu wanao ongoza kwa Kujaribu mpira wetu kwa Kuweka Siasa Katika Michezo.

Mataifa makubwa Duniani, Na Walio wekeza nguvu katika Michezo huwa huwezi kuona wakimtumia Mwana Siasa Kama Mgeni Rasmi Wa Mchezo Fulani. Hata Hivyo Jukumu na lengo la Mgeni rasmi Katika Mpira wa Miguu haliwaji kuwa lenge lenye kuleta Mashiko kutokana Na Namna Mchezo unavyo Fanyika.

Kuna Watu wengi sana Nchi hii ambao wamefanya Makubwa Katika Michezo nje ya Wanasiasa wanao ingia Na Kutoka. Lakini Legends hawa wamekuwa Hawapati hata Nafasi kidogo ya Kuwa Mgeni rasmi na wamekuwa Wanaishia Kuwa Wachambuzi wa Mchezo pamoja na Makubwa Yote waliyo Fanya Katika Kukuza Mchezo wa Soka Na Michezo mingine.

Vilabu Vikubwa Vya Yanga Na Simba Ambavyo Tumekuwa Tukivitetea Pale Wanasiasa wanapo Jaribu kuwaingilia Ndio vimekuwa Vilabu vinavyo ongoza Nchi kwa Kuwatumia Wanasiasa Kama Wageni Rasmi katika Michezo Yao. Lengo Lao Huwa nini? Ni Busara Ifike Tuwaache wanasiasa wafanye siasa zao na watu wa mpira wafanye mpira wao, Kama Taifa Tukiendelea Kuwatumia Wanasiasa katika Michezo Mbali Mbali si Ajabu Kuona Haya Yanayo endelea kwenye mpira yenye ushabiki ndani yake.

Kama Kuna Haja ya Kuwa na Mgeni Rasmi katika Michezo , ni vyema watu wa kwanza kufikiriwa wawe wale Legends ambao Vizazi vya sasa Havijui ni Makubwa gani wamefanya katika Soka. Ni wakati wa Simba Na Yanga kuacha kuwa Watumwa wa Viongozi wa Siasa Na Kutumia Kuwapa Umaarufu Viongoi wa Siasa Bila sababu ilihali ndio wanao ongoza kwa kurudisha nyuma maendeleo ya Mpira wetu.

Kataa Wageni Rasmi wa Kisiasa Katika Mpira wa Tanzania.
 
Kituko NI pale eti kamisaa WA mechi Naye analazimisha kupiga picha na waamuzi ...sijajua why tff na wanauzamani sana
 
Ulishawahi kuona hiz timu mbili za k/koo mgeni rasm anatoka nje ya mfumo wa serikali? Kama jibu ni hapana, " soma katikat ya msitari"
 
Kidumu chama.........
 
Kituko NI pale eti kamisaa WA mechi Naye analazimisha kupiga picha na waamuzi ...sijajua why tff na wanauzamani sana
Ile picha ya pamoja ilikuwa inachukuliwa kama ushahidi wa wahusika kuushuhudia mchezo
Zamani kulikuwa amna azam tv ukiritimba pia ulikuwa mwingi so kamishna wa mchezo ni shuhuda namba katika kutoa report ya mchezo husika lakin kwa sasa ni vitu ambavyo vimepitwa na wakati
 
Ndio 100%
 
Back
Top Bottom