Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Mchezo wa kabumbu, ujulikanao kama Mpira wa miguu, kwa kimombo Soccer au Football. Ni miongoni mwa michezo pendwa Duniani, na ni mchezo unaoshika nafasi ya kwanza duniani kwa kutizamwa na kufatilia. Kwa hapa Tanzania mpira wa miguu umekuwa una vipindi maalumu vya uchambuzi kwenye Radio na TV ukilinganisha na michezo mingine kama Mchezo wa ngumi, mpira wa kikapu na kadharika.

Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu uhalali na uharamu wa mchezo wa mpira wa miguu kwenye Dini ya kiislamu. Wengi wakisema ni mchezo haramu, na hauruhusiwi katika Dini. Lakini cha kushangaza waarabu wenyewe ambao ndio Dini imetoka kwao ni wafuasi namba moja wa mchezo huo ambao hivi karibuni tumeona wamepindua meza kwa kuamua kusajilii miamba ya soka kutoka sehemu mbalimbali za ulaya na mabara mengine hili kuvutia Soka la uarabuni. Vivyo hivyo tumeona Mchezaji mpira "Christiano Ronaldo" akiwa kwenye basi mmoja katika jiji huko Nchini Iran 🇮🇷 ambayo ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya kiislamu, lakini tuliona Ronaldo akikimbiliwa kama Masiha au Mwokozi, na watu wa Iran. Hata hapa tunaona watu walioshika Dini mfano haji Manara kila Mwaka anaenda kuhijj Macca na sehemu takatifu za urabuni na kuhubiri Dini lakini pia ni muumini mzuri wa mpira wa miguu.

Na Nchini pia tunaona Masheikh wengi wakiwa misikitini wanahubiri mpira ni haramu lakini wao ndio namba moja wanaokwenda kutizama soka, mfano nilienda Jijini Mwanza wilaya ya Sengerema, kuna msikiti hupo mjini alafu kwenye njia ya kuingilia msikitini kuna vibanda viwili vya kahawa vyenye TV ambavyo watu wakitoka kuswali upumzika hapo kunywa kahawa na mazungumzo ya hapa na pale, ila vibanda hivi ufurika siku za mechi ya Simba na Yanga na mechi nyingine za kuvutia, na wanaokaa hapa wengi wao ni waislamu ambao wanataka kuingia msikitini au wanaotoka kuswali msikitini.

Kwa anayefahamu, tunaomba maelezo pia kama ikiwezekana na vifungu vya Quran kwamba mpira ni haramu... Maana wengine wanasema vitu ambavyo havikufanywa na mtume vingi ni haramu, na mwingine akauliza mtume alihubiri kwa kutumia kifaa gani, sasa kwa nini hawa masheikh wanatumia Microphone. Na kadharika sasa tunaomba ufafanuzi kuhusu mpira wa miguu juu ya uharamu wake.

View: https://www.instagram.com/reel/Cv5i1zWrLAy/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==
 
Uislam vitu vilivyoharamishwa ni pombe, nguruwe, basi
Kwa hiyo mpira si haramu?

Maana ukipitia hata Comment za haki Manara kwenye post aliyoenda huko uarabuni alipozikiwa Mtume utakuta watu wakimsihi na kumuomba aachane na mpira kwa sababu kwenye Dini ni haramu... Sasa hapo kipi ni kipi
 
Uislamu unaangalia outcomes ya kitu yaani matokeo ya kitu .

Mfano mpira kuanzia uvaaji labda nguo fupi ,matangazo ya pombe kweny jersey na udhamini mwingine kama mambo ya ushoga ..

Na saudi ni nchi usisema labda wote ni waislamu wote , waislamu wanafuata kitabu sio idols wala matamko ya mtu zaidi ni fatwaah juu ya uhalisia wa jambo kwa dalili za Qur an na sunnah...

Hata israel wanasema taifa teule wakristo ila huo ukristo hautakiwi hata kufanya mahubiri yake...

Vitu vinavyoletwa na mpira ndio inapelekea dhambi ila sio mpira halisi kama mtavaa vizuri nguo ndefu kidogo,hapatokuwa na matangazo ya pombe na vitu vingine ...

kiufupi kama sio muislamu hapo hautoelewa kabisa .
 
Kwa hiyo mpira si haramu?

Maana ukipitia hata Comment za haki Manara kwenye post aliyoenda huko uarabuni alipozikiwa Mtume utakuta watu wakimsihi na kumuomba aachane na mpira kwa sababu kwenye Dini ni haramu... Sasa hapo kipi ni kipi
aya gani inasema mpira ni haram? Hakuna aya yoyote kwenxe quran inayokataza mpira
 
aya gani inasema mpira ni haram? Hakuna aya yoyote kwenxe quran inayokataza mpira
Hapo ndio utamkamata !?😅😅uharamu wa mpira ni mambo yanatokana na mpira kama kukaa uchi , matangazo ya pombe mambo ya betting yaani kamari.

Ila mpira hauna tatizo..

Atakusumbua kwa vile uislamu unaangalia matokea ya kitu ...
 
Kweli maana matangazo ya pombe na kamari hata kwenye tv yapo! Kwa iyo na tv nayo ni haramu?
 
Kweli maana matangazo ya pombe na kamari hata kwenye tv yapo! Kwa iyo na tv nayo ni haramu?
Unanielewa au hauna elimu?
Mpira unatumika kupromote pombe na kamari ,kuvaa uchi hayo mambo ndio yanapelekea uharamu..

Swali ulishaona wapi channel ya dini ile pure hata ya kikristo ikipromote pombe na betting?

Je hizo betting na pombe wewe unaona ni swa kwako?

Ukijibu ntakupa elimu kidogo.!!
 
Kiufupi mpira ndio bomu lilisukwa kiustadi kuumaliza uislam mazima. Ona huko kwenye nchi kuliko na uislam mwingi ndio mpira umeenda kutua huko mpaka ulaya inaona wivu kuwa soka lao linapoteza mvuto, ligi zao zinaharibiwa kwa mastaa wengi kukimbilia uarabuni kuliko na uislamu asilia. Michuano mikubwa kupelekwa huko. Ni suala la muda tu uslam utaangamia duniani kwa mambo ya starehe na burudani na mioyo ya waislam itapenda zaidi mpira, kujaza viwanja kuliko kujaza misikiti. Nani ataenda msikitini wakati mechi kali yenye mastaa nguli inachezwa uwanjani? Mpira unadunda na ndio umekuwa dini mpya pendwa
 
aya gani inasema mpira ni haram? Hakuna aya yoyote kwenxe quran inayokataza mpira
Mimi nimeuliza hili kupata uhakika... Maana nimemuona sheikh hapo kwenye video anasema mpira ni haramu, na niliwahi kumsikia haji Manara akisema "Kwanza Mpira" ni haramu, pia kwenye comment za page ya Manara, watu wanamwambia Manara mpira ni haramu.... Sasa na mimi ndio nimeuliza kupata ukweli juu ya uharamu huo
 
Elewa kwanza sio kila muarabu ni muislam japo wengi wao ni waislam.
Mpira ni Haram kwa dini zote.
Uharamu wake huja kutokana na nampangilio wa namba kuanzia idadi ya wachezaji,mda wa kucheza, Angel, pitch nk vipo calculated.
Mpira ni ibada
 
Hapo ndio utamkamata !?😅😅uharamu wa mpira ni mambo yanatokana na mpira kama kukaa uchi , matangazo ya pombe mambo ya betting yaani kamari.

Ila mpira hauna tatizo..

Atakusumbua kwa vile uislamu unaangalia matokea ya kitu ...
Sasa kukaa uchi, matangazo ya pombe, betting na mpira kuna uhusiano gani... hapo haramu sio mpira ni vitu husika kama kukaa uchi, pombe, betting... Ambavyo sio kila mtu anayecheza mpira au kutizama mpira anavifanya... Kukaa uchi, betting na pombe ni hulka ya mtu tu, wapo watu wanaopenda mpira na si wafuasi wa hivyo vitu... Je ni vyema kuendelea kusema mpira ni haramu
 
Elewa kwanza sio kila muarabu ni muislam japo wengi wao ni waislam.
Mpira ni Haram kwa dini zote.
Uharamu wake huja kutokana na nampangilio wa namba kuanzia idadi ya wachezaji,mda wa kucheza, Angel, pitch nk vipo calculated.
Mpira ni ibada
Ndio nakubaliana na wewe kwamba sio kila muarabu ni muislamu, lakini asilimia zaidi ya 80% ya waarabu duniani ni waislamu, sijawahi kuona muarabu kanisani. Labda unless useme wapo wapagani ambao hawana dini. Pia ningetaka uzungumzie kwa kina Mpira ni ibada kivipi, maana hata wangecheza watano, wakabadili angel, pitch na vinginevyo bado ungesema ni ibada... Sasa tupe mbadala mpira uchezejwe hili husiwe ibada
 
Niliwahi kuambiwa na mtaalamu mmoja wa dini kuwa, mchezo km mchezo hauna uharamu wowote. Tatizo au kilichopelekea kuharamishwa ni kule kutowezekana kutenganisha vitendo vichafu vinavyoendana na mchezo husika.......uongo, ushirikina, rushwa, matusi, ugomvi, mauaji, n.k
 
Ndio nakubaliana na wewe kwamba sio kila muarabu ni muislamu, lakini asilimia zaidi ya 80% ya waarabu duniani ni waislamu, sijawahi kuona muarabu kanisani. Labda unless useme wapo wapagani ambao hawana dini. Pia ningetaka uzungumzie kwa kina Mpira ni ibada kivipi, maana hata wangecheza watano, wakabadili angel, pitch na vinginevyo bado ungesema ni ibada... Sasa tupe mbadala mpira uchezejwe hili husiwe ibada
Google utawaona waarabu Kanisani.
Au haujawahi sikia makanisa yanapigwa moto nchi za kiarabu
Ni nchi chache uarabuni hazina makanisa.
Mpira kombe la dunia mpira wa miguu ni la kishetani.

Biblia inamtaja shetani kama joka

Nembo ya kombe la Dunia ni chatu aliyejipinda kichwa kikiwa juu

Na kombe lenyewe la mpira kombe la dunia ni chatu aliyejipinda kichwa kikiwa juu

Timu zinazocheza kombe la dunia zinashindania kuchukua kombe lenye sanamu ya joka kuu shetani wachukue sanamu ya joka shetani kupeleka kwao.

Angalia vizuri mwenyewe kuhakikisha ninachosema nembo ya kombe la dunia ikitulia au kwenye TV linavyonyeshwa timu zikicheza na kombe lenyewe linavyoonekana ni ushetani mtupu

World football Cup ni kugombea kichwa cha shetani
Mpira unapromote ushoga
 
Hapo kwenye kupromoti ushoga ni kivipi?
 
Back
Top Bottom