Michepuko inaanza leo rasmi!

Michepuko inaanza leo rasmi!

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,956
Reaction score
25,345
Kipindi cha michepuko kimewadia! Utafiti unaonyesha kwamba kila michuano mikubwa ya mpira inapoanza kama vile Kombe la Dunia, UEFA Champions League na Kombe la Mataifa ya Afrika, wanaume wengi wakware huwalaghai wake/wapenzi zao kwamba wanaenda kutazama mechi kumbe hutumia mwanya huo kuteleza kwenda kwa nyumba ndogo (Michepuko).

Leo michuano ya Kombe la Dunia inafungua pazia huko Brazil. Tayari kutakuwa na wanaume wakware ambao wameishapanga ‘appointment' za kukutana na michepuko yao kwa kutumia kisingizio feki cha Kombe la Dunia. Nawaasa akina mama muwe makini na ‘Njia Kuu' zenu kwani huu ndio wakati mtakaodanganywa na hatimaye ‘kuibiwa' waume zenu kirahisi kabisa. Jengeni utaratibu wa kuandamana na waume zenu kwenda mpirani ili muweze kuzidhibiti nyendo zao za kilaghai. Siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli. Nimetimiza wajibu wangu wa kuwapa tahadhari. Kama kuna mwanamke atamuachia mumewe aondoke nyumbani hiiivi hivi na hatimaye kuibiwa, shauri yake.

Nawasilisha.
:help:
 
Mimi nina kibali cha kuangalia mechi zote hadi fainali, nimekodishiwa Lodge ya karibu na nyumbanio kwa zile mechi ambazo zitaisha saa kumi na moja asubuhi.....Nampenda Mke wangu hahhahahahahahhaaaa
 
Aende tu,tena akinogewa aseme kashinda ticket ya kwenda Brazil kabisa ili ahamie huko huko!!!


Hahaaa, nimeipenda hii. Ila mi nitasema tumepewa offer ya kuangalizia mpira hotel, mens only bila wake zao maana wataharibu ushangiliaji!
 
Mimi nina kibali cha kuangalia mechi zote hadi fainali, nimekodishiwa Lodge ya karibu na nyumbanio kwa zile mechi ambazo zitaisha saa kumi na moja asubuhi.....Nampenda Mke wangu hahhahahahahahhaaaa

Unatudanganyaaa!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom