Sielewi ni kwa sababu gani hali iko hivi, lakini ni wazi kwamba ubora wa walioko mjengoni uko chini. Watu wanashindwa hata kuunda maswali yanayostahili kuulizwa bungeni. Maswali mengi ni ya kuulizia miradi ya shule, urefu wa barabara, visima vya maji, n.k. vya kiwango cha wilaya na majimbo. Swali linalohusu jimbo moja linapewa sapoti na mwingine akisema, hata jimboni kwangu ni hivyo!
Sikiliza majawabu ya serikali sasa! Taaabu! Kila kinachosemwa na waziri, kinaitwa ni jawabu lakini ukweli ni kwamba mengi hayana maana kwa mwananchi wa kawadia. Tunachosikia ni vijimaneno na kuchanganya na viingereza ili tujue waziri lugha inapanda: Mtu unajibu swali la kilimo, linalowahusu wakulima wa Tanzania unaweka mipango yako kwa vijiingereza vilivyotawaliwa na matamshi ya Kiswahili!
Wenzangu mumewasikia wachangiaji wa wizara ya elimu? Taabu kabisa. Nahisi wengi wanasaka maneno yenye nadharia fulani vitabuni halafu wanakuja kwa kuvuta hewa kwa nguvu, wakitaka serikali iwasikilize; Elimu inahitaji mabadiriko, mitaala ibadirike, angalia wenzetu ulaya, elimu haiko sawa, haiwapi uwezo wa kujitegemea.
Hili siyo Bunge la miaka 60 baada ya uhuru. Wapo maprofesa kama Kabudi, atakapoanza kujibu kwa mtindo wa kufundisha kama alivyokuwa anafanya bunge liliopita, ajue hakuna wanafunzi wa kuelewa.