Michango ya mwenge ni sawa na kutakatisha fedha

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,793
18,216
Leo nimesikia kwa masikio yangu mwenyewe kiongozi mmoja wa CCM akimkoromea mtendaji wa Kata kwanini hakusanyi michango ya mwenge. Hili jambo limemisikitisha sana kwa kweli. Unajua tangu zamani nilikuwa nasikia walimu wakilalamika kukatwa mishahara kuchangia mafuta ya mwenge nikadhanini masikhara! Leo mimejionea mubashara bila chenga.

Kitendo cha CCM kuwakamua walimu na wananchi fedha kwa ajili ya kuchangia mwenge ni uhalifu kama uhalifu mwingine. Ikiwa mafisadi wengine wamekuwa wakikamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa utakatishaji fedha, sasa wakati umefika hawa wachumiatumbo wa CCM na yeyote anayehamasisha utakatishaji wa fedha wakamatwe na kufunguliwa mashtaka ya utakatishaji fedha.

Ikiwa serikali haina mafuta ya kuwasha mwenge kwanini bado wanang'ang'ania kuuwasha? Si wakimbie tu bila mwenge kwani lazima? Wananchi wamekuwa kila siku ndio wahanga wa kila upuuzi unaoshobokewa na hawa mafisadi wa CCM.

Ni juzi tu CAG ametoka kuwaeleza jinsi wanavyoibiwa matrilioni ya fedha lakini bado hawa wanaizaya bado wanaendelea kuwakata walimu fedha na kuwakamua wananchi hata zile fedha kidogo zilizobaki baada ya kiasi kikubwa kukamuliwa na mafisadi wa CCM! Waache ujinga wao wa kipuuzi. Wananchi wananufaikaje na hiyo mienge yao ya kishetani? Nchi ya kipuuzi sana hii.
 
IMG_20230328_185528.jpg
 
Moja ya pesa hata ukose kuandika muhutasari wa kutoa fedha huwezi rudishwa ni kwenye swala la mwenge,yani unapeleka muhutasari hauna mahudhurio na unapita na unaenda toa fedha
 
Back
Top Bottom