Michango ya harusi mikubwa halafu tukifika shereheni hatushibi

Michango ya harusi mikubwa halafu tukifika shereheni hatushibi

Wakati we unalalamika hujashiba kamati ya mapishi huwa wanaoendelea vyakuja si mchezo, yahani kwa mahesabu ya break fast hadi lunch!!
 
Hakuna kitu cha kipuuzi kama kulipia ukumbi Million Tatu, Mbili alafu A/C zero, bora ukaenda readers club, unalipia laki 600 tu vinywaji unajitegemea, mpambaji laki nane, keki 180, eti mtu keki laki tano???
 
Ndugu zangu naomba niende kwenye Mada huska
Kiukweli kuna jambo linaniumiza Sana hasa swala la michango ya ndugu wanao owana
Kimsingi hua wanagawa card ili tuwachangie fedha ili wafanikishe sherehe yao
Cha ajabu unakuta Single unaambiwa uchangie 45.000 au chini ya hapo km itakuwa Dabo basi Dau linaongezeka
Mwisho siku ukienda kwenye sherehe unakuta unapewa chakula ambacho ni saizi ya mtoto wa Miaka 2
Unakula ila hushibi
Ndugu wadau hii imekaaje au ni Mimi tu sishibagi vzr



Mbarikiwe, karibuni mchangie hoja, povu lina ruhusiwa
Ni shida kwa kweli
 
Dalili za watu wa mikoani. Buku 45 analalama. Demu utahonga Shs ngapi?
 
Unatusingizia sana watu tunaotoka kanda ya ziwa nadhan ile ni hulka ya mtu tu wala haihusiani na kanda Fulani
Ila anyway you have made my day nmecheka sana
Misosi kwenye harusi mtu wa kanda ya ziwa hawezi shiba labda wawe wanajisevia wenyewe hapo itabidi na muandaaji wa chakula naye sasa alipwe mara tatu maana ile kanda watu wanakula aisee hakuna cha mtoto, mwanamke , wanaume sasa ndo balaa utadhani mashindano au siku inayofuata ameambiwa hakutakuwa na chakula.
 
Msingi wa Sherehe ni kula na Kunywa ila siku hizi wanatumia hela zote kwenye mambo yasiyo na msingi. Magari ya ufahari, wachukua video, kumbo za kifahari nauzembe kama huo. Hela ya msosi inabaki kiduchu.
Kuna jamaa yangu juzi karudi anatukana wamemlaza njaa.
 
Hahahhaha...

piga beer mzee..

ila mi nishajitoa hizo habari.
 
Harusi ni biashara za watu....pale kamati ndio zinaongoza kwa kupiga hela.
 
kama haujawahi kuwa kiongozi kwenye kamati nyeti za harusi, hapa utalalamika sana.
Btw, harusini sio restaurant
 
michango yenu ya harusi mnatuboa sana hamjui tu, oaneni bila kutusumbua kwani mmeambiwacbila harusi hamtazaa watoto?
muwe mnatualika tu kwenye sherehe zenu tuje kula na sio kadi za michango, kuoa uoe wewe mi nitoe hela yangu ya nini?
wabongo bwana
 
Afadhali wewe mkuu sikiliza mimi sasa
Tarehe kama 10/9/2018 mtoto wa kaka anayesoma shule ya Brain Trust School iliyopo Buza aliniletea kadi ya mchango akamiambia
Bamdogo mwalimu kasema nikuletee hii barua,kuifungua nakuta wanahitaji mchango wa mahafali ya darasa la 7 kiasi cha 20,000/=.
Baba yake akalipia hiyo hela sasa siku ya mahafali nikaulamba saf nikategemea nitakula msosi wa maana.
Dah muda wa msosi sikuamin nilijikuta natukana kimoyomoyo maana tulipikiwa wali,pilau kidogo,mtori na njegere soda mojamoja na maji ya 500 dah yaan baada ya matonge 6 sahan nyeupe na sikushiba kabisa
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Single 100,000
Double 150,000


Ni wizi kama wizi mwingine
Fedha inakusanywa halafu tazama matumizi yake
Mapambo
Zawadi kwa mwoaji au mwolewaji
Pombe
Usafiri
Upuuzi mtupu, tunahitaji mageuzi makubwa ya fikra kuachana na uninga huo
 
Back
Top Bottom