Michango kuwanusuru viongozi: CHADEMA imekubali hatia?

Kwanini wasiende kutumikia jela miezi 5 ni michache sana
bora hizo pesa wakanunue kiwanja cha kujenga ofisi ya makao makuu ya chama chao
#statesmann Ingekuwa wewe ungechagua jela au ungelipa au ungeomba msaada wa pesa ili uachiwe?
 
Hamuelewi kuwa siasa ni mikakati na kuwa mmewapa CHADEMA Nafasi ya kujitangaza?
 
Interest,
watu wengine bhana mnachekesha sana yaani. Umeshawasikia wamesema imewabidi wanunue haki maana yake ni kwamba kwa mwenendo mzima wa kesi na yaliyozunguka nia ilishaonekana, hii ndio africa mkuu na kama unabisha subiri siku yekikufika utaielewa zaidi,...
 
Sioni ssbabu ya kuwa kila taasisi kuwa ni chanzo cha mapato, hata kama tunataka maendeleo ila sio kwa vyanzo hivi vya mapato, si busara mapato yatokane na polisi, mahakamani, faini za tra na Sumatra, kwa ni mapato hayo yanaongeza umaskini kwa unaowaletea maendeleo, pia taswira ya mahakama inaharibika kabisa, na shauri wakate rufaa uenda majaji wakatumia busara zaidi na kuipa mahakama taswira nzuri!
 
Wakate kwa nani ,kama mahakama nayo iko chini ya CCM .Watu wanachangishana hatutaki ujinga
 
Mtoa mada ipo hivi hukumu iliyotolewa leo haiwezi kutenguliwa kwa kusudio la mshtakiwa kukata rufaa!! Kisheria hukumu huwa inatekelezwa huku taratibu za rufaa zikiendelea!!

Hukumu ya awali itabatilishwa na hukumu ya mahakama ya juu zaidi kwenye shauri hilo!! Ndipo utekelezaji wa adhabu ya awali hukomea hapo
Je Kama mahakama ya juu ikitengua hukumu wakati wao wameshalipa fain watarudishiwa pesa waliyotoa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kulipa faini ni kukubali kosa, maana yake wamekutwa na jinai ivyo ubunge udiwani wasahau
Kukata rufaa ni process kama ilivyo process ya kuhukumiwa...
Hakimu kwa kutumia sheria aliwapa option ama kwenda jela miezi 5 au kulipa fine ...viongozi wamekubali kulipa fine ili wakwepe kwenda jela ..wakae uraian ...sheria haijakataza kwamba ukilipa fine huwezi kukata rufaa...
Suala la kukata rufaa linabaki palepale ...ni sawa wangeenda jela miezi 5 bado wangekata rufaa..lakini ukataji wa rufaa wakiwa gerezan huenda ungechukua muda mrefu zaidi hata baada ya kumaliza kufungo ,chukulia kesi imeendeshwa miaka miwili si rufaa itaenda miaka 4.
Kwa hiyo ni kheri walipe fine huku wakiendelea na shughuli zingine za kijamii.
 
Haijakubali kushindwa ila sisi ccm tunachanga tu......

Dkt. Mashinji kuchangiwa faini na chama (CCM)
 
Wanaweza kukata rufaa na huku tayari wamekwishalipa faini zao LAKINI rufaa yao ikikubaliwa na baadaye wakashinda kesi kila mmoja anaweza kurudishiwa fedha alizotoa kama faini.
Hivi ikitokea wakakata rufaa na ikakubaliwa kwa kushinda kesi, mahakama (serikali) itapaswa kuwarudishia fedha zao. Je, naweza kudai 2000 niliyochanga wanirudishie?
 
Mtoa mada ipo hivi hukumu iliyotolewa leo haiwezi kutenguliwa kwa kusudio la mshtakiwa kukata rufaa!! Kisheria hukumu huwa inatekelezwa huku taratibu za rufaa zikiendelea!!

Hukumu ya awali itabatilishwa na hukumu ya mahakama ya juu zaidi kwenye shauri hilo!! Ndipo utekelezaji wa adhabu ya awali hukomea hapo
Kitendo cha kukutekeleza hukumu hasa kwa faini ni prima facie kwamba umekubaliana na hukumu unequivacally ni sawa kwamba tayari amekwisha tumikia kifungo cha muda aliopewa pale ambapo hukumu inatolewa ina alternative hivyo hawezi kukata rufaa kwa kitu ambacho amekubaliana nacho kama kilivyo na kukubali kuilipa serikali garama ya uovu alioufanya. Kitu ambacho alitakiwa kufanya ni kutoa notice of appeal na ku omba bail pendaing appeal hapo ingeshika maji lakini hii rufaa ni sawa sawa na rufaa inayokatwa kwa mtu aliye plea kosa unequvacal. Otherwise wa appeal kwenye point of law not fact.
 
Kulipa faini ni kukubali kosa, maana yake wamekutwa na jinai ivyo ubunge udiwani wasahau

Aaah kwakweli elimu yetu ifanyiwe marekebisho..Kwani wameenda jera au wamefanya kosa la kukwepa kodi ?
 
Kulipa faini ni kukubali kosa, maana yake wamekutwa na jinai ivyo ubunge udiwani wasahau
Hata ukikata rufaa siyo kwamba unatoka mara moja. Pili wamepewa option mbili kufungwa au kulipa fine. Badala ya kukaa gerezani wakati rufaa yao inataka kusikilizwa bora walipe fine wakati rufaa yao inasikilizwa. Kipi kuwa nje na kukata rufaa au kuwa ndani na kukata rufaa? Kukata rufaa hakukupi uhuru wa kuwa nje ya gereza mpaka hapo utakapokuwa umeanza kusikilizwa rufaa yako na kuomba bail ya kuwa nje. Sasa jaribu kufikiri rufaa yako inaanza kusikilizwa baada ya miezi miwili, unataka muda huo uwe ndani?
 
Back
Top Bottom