Shinyanga: Viongozi wa CHADEMA Simiyu waliofungwa maisha waachiwa huru

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,628
218,059
FB_IMG_1668590125455.jpg


Huu ulikuwa ule ule unyama wa awamu ya 5 wa kuhakikisha viongozi wote wa Chadema wanafungwa jela .

Katala Kikaja na Lilanja Ng'hulima ambao ni viongozi wa Chadema huko Simiyu , Walikamatwa kubambikwa kesi ya uongo wakati wa Ulioitwa uchaguzi wa 2020 , Mahakama ya Mkoa wa Simiyu ikawahukumu Kifungo cha maisha jela .

Baada ya Chadema kukata rufaa , leo Wameachiwa huru na Mahakama ya Rufaa mjini Shinyanga baada ya kuonekana hawakuwa na hatia yoyote na kwamba walifungwa kwa matakwa ya viongozi wa CCM. Wahanga hao tayari Wametumikia kifungo hicho feki kwa muda wa miaka miwili

Hii Nchi ilipofikia hakuna haja ya Kuiombea Dua .

--

Makada hao walifungwa jela maisha kesi iliyotokana uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.

Mwanza. Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga imewachiwa huru makada wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Katala Kikaja na Ng'hulima Lilanga waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya wizi, unyang'anyi wa kutumia silaha na ubakaji.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Novemba 16, 2022 na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Athuman Matuma baada ya kuridhika na hoja za warufani kuwa ushahidi uliowatia hatiani Aprili 12, mwaka huu, ulikuwa dhaifu, unaotia mashaka na usiokubalika mbele ya macho ya sheria.

Wana Chadema walitiwa hatiani kwa makosa mawili ya wizi, ubakaji, kuharibu mali na unyang’anyi wa kutumia silaha baada ya kukamatwa wakiwa kituo cha kupigia kura Kata ya Dutwa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu walikokuwa mawakala wa wagombea wa chama hicho kikuu cha upinzani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.

Pamoja na wizi wa Sh300, 000, warufani hao kwa pamoja walidaiwa kumbaka msadizi wa kituo cha kupigia kura ambaye jina lake lilihifadhiwa kulinda utu na heshima yake mbele ya jamii.

Tangu walipokamatwa siku ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020, kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo Aprili 12, mwaka huu, warufani hao wamekaa mahabusu na gerezani kwa takribani miaka miliwi na miezi mitatu kutokana na shitaka la unyang’anyi wa kutumia silaha ambayo ni moja ya mashtaka yaliyokuwa yanawakabili kutokuwa na dhamana.

Hadi kuachiwa huru leo, warufani hao wametumikia takribani miezi saba ya adhabu yao katika magezeza ya Bariadi, Shinyanga na Butimba jijini Mwanza.

Mwananchi digital


Uchambuzi....

Katala Kikaja na Ng'hulima Lilanga walikua mawakala wa Chadema kwenye uchaguzi mkuu 2020, kata ya Dutwa, Wilaya Bariadi mkoani Simiyu. Usiku wa 27 Oktoba 2020 walipewa vitisho na viongozi wa CCM kwamba wasiende kusimamia kura za Lissu, kwa sababu wanataka JPM ashinde kwa 100% eneo hilo.

Wakapuuza vitisho hivyo. Oktoba 28, 2020 waliwahi vituoni alfajiri, mmoja akisimamia Dutwa A na mwingine Dutwa B. Wakiwa hapo walisikia taarifa kuwa kuna mawakala wamezuiwa kuingia vituoni na wengine wameingia lakini wakatolewa kwa nguvu na polisi.

Lakini wao wakaendelea kubaki vituoni, wakisubiri zoezi la kupiga kura lianze. Ghafla wakaja polisi wenye silaha ambao walitumia nguvu kuwatoa na kuwafunga pingu. Wakapelekwa kituoni bila kuwaeleza kosa lao. Uchaguzi ukamalizika na matokeo yakatangazwa wakiwa bado rumande.

Mwezi mmoja baadae wakapandishwa kizimbani kwa tuhuma za ubakaji na unyang'anyi wa kutumia silaha. Wakastaaajabu sana. Wakajiuliza wamembaka nani? Lini na wapi?

Hati ya mashtaka ikaeleza kuwa alfajiri ya 28 October 2020 walipoenda kituo cha kupiga kura, walimkuta msimamizi msaidizi wa uchaguzi, ambaye walimbaka kwa zamu, kisha wakampora pesa taslimu TZS 300,000/=. Baada ya kufanya tukio hilo wakabaki kama mawakala wa Chadema wakisubiri kusimamia kura.

Jambo la ajabu hati ya mashtaka haikumtaja huyo aliyebakwa wala hakuitwa mahakamani kutoa ushahidi. Aliwasilisha ushahidi wake kwa maandishi kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kumlindia utu wake. Mahakama ya Hakimu Mkazi Bariadi ikawahukumu KIFUNGO CHA MAISHA JELA.

Baada ya kusota jela kwa miaka miwili, wakakata rufaa. Hatimaye leo Mahakama Kuu kanda ya Shinyanga imewaachia huru. Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Athuman Matuma amesema ushahidi uliowatia hatiani ulikuwa DHAIFU, UNAOTIA MASHAKA na USIOKUBALIKA KISHERIA.

Miaka miwili ya mateso, miaka miwili ya kupakaziwa kesi, miaka miwili ya kutumikia adhabu bila hatia. Kama si kukata rufaa vijana hawa wangemalizia maisha yao yote gerezani na kuacha familia zao zikiteseka. Na dunia nzima ingewahukumu kama majambazi na wabakaji 😭 maana mahakama ilishawa-label hivyo. Hivi ndivyo serikali ya awamu ya 5 ilivyosaidia kuimarisha Demokrasia nchini. Subhanallah.!
FB_IMG_1668590125455.jpg
FB_IMG_1668612796420.jpg
 
Back
Top Bottom