Michael Augustine Lukindo


Nani yupo nchi za watu?

Au una hamu tu ya kuwapaka waishio nchi za watu?

That's too imbecilic!!!
 
Mkuu kuna tangazo limekuja hapa foreign affairs kutafuta ndugu toka kwa mkewe ni serious watanzania wa mbele wanatia aibu

Wewe ni mfanyakazi wa foreign affairs? If so, you are so judgmental, full of assumpions, prejudicial and unprofesional.

Fanya kazi yako kwa weledi hata kama unawahudumia wanatia aibu. Otherwise, unaidhalilisha hata hiyo foreign affairs.
 
Nani kaji appoint?

Ili iweje? Tatizo umelichukulia hili suala langu binafsi ndo maana huelewi lolote...

Haya kila kheri ktk kutafuta will ya Lukindo....

Unapojivika jukumu la kutafuta ndugu wa marehemu bila kujua marehemu ametakaje unaji appoint kuwa msaidizi wa marehemu, bila kujua alitaka nini.

Nimelichukuliaje hili kama suala lako binafsi kwa kutaka kujua kama kuna will na marehemu alitaka nini kuhusu kuhusisha ndugu zake? How is that "kulichukulia hili suala lako binafsi"?

Unajuaje kwamba nahitaji kila la heri na si kila la shari?
 


Hivi ukiwa ofisini ukaletewa suala ulishughulikie ni kuji appoint?

Unaelewa kweli?

Sijui unalotaka kati ya la kheri au la Shari mi nimekutakia la kheri ni uamuzi kulikubali kulikataa ukataka la Shari...

Kuendelea kubishana hapa haitasaidia kitu muhimu ndugu wa marehemu wapatikane hayo mengine yakwako..
 
Wewe ni mfanyakazi wa foreign affairs? If so, you are so judgmental, full of assumpions, prejudicial and unprofesional.

Fanya kazi yako kwa weledi hata kama unawahudumia wanatia aibu. Otherwise, unaidhalilisha hata hiyo foreign affairs.

Mkuu kama ungesikia mambo ya baadhi ya watanzania wenzetu huko nje ndo ungejua namaanisha nini...

Tukienda kwenye mikutano huko mtu unajisikia aibu badala ya wao

Inasikitisha...
 
Nani yupo nchi za watu?

Au una hamu tu ya kuwapaka waishio nchi za watu?

That's too imbecilic!!!

Oh kumbe uko bongo ndo maana unafanya kazi kibongo kibongo?

Hapa bongo professionalism doesn't matter anyway. Ili mradi liende.

Ingekuwa mtu wa uraiani kaandika uliyoandika sawa lakini wewe unasema uko foreign affairs hata office manners huna?

Unaandika kutokea foreign office as if upo bar?
 
Mkuu kama ungesikia mambo ya baadhi ya watanzania wenzetu huko nje ndo ungejua namaanisha nini...

Tukienda kwenye mikutano huko mtu unajisikia aibu badala ya wao

Inasikitisha...

Mie huwa nasoma na kuona mapicha mara nyingi mnapoenda huko mnaenda kufungua matawi ya vyama vya siasa.
 
Mie huwa nasoma na kuona mapicha mara nyingi mnapoenda huko mnaenda kufungua matawi ya vyama vya siasa.

Inawezekana wenyewe hawaoni Aibu ila kwa uso wangu uloumbwa na haya huona aibu sana....
 

Hivi kibaya nilichoandika hapo ni kipi?

Shutuma zote zanini?
 
Hivi kibaya nilichoandika hapo ni kipi?

Shutuma zote zanini?

Rudi nyuma soma posts zako zote, zikiwemo zile ambazo umefuta (thanks to Kiranga kaziquote zote) then reflect kama mwajiriwa aliyeajiriwa na foreign affairs kutumikia watu regardless ya matatizo yao anaweza kuandika kama ulivyoandika.

Ingekuwa nchi za watu kesho asubuhi ushafukuzwa kazi wewe. You lucky unaweza kuandika ulivyoandika and managdm to gdmt away with it.
 
Last edited by a moderator:

Hongera kuchangia thread hii...
 
Inawezekana wenyewe hawaoni Aibu ila kwa uso wangu uloumbwa na haya huona aibu sana....

May be you see the same people every time you go abroad.

Sidhani kama watu walio bize na kazi zao wana huo muda wa kuhudhuria hafla za kufungua matawi ya vyama vya siasa.

By the way, we need cofident people in the foreign affairs na siyo watu wenye haya sijui aibu.

Siyo mnaenda kusgn mikataba ya kimataifa huko bila hata kuuliza kisa eti mna nyuso za haya au mnaona ni aibu kuuliza.
 
Kulikuwa na ugumu sana wa kuchangia kwenye hii thread?

Pamoja na kutembea kote huko nje kama unavyodai lakini huna hata manners za kiofisi?

I just hope that foreign affairs hajajaa unprofessional people kama wewe.


Nimekudharau sana
 
Hivi ukiwa ofisini ukaletewa suala ulishughulikie ni kuji appoint?

Hapana ila unatakiwa ushughulikie hilo suala in a professional manner bila kuanza kukandia mwenye tatizo.

Unatakiwa usiwe judgmental, prejudicial au kufanya assumptions.

Hakuna ubaya wa mtu yoyote kuwa judgmental or prejudicial. These are natural things for every human being to have.

Tatizo ni pale unapozitumia au kuzionyesha hizi tabia kwenye kazi zako za kuhudumia watu kama ulivyofanya kwenye hili suala.

If you serving people in an official capacity then keep your assumptions, prejudice, etc to yourself.

Otherwise, next time hakuna atakayekuletea tatizo mezani kwako ulishughulikie.
 
Nimekudharau sana

Kwani kabla ya hapo ulikuwa unanipenda sana eh?

Sijawahi kukupigia goti hata siku moja kukuomba unipende.

Neither I am here to please or amuze you ili usinidharau.

Pia sitapungukiwa na chochote kutokana na wewe kunidharau.

Ila nitakwambia fanya kazi bila kubagua watu na matatizo yao. That is what you were employed to do.

Whether unayemhudumia hajawasiliana na ndugu zake kwa miaka 30 au mwezi mmoja is not for you to judge unless kama mna kitengo adjudication hapo foreign affairs.
 

Michael Augustino Mwaimu Lukindo pichani Enzi za uhai wake.




Kama unafununu au kujua lolote kuhusiana na ndugu yetu huyu unijulishe mimi naitwa Lugome Fautus email yangu ni g5state@yahoo.co.uk . Lengo nikuweza kuwafahamisha ndugu zake nyumbani Tanzania na popote pale walipo. Source: LUKAZA

Wana Jamiiforums pamoja na mapungufu yote ya kibinadamu tusaidiane ndugu, familia na marafiki wa Michael Lukindo wapate habari hizi za msiba
 
EMT na lusungo ,

Kwanza kwako Lusungo:
Wewe ndiyo unatia KINYAA kwa kuwa mhudumu wa Watanzania na unapata habari za mtu na unaanza kuongeza za kwako. Kama huyu jamaa ulikuwa humfahamu, kwa nini unaanza kumhukumu? Unajua kichwani mwake kulikuwa na madudu gani yanachemka hadi akasahau au kukata mawasiliano kwao? Unajua ndugu zake walimfanya nini hadi akaacha kuwasiliana nao? Kama alikuwa Yatima je aliyelelewa na Masister wa Kikatoliki?

Hata kama wana maisha mabaya, acha wawe. Kama hadi amekufa hajaja kwako kuomba fedha, mwache. Kama una huruma sana na Watanzania, mbona wapo wengi tu hapa Tanzania wana hali mbaya zaidi ya hao Wavaa jezi walioko USA? Au Walevi walioko Russia? Acha hiyo Mkuu. Sababu zinazopelekea mtu asiwe na mawasiliano kwao ni nyingi. Si kawaida mtu kufanya hivyo na akifanya, usirukie kumhukumu. Usihukumu, na wewe utakuja kuhukumiwa.

Kwako MTM:
Mkuu, na wewe unaleta mambo ya Kibongo bongo. Kama umeowa au kuolewa nchi za wenzetu, mwenye amri ya mwisho anabaki Mkeo/Mmeo na kama siyo Mkeo/Mmeo basi Watoto kama wamemaliza miaka 18. Sidhani aliyeleta hii habari kama alivyoandika kuwa wamepata maombi kutoka kwa Mkewe, wanaelewa matakwa ya Marehemu ilikuwa ikisema nini. Huwezi kumvamia Mwanamke wa USA au Ulaya na kuanza kudai, je Mumeo alidai iwe hivyo? Mambo ya matakwa ni mambo ya kifamilia na kama Mkewe anavunja, basi ni Mkewe anavunja na dhambi hiyo ataibeba yeye.

Hata kama aliandika, inaweza kuwa dakika ya mwisho, jamaa aliomba ndugu zake wajulishwe na Mkewe sasa kaanza kutafuta ndugu wajulishwe.

Ila nakubaliana na wewe kuwa Lusungo angeishia kutafuta ndugu tu wa Marehemu, akipata tuseme simu au sanduku la barua, basi wamjulishe Mke wa Marehemu na mengine yote wamuachie yeye. Labda aombe tena Ndugu wajulishwe kuwa Lukindo amefariki. Haya ya miaka 30, maisha mabaya blaa blaa, hayamhusu.
Anyway, nilishawahi kukutana na watu kadhaa wa aina hiyo. Si kuwa wana maisha mabaya, la hasha, wana maisha mazuri mno. Wanaishi maisha ya Wastani kwa Ulaya ambayo kwa Africa, ni wachache wanaishi. Ila na wao wamekaa miaka kibao na hawana mawasiliano na ndugu. Si kuwa ndugu hawafahamu anapoishi, hapana. Wanapafahamu, wana simu zao, wameshafika wanapoishi ila ghafla jamaa wanaamua kukata mawasiliano moja kwa moja na ndugu zake wote. Mmmoja mwisho amemalizia hata kukata Mawasiliano na Mkewe na Watoto wake. Sasa huyu utasema DARINI kwake kweli kumekaa sawa?
 
Mkuu kama ungesikia mambo ya baadhi ya watanzania wenzetu huko nje ndo ungejua namaanisha nini...

Tukienda kwenye mikutano huko mtu unajisikia aibu badala ya wao

Inasikitisha...


Ukienda nje kwa watanzania una kiingereza cha kuongea ukaeleweka? Ni wewe unasikitisha au wao? Kwanza ukiongea wala hutaeleweka unaongea nini labda upewe karatasi uandike iwapo Rais wako Kikwete hushindwa na kuamua kuongea Kiswahili utaweza? Ndio maana unahate sana dual citizenship sababu ya kuonea wivu watu wa nje wala usiwasikitikie wao wanawasikitia watanzania ambao wanaburuzwa na CCM na kuishi kimasikini sana huku wakubwa wakikwapua mabilioni feel sorry to many Tanzanians back home who live in poverty and hunger rather than Tanzanians living abroad
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…