Miaka niliyoishi si haba

Miaka michache iliyopita nilibahatika kutembelea America, Washington State.

Washington huwa kuna baridi, na siku niliyofika ndio usiseme, ilikuwa baridi sana😱, bahati mbaya nikawa na kikohozi huku nikiwa najisikia na kahoma fulani hivi. Haikuni simamisha kutaka kutoka na kuona mji.

Hatahivyo kama kawaida nikameza dawa yangu Panadol, na huyo nikaingia Mtaani💪 Nikaingia kwenye mgahawa nikavuta kigoda na kuagizia 'Tea' na uzuri nikaona "Chai Masala" kwenye menu, nikagusa tu kuashiria ndicho nilichokuwa nahitaji pale. Nilipata chai yangu, taratibu nikaanza kunywa napepesa pepesa, ghafla, nikapiga chafya, wakaniambia 'Bless you' na kwa ukarimu nikaitikia tu, 'sank you' huku mmoja wa nilio kaa naye karibu kwenye vigoda akasema 'I hope its not a cold' nikaitikia tu 'yes', 'its very cold' (sikuwa nimeelewa vizuri) Haikuishia hapo, mzee mmoja wa makamo akanisogelea na kuninong'oneza, alisema ' In Washington State, it is illegal to walk around in public if you have a common cold' hapo ndiyo ilikuwa Aha💡🤔 moment yangu, kumbe, "Common cold" Yaani akimaanisha Homa ya mafua.
Aloo,nilishikwa na butwaa, nikasimama taratibu na kuondoka kurudi hotelini, ka mwendo hivi, kwa miguu, ka dakika tano sita tu lakini njiani kila nikiona Polisi naomba nisipige chafya nikakamatwa kwakuwa na homa ya mafua.😪🤒

Wacheni. Duniani kuna mambo, na nimeona na kusikia mengi, lakini haya ya huyo Bro wetu Mshana Jr, Aloo ni ya kufikirisha🤯 zaidi.
 
In Washington State, it is illegal to walk around in public if you have a common cold' hapo ndiyo ilikuwa Aha[emoji362][emoji848] moment yangu, kumbe, "Common cold" Yaani akimaanisha Homa ya mafua.[emoji1][emoji1]
 
Nmeona meanasiasa akikataza kuchanganya dini na siasa akisema hayo katika jukwaa la dini.

Pia meanasiasa huyo aliwahi Apa kwakutumia kitabu Cha DINI kutekeleza shughuli zake za kisiasa.
 
Nimeona mke wa mtu akilia kwa usaliti kwa mume wa mtu ambaye sio mumewe na kuapa kumkomesha kisa Ana mwanamke mwengine zaidi yake [emoji119][emoji28] (unaweza ukahisi status ni za mume wake kumbe ni za mume wa mtu mwengine)
 
Kwa utoto wangu huu nami nimeona vichache pia. Nimeona marafiki wazuri wakiwa msaada mkubwa kwa mtu na ndugu wa damu wakiwa liability na maumivu kwenye maisha ya mtu.

Nimeona ndugu wakisubiri mtu afe kwa madai ya kwamba ameoza kabisa na huku pesa za michango ya msiba kupatikana haraka wakati pindi ndugu yao yuko hai pesa ya matibabu ilikua ya tabu.

Nimeona watu wakichangishana kwa tabu hela ya msiba na mambo ya kusafirisha huku hao hao wanapofika kwenye transit stations ndio wanunuaji wa bia na nyama choma kwa wingi lakini hela ya michango its a no kwao.

Nimeshuhudia ndugu wakimuacha mwanaume aliewasaidia kipindi cha pesa nyingi kwa kuwasomesha ama kuwapiga tafu lakini kwenye shida inabakia mke na watoto kupambana na hali zao huku watoto wakipiga simu wanapewa bonge la block.
Nimezoom wake za viongozi wa dini mbalimbali wakitafuta suluhisho za ashki zao nje ya ndoa huku wakiwa viongozi wa wanawake wenzao na masuala ya kifamilia ndani ya taasisi za dini zao.

Nimeona waliokufa na njaa, kukiwa na masufuria makubwa kwenye misiba yao kwa madai ya "sherehe ya mwisho ya marehemu."
Nikaona meza zikipinduka nyakati flani flani kwenye maisha ya mwanadamu. Unakuta aliyekuaga juu anashuka chini rapidly huku aliyedharaulika akipanda juu in a moment..kimbembe itokee katika ofisi.

Maybe bado sijaona...Mungu anipe uzima kuyaona mengine pia.
 
Kasie naona umekuwa wa baridi siku hizi kunani? Au sie huyu kasie mahaba matata tunaemjua?[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Maybe bado sijaona...Mungu anipe uzima kuyaona mengine pia[emoji419][emoji375]
 
NIMEONA;

Jambazi mbobevu akiwa mtoa mfano mzuri jinsi Jambazi mwenziye anavyopaswa kuuwawa kwa kipigo kizito.

Mcha Mungu kupita kiasi akiwa ndiye kungwi wa ufisadi, uzinzi, uchawi, uuzaji wa madawa ya kulevya, ukwepaji kodi, ubinafsi, ujambazi na hata utapeli,

Anayethamini zaidi maisha (nyumba, gari na milki za kifahari) kuliko kuishi (akijinyima kula na kupatwa vidonda vya tumbo) na kujitibu kwa gharama zaidi bila kuinjoyi pesa zake au asiishi kabisa kwenye nyumba aliyojenga kwa kufariki.

Mzee akijisifu kwenye mazishi kuwa Rafiki zake, Ndugu zake na Jamaa zake waliishi pamoja eneo flani, na wengine walimkuta hapo hapo akiishi ila wote walifariki na kumwacha yeye pekee akidunda ilihali naye ni Marehemu Mtarajiwa.
 
Mimi nimeona Kuishi ni Leo Jana na kesho haipo tena. na nikaona hakuna miaka Kuna siku tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…