Nimeona mengi, wewe umeona nini?

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Ingawa miaka nilioishi duniani inahesabika kwa urahisi lakini walau naweza kusema nimeona mengi. Nimeona daktari akiumwa saratani ya koo kwa ajili ya matumizi ya vitu anavyokataza wengine.

Kisha nikamuona wakili aliyehukumiwa kwenda jela kwa kosa la kudhulumu mali za yatima na wajane.

Halafu nikapata ile habari yenye maumivu, habari iliyonitoa machozi na kunipa simanzi ya moyo. Kwamba rafiki yangu ambaye ni tabibu wa akili naye kajiua kwa msongo wa mawazo.

We umeona mangapi? Nimeona tabasamu kwa mtu aliyepaswa kulia, halafu nikaona maumivu katika kicheko cha mtu aliyesalitiwa.

Ukiona mtu anakupa faraja, nenda kafanye ibada, kwa kuwa haina maana kila kitu kwake kiko sawa, ila anajali hata akaamua kugawa tawi la kivuli chake katika msiba wa hisia zake.

Maisha sio yale uliyofikiri, maisha ni haya ambayo hesabu zako za shule zinakataa kujaza jedwali la upendo lililo wazi.

Kitu gani umewahi kuona? Ukitaka imani yako iwe na dosari, basi anzisha urafiki na kiongozi wa dini.

Nimeshuhudia vita katika nyumba ya balozi wa amani. Kisha nikaona uongo na ulaghai katika nafsi zilizoapa na kutii.

Halafu nikaona upendo katika sura ya kahaba, halafu baadaye nikashangazwa, nikaoneshwa ukahaba Katika sura ya aliyeitwa muumini.

Ndipo nikaamua kukubali, kuwa tukiamua kuhesabu vya kila mtu hesabu zetu daima hazitofika mwisho.

NB: it's not always easy but that's life.

Ameandika Ibrahimu Mwiru
 
Nimeona balozi wa nyumba 10 ameamua ugomvi wa wana ndoa na kumuambia mume amuache mke wake kwake mpaka kukuche kwanza, halafu balozi hana mke

Nimeona jamaa aliepelekwa mortuary baada ya daktari kuhakiki kuwa amekufa anatoka kwenye chumba cha kuhifadhi maiti

Nimejiona nikijizika mwenyewe kwenye vita ili adui asinione na wakapita nikatoka zangu FACT

Kila mmoja amekutana na mengi na mengine tutakufa nayo hatusemi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom