Ngorunde
Platinum Member
- Nov 17, 2006
- 5,499
- 11,595
Ukweli uliosimama." ukitaka imani yako iwe na dosari basi anzisha urafiki na kiongozi wa dini" .. hii ni sahihi for 100 percent
Ukweli uliosimama." ukitaka imani yako iwe na dosari basi anzisha urafiki na kiongozi wa dini" .. hii ni sahihi for 100 percent
In Washington State, it is illegal to walk around in public if you have a common cold' hapo ndiyo ilikuwa AhaMiaka michache iliyopita nilibahatika kutembelea America, Washington State.
Washington huwa kuna baridi, na siku niliyofika ndio usiseme, ilikuwa baridi sana, bahati mbaya nikawa na kikohozi huku nikiwa najisikia na kahoma fulani hivi. Haikuni simamisha kutaka kutoka na kuona mji.

moment yangu, kumbe, "Common cold" Yaani akimaanisha Homa ya mafua.

Adhabu haiendani na kosa, ni kubwa sana, futa hayo mawazoNikikumbuka jirani nimemtegeshea shoti!!
Ana tabia ya kuja kukojoa kwenye bustan yangu siku....
Nataka nimfanye asidinde tena.......
Ngoja nifikirie kwanza !!!!
Hebu nitakuja huko tutete
Anakwambia fuata ninayosema, si ninayofanya...Nmeona meanasiasa akikataza kuchanganya dini na siasa akisema hayo katika jukwaa la dini.
Kasie naona umekuwa wa baridi siku hizi kunani? Au sie huyu kasie mahaba matata tunaemjua?Mshana, on a serious note, mimi huyo mkaka tuu anayeimba na hiyo kofia yake.
Mwambie nimemuelewa hasa hizo ndevu. Sema tuu ana mtu wake tayari ila ningemfungia safari hadi huko aliko, mie ni mapendo daima tuu hakuna la ziada.
Back to the topic, nimeona mtoto chini ya miaka 10 ana busara kuliko wazazi wake kiasi cha kuongea na mchungaji namna aongee na wazazi wake waache mabishano kwani hayuko tayari kulelewa mtoto wa kambo na wao wanaendekeza starehe zao.



Oh una utani na MsukumaNimeshuhudia Mtu aliyeishia La Saba Akiitwa Dokta(Doctorate)
Hizi zipo nyingi sanaMi nmeona mpangaji akinunua nyumba aliyopanga, afu akampangishia aliekuwa mwenye nyumba.
Maybe bado sijaona...Mungu anipe uzima kuyaona mengine piaKwa utoto wangu huu nami nimeona vichache pia. Nimeona marafiki wazuri wakiwa msaada mkubwa kwa mtu na ndugu wa damu wakiwa liability na maumivu kwenye maisha ya mtu.
Nimeona ndugu wakisubiri mtu afe kwa madai ya kwamba ameoza kabisa na huku pesa za michango ya msiba kupatikana haraka wakati pindi ndugu yao yuko hai pesa ya matibabu ilikua ya tabu.
Nimeona watu wakichangishana kwa tabu hela ya msiba na mambo ya kusafirisha huku hao hao wanapofika kwenye transit stations ndio wanunuaji wa bia na nyama choma kwa wingi lakini hela ya michango its a no kwao.
Nimeshuhudia ndugu wakimuacha mwanaume aliewasaidia kipindi cha pesa nyingi kwa kuwasomesha ama kuwapiga tafu lakini kwenye shida inabakia mke na watoto kupambana na hali zao huku watoto wakipiga simu wanapewa bonge la block.
Nimezoom wake za viongozi wa dini mbalimbali wakitafuta suluhisho za ashki zao nje ya ndoa huku wakiwa viongozi wa wanawake wenzao na masuala ya kifamilia ndani ya taasisi za dini zao.
Nimeona waliokufa na njaa, kukiwa na masufuria makubwa kwenye misiba yao kwa madai ya "sherehe ya mwisho ya marehemu."
Nikaona meza zikipinduka nyakati flani flani kwenye maisha ya mwanadamu. Unakuta aliyekuaga juu anashuka chini rapidly huku aliyedharaulika akipanda juu in a moment..kimbembe itokee katika ofisi.
Maybe bado sijaona...Mungu anipe uzima kuyaona mengine pia.


Mimi nimeona Kuishi ni Leo Jana na kesho haipo tena. na nikaona hakuna miaka Kuna siku tuWalau naweza kusema nimeona mengi. Nimeona daktari akiumwa saratani ya koo kwa ajili ya matumizi ya vitu anavyokataza wengine.
Kisha nikamuona wakili aliyehukumiwa kwenda jela kwa kosa la kudhulumu mali za yatima na wajane.
Halafu nikapata ile habari yenye maumivu, habari iliyonitoa machozi na kunipa simanzi ya moyo. Kwamba rafiki yangu ambaye ni tabibu wa akili naye kajiua kwa msongo wa mawazo.
We umeona mangapi? Nimeona tabasamu kwa mtu aliyepaswa kulia, halafu nikaona maumivu katika kicheko cha mtu aliyesalitiwa.
Ukiona mtu anakupa faraja, nenda kafanye ibada, kwa kuwa haina maana kila kitu kwake kiko sawa, ila anajali hata akaamua kugawa tawi la kivuli chake katika msiba wa hisia zake.
Maisha sio yale uliyofikiri, maisha ni haya ambayo hesabu zako za shule zinakataa kujaza jedwali la upendo lililo wazi.
Kitu gani umewahi kuona? Ukitaka imani yako iwe na dosari, basi anzisha urafiki na kiongozi wa dini.
Nimeshuhudia vita katika nyumba ya balozi wa amani. Kisha nikaona uongo na ulaghai katika nafsi zilizoapa na kutii.
Halafu nikaona upendo katika sura ya kahaba, halafu baadaye nikashangazwa, nikaoneshwa ukahaba Katika sura ya aliyeitwa muumini.
Ndipo nikaamua kukubali, kuwa tukiamua kuhesabu vya kila mtu hesabu zetu daima hazitofika mwisho.
Angel NylonView attachment 2724878