Miaka mitatu michungu mtaani

Miaka mitatu michungu mtaani

YATC

Member
Joined
Jan 21, 2015
Posts
77
Reaction score
19
Wana jukwaa habari...nina miaka mitatu sijapata kibarua...nimeanza kupanick...nimejaribu kila njia kutafuta kazi, omba sana matangazo mbali mbali, mpaka ela ya bundle application, kufanya certification vyeti nauli za kuzunguka zinanipiga chenga, ombi langu msaada hata kujitolea sehemu nina Bach in Finance, sichagui kazi! Nimetamani na kujaribu kujiajili ila kama ilivyo kawaida kwa watanzinia wengi mtaji umekua kikwazo. Nakaribisha mawazo pia kama kuna sehemu nina kosea nirekebishe Natanguliza shukrani
 
Daah kaka sina la kusema sana ila Nakushi.tu uskate tamaa Inshalaah mwenyezi Mungu Akusimamie utapata Kazi tu kaka!!!
Ila kama unajaribu ku apply kazi mitandaoni jaribu ku apply moja kwa moja kwa kutuma maombi kweny emailz na website zao istumie watu kama kina zoom ni wazushi tu..endelea kutembelea mitandao pia
Www.ajirazetu.co.tz
Www.utumishi.co.tz
Kwa watu wa Finance na Accounts hua naona ona wanaotajika sana..jaribu kaka!!
 
na vyuo vinatema tena mwezi wa sita..kaz ipo..!
 
YATC
Duuih!! Pole sana ndugu, kikubwa usikate tamaa ila nikushauri jambo kwa kukupa mfano.

Nina shem wangu nae alikaa kitaa sana akizunguka huku na kule kutafuta kazi. Nilimpa mbinu mbili moja ni kusoma post graduate diploma au kujitolea kufanya kazi.

Aliamua kujitolea, nilimuelekeza mashirika makubwa ya kujitolea ili kuupata mfumo wa juu kabisa ili uweze kupata kazi katika mashirika ya chini. Mfano ukijitolea Ewura ni rahisi kwako kupata kazi Tanesco na idara za maji zote za mikoa yote pia mashirika ya gesi! Sababu kubwa ni kwamba yapo chini ya Ewura na ule mfumo wote utakuwa umeujua, upo ndugu. Hapo nafasi ni kubwa kwako kupata ajira kwa mashirika mbali mbali sababu kubwa ile inferiority itakuwa imekutoka.

Itakuwa ngumu kwako kutoka Dawasco au Moruwasa kupata kazi kwenye mashirika ya kitaifa.

Believe it yule shem baada ya miezi saba ya kazi amekula shavu nono mpaka inatia hasira! Pata picha alikaa mtaani zaidi ya miaka miwili na kajitolea miezi saba akala shavu, kwa nini wewe??

Kikubwa angalia na shirika la kujitole coz kuna mashirika hata ufanye nini cha ajabu ukaweka kwenye CV hupati kazi!! Kila la heri ndugu
 
Last edited by a moderator:

mkuu nimeomba sana kujitolea...lakin sito kata tamaa ntaendele asante kwa ushauri
 
Last edited by a moderator:
Pole sana,mimi mwenyewe jobless ila ipo siku mungu atatusaidia,funga,omba utaona matokeo yake.
 
omba hata nafasi za f6 uhamiaji,au zimamoto wanazotangazaga unaweza tokea huko amini usiamini mm nlifit mwaka na nusu na nlikua na kigugumizi jenga picha kwenye interview nlivyokua napata shda ila sikukata tamaa nlifanya aplications kama 150 na interview 15.,ambayo nlifanikiwa ilikua ya 16..,japo ma hr wengi walikua wananzarau na kunkeje5i ila sikukata tamaa, mwezi october 2014 nlipata kazi nzuri tena serikalini..,ila sitowasahau erolink,spanco,icon na wengne wengi walivyokua wakinyima kazi eti kwa kua nna kigugumizi....MUNGU awasaidie wote wanaotafuta kazi bila kukata tamaa
 
Mimi nilimaliza Chuo mwaka 2011 nimekuja kupata kazi december 2014, so usikate tamaa nduguyangu Mungu atakusaidia milango itafunguka
 
Pole sana ndg.
Jaribu kusomea ualimu mkuu unaweza baadae ukawa mwalimu na mhasibu hapo apo chuoni au secondari.
 
Pole sana Mkuu ila usikate tamaa humu pia kunawekwa matangazo ya ajira mbali mbali jitahidi uwe unayaangalia na kutuma maombi mengi kadri unavyoweza. Pole sana Mkuu na kila la heri katika kutafuta kwako ajira..
 
Daah kaka sina la kusema sana ila Nakushi.tu uskate tamaa Inshalaah mwenyezi Mungu Akusimamie utapata Kazi tu kaka!!!
Ila kama unajaribu ku apply kazi mitandaoni jaribu ku apply moja kwa moja kwa kutuma maombi kweny emailz na website zao istumie watu kama kina zoom ni wazushi tu..endelea kutembelea mitandao pia
Www.ajirazetu.co.tz
Www.utumishi.co.tz
Kwa watu wa Finance na Accounts hua naona ona wanaotajika sana..jaribu kaka!!

www.ajira.go.tz
www.utumishi.go.tz
 
Pole sana ndg, lkn hupaswi kukata tamaa wala kupanic. Kuwa na subira, ongeza bidii katika utafutaji, na jaribu kubadili mbinu zako za utafutaji.
 
Inatilisha uchungubunapowaza wengine watahitimu soon bdo we hata pa kujishikiza huna,pole sana nakushaur usikate tamaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom