So, unaomba pia unakosa! Au inakuwaje??
Pole sana ndg yangu. Tupia namba ya simu tuongee
Kuna kazi wametangaza advans bank deadline tar 2 february 2015 post ni finance assistant....
Jiajirini mtaota mvi na vibahasha vyenu mkononi
omba hata nafasi za f6 uhamiaji,au zimamoto wanazotangazaga unaweza tokea huko amini usiamini mm nlifit mwaka na nusu na nlikua na kigugumizi jenga picha kwenye interview nlivyokua napata shda ila sikukata tamaa nlifanya aplications kama 150 na interview 15.,ambayo nlifanikiwa ilikua ya 16..,japo ma hr wengi walikua wananzarau na kunkeje5i ila sikukata tamaa, mwezi october 2014 nlipata kazi nzuri tena serikalini..,ila sitowasahau erolink,spanco,icon na wengne wengi walivyokua wakinyima kazi eti kwa kua nna kigugumizi....MUNGU awasaidie wote wanaotafuta kazi bila kukata tamaa
aisee na sisi bado tunamwagwa mwezi wa sita!
kwani ukimwaga ndo unakuja chukua kitengo mkuu, jiandae kisaikolojia huku ni zaidi ya udhaniavyo.
zipompakwani ukimwaga ndo unakuja chukua kitengo mkuu, jiandae kisaikolojia huku ni zaidi ya udhaniavyo.
hahahahha yaani nkuonee wivu, sikujui unijui utakuwa na matatizo mkuuzipompa
yani umekurupuka vibaya sana kijana, post yangu imeendana wazi na janga la mleta uzi, wewe kwa fikra zako za wivu umeona mimi kusema ''na sisi tunamwagwa mwezi wa sita umeona labda nimesema mwezi wa sita napata kitengo bandari'' mkuu usipanik, maisha ndo haya haya!
Wana jukwaa habari...nina miaka mitatu sijapata kibarua...nimeanza kupanick...nimejaribu kila njia kutafuta kazi, omba sana matangazo mbali mbali, mpaka ela ya bundle application, kufanya certification vyeti nauli za kuzunguka zinanipiga chenga, ombi langu msaada hata kujitolea sehemu nina Bach in Finance, sichagui kazi! Nimetamani na kujaribu kujiajili ila kama ilivyo kawaida kwa watanzinia wengi mtaji umekua kikwazo. Nakaribisha mawazo pia kama kuna sehemu nina kosea nirekebishe Natanguliza shukrani