Miaka 8 bila kazi, tangu nimalize chuo kikuu

Miaka 8 bila kazi, tangu nimalize chuo kikuu

Elimu ni Kwa manufaa yako ndugu yangu. Pambana Kwa ajili ya kesho yako. Ajira yako itokane na akili yako, nguvu zako na utimamu wa mwili uliojaaliwa na muumba. Usiweke matarajio yako Kwa watu. Success lies on your own shoulders. It's your burden dude! Pambana!!
Kuna mtu nilimsikia akiongea kauli fulani fupi ila inamaana sana kwa kizazi hiki.

Jitafakari ni kitu gani you are good at, then wekeza muda wako , akili yako, effort na elimu ya darasani kuliendea jambo hilo.
 
Thanks for your most exciting highlights...
But, the only issues is my lost time...
Hujapoteza chochote comrade,,,hao waliokutangulia kujenga, wewe ukijenga Sasa hivi, nyumba yako itakuwa mpya na ya kisasa zaidi. Kama hujaoa, ukuoa, utaoa mwanamke mwenye malengo na mtazamo unao utaka. Una nafasi ya kufanya kila kitu unachokitaka kama utasahau kujilaumu na kuwekeza maarifa ulio nayo kujipatia kipato.
 
Hujapoteza chochote comrade,,,hao waliokutangulia kujenga, wewe ukijenga Sasa hivi, nyumba yako itakuwa mpya na ya kisasa zaidi. Kama hujaoa, ukuoa, utaoa mwanamke mwenye malengo na mtazamo unao utaka. Una nafasi ya kufanya kila kitu unachokitaka kama utasahau kujilaumu na kuwekeza maarifa ulio nayo kujipatia kipato.
Asante sana, mkuu
 
Habari wanaJF....

Toka nko Primary school (PS), walimu wetu walipenda sana kutusihi kusoma kwa bidii ili tufanikiwe kimaisha. Toka mentality hiyo ya PS, niliwekeza mda wangu kwenye kusoma kwa bidii ili niyaishi maisha wanayosema walimu wetu.

Nmesoma shule kwa takilibani miaka 16 (toka Primary school mpaka nachukua degree yangu) kwa juhudi kubwa sana. Hatimae mambo yaligeuka toka pale nilipomaliza chuo na kurudi mitaani kufuata maisha yale walimu wetu walituambia, chakushangaza mambo yako tofauti kabsa.

Sasa na miaka 8 toka nmemaliza chuo, sjawahi kupata kazi ya maana. Tofauti na vibarua vidogo vidogo baada ya kumaliza chuo. Si kwamba skutafuta kazi, nmezunguka almost mikoa 8 Tanzania, nmefanya interviews za serikali zaidi ya 20, private sector zaidi ya 60. Nmerudi nyumban wale niliowaacha la 7 na F4, wana nyumba, biashara wengine magari.

Conclusion:
Tanzania [emoji1241] elimu haina maana.
Exactly bongo soma km una connection hivhiv ni ushenzi tu

Certificate inakutosha
 
Information technology unataka kuajiriwa?
Wakati form four Tu wanaingiza hela Kwa kufanya settings Tu za simu na Ku download watsap na nyimbo?


Wewe hujaamua Tu kujiajiri....usingekosa kazi kabisa...
Hata kufundisha computer huwezi??
 
Back
Top Bottom