Miaka 60 ya uhuru wa Tanzania: Ni uhuru bila mjeredi wa mkoloni lakini ni utumwa wa maisha katika ukombozi wa fikra

LODSI

New Member
Dec 7, 2021
4
3
Takribani miaka 60 tangu Tanganyika tupate uhuru wetu na ni takribani miaka 57 tangu Tanganyika iungane na Zanzibar tukawa TANZANIA ya leo, kwa miaka yote hiyo 60 kuna namna ambayo mtu mmoja mmoja, familia na serikali kwa ujumla ilitakiwa kichangua njia sahihi ya kuendesha maisha ya watu wake na sio kuchaguliwa na Mataifa yaliyoachilia ukoloni au yanayojiweza kiuchumi ( kuna pahali tunakwama )

1.UKOMBOZI WA ELIMU NDIO ULIKUA MFUMO PEKEE WA KUMWEKA MTANZANIA KUWA HURU NA NCHI YAKE PASIPO KUANGALIA MATAIFA MAKUBWA YATASEMA NINI KWENYE HAYA MAAMUZI KAMA NCHI
Namaanisha elimu ya Tanzania imejazwa kwenye makaratasi na nadharia zaidi kuliko hata vitendo na utekelezaji wenyewe pia mfumo wa elimu umesukwa kumpotezea mda mwanafunzi kiasi cha kutumia mpaka miaka 25-30 kuanza kujitegemea rasmi ( hii haiko sawa ). Mfumo hauko sawa kwa kuwa haumuandai mtu kuja kupambana na changamoto za kiulimwengu kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia bali una mwandaa mtu kupita kwenye njia zile zile ambazo kila msomi alipita hata yule wa miaka ya 90 au 2000 na ndio maana mifumo ya ajila imekua migumu kwa sababu msomi wa mwaka 2000 bado amekalia kiti chake na unamtengeneza msomi mwingine kwa mfumo ule ule wa kusubili aajiliwe hivyo lazima akae miaka mingi mpaka pale nafasi ya yule wa 2000 itakapo kwisha mda wake ndipo awekwe msomi wa 2020's ili hali Dunia inabadilika na inaenda kasi zaidi na hii ndio sababu ya sisi kuwa watu wa kuiga au kusubili mataifa yaliyo mbele yetu yatuamulia la kufanya.

RAI YANGU KWA SERIKALI NA WASHIKA DAU JUU YA SUALA LA ELIMU LINGEJARIBU YAFUATAYO

i. Suala la kwenda jkt liwe la lazima kwa wahitimu wa elimu ya kidato cha nne kwa maana jkt ndiko kunako mfunza mtu uzalendo na kujitegemea hivyo naiman mtu wa kidato cha 4 akili yake inakua haina mambo mengi sana hivyo akifundishwa kujitegemea vizuri itamjenga akirudi mtaani aweze kusimamia ndoto yake na aweze kuandaa mfumo wake wa ajila

ii. Elimu ya kidato cha sita ingeangaliwa kwa uzuri sana na si kila somo lingewekwa kule namaanisha yale masomo yanayotekelezeka kwa vitendo sana sana ikiwemo biolojia, kemia, fizikia na kilimo na ufugaji pamoja na biashara na kompyuta ambayo ajira zake ni uinjinia, udaktari, ufundi, ufamasia, kilimo, mambo ya habari na mawasiliano (IT) mengineyo yangewekwa katika mfumo wa diploma ambapo mwanafunzi baada ya kutoka kidato cha 4 akaenda jeshini akajifunza vizuri kujitegemea kabla akili haijakomaa atumia mda mwingi hata wa miaka 4 katika kubobea na kitu kimoja au viwili tu na mtu huyo tiketi ya kuingia chuo kikuu ni mpaka afanye tafiti au uvumbuzi wa jambo kwenye tasnia aliyobobea

iii. Serikali ingeona wajibu wa kusapoti vipaji kwani vipaji ni ajira kwa nafasi kubwa sana, tunao vijana wakiwa wadogo kabisa wanafanya mambo makubwa na ya kipekee kwa mfano vipaji vya mipira hao walitakiwa kupelekwa akademia ya mpira wa miguu huko atajifunza lugha, maadili, na anavozidi kukua anagusa shule na kipaji chake hakika timu ya taifa isingekua inafanya madudu kiasi hiki

> Vipaji kama uundaji wa vifaa mbali mbali na matumizi ya kompyuta wangelelewa kuviishi vipaji vyao leo tusingekua tunalipa pesa zetu kwa mainjinia kutoka nchi nyingne na tusingekua tunapata wakati mgumu katika kuandikiana mikataba katika ujenzi wa miradi mbali mbali kwa maana ni vipaji tulivyovilea na kuvigharamia wenyewe.

Pia watundu wa kompyuta wangewekewa mfumo mzuri wa kuendelezwa kuviishi vipaji vyao lakin serikali inawapotezea wanakua wanasoma kwa mlolongo mrefu wanakosa ajira wanaanza kuanya cyber penetration wanakamatwa kwa makosa ya cyber crime ndoto zao zinafia jela kumbe tungelea hizi talanta katika Dunia ya sayansi na teknolojia hawa ndio wangekua mwanga hasa kipindi hiki ambacho pesa ya kidigitali (cypto currency) na biashara za mtandaoni zimeshika kasi

iv. Masomo ya biashara yangewekewa ulazima na yangefundishwa kwa mapana zaidi kuanzia kidato cha 3 na 4 ili mtu anapokwenda diploma ya biashara awe hata na uwezo kuwa na blue print ya kampuni lake au aweze kuwazia njia moja au 2 zitakazomweka kwenye soko la kibiashara kwa utofauti ili hali amebobea kwenye hilo hivyo hata kukopa pesa kwa ajili kuendesha biashara lingekua jambo rahisi kuliko kumkopesha mtu mamilioni ya pesa ili apate degree isiyokua na ubobezi wala ajila na umri umekwenda sana

v. Pia jambo jingine ni kuwa vijana wasomi na pia wapambanaji wako na mawazo ya kimkakati ambayo yanaweza kuiweka Tanzania kwenye mstari wa mbele kiuchumi, kisayansi na teknolojia, kisiasa, kijamii na kitamaduni lakini hakuna mfumo mzuri au platform ambayo vijana wanaweza toa maoni yao kwa serikali nini kifanyike kutokomeza umasikini, nini kifanyike nchi iache kufurahia pesa za misaada ambazo zinazidi kugharimu maisha na rasilimali za watanzania, nini kifanyike ili mfumo wa elimu uwe rafiki na Dunia ya sasa na mambo mengi sana naimani serikali ingeamua kutumia wasomi na vijana hasa katika kuendesha mambo yake kuna mabadiliko ya haraka (rapid changes) yangeweza kuletwa kuliko kutegemea wanasiasa na watawala ambao umri umeenda katika utunzi wa sera na kupanga mikakati ya kimaendeleo kwa 100% ( yani Tanzania ya watu takribani 60 milioni inaongozwa na mawazo ya watu ambao hata 10 milioni hawafiki na waliobakia 50 milioni mfumo wa kutoa mawazo yao sio rafiki sana)

vi. Mwisho Serikali na washikadau wangekua na utaratibu mzuri wa kutoa mafunzo ya vitendo kwa ajili ya kumpa nafasi mtu aweze kujiajiri namaanisha kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia swala la pesa za kidigitali ilitakiwa liwe limefundishwa buree, swala la FOREX ilitakiwa liwe linefundishwa buree na mambo kadha wa kadha

KUNA MENGI YA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHANA NA SIO KILA WAZO LA MWANA JF AU MTANZANIA LINAWEZA KULETA SURUHISHO KATIKA TANZANIA ILIPOFIKIA KWA MAANA KUNA MENGINE TUMESHACHELEWA NA KUNA MENGINE TUPO NDANI YA MDA NA MENGINE YANAKUJA KWA HIYO NI SWALA LA KUONA TUPO TAYATI KWENDANA NA MABADILIKO AU TUACHE VIJANA WAYATAFUTE MABADILIKO KWA MBINDE KAMA ILIVYO SASA???

Kwa maana
●leo hii vijana wanaanza maisha ya kujitegemea na kujipambania wakifika chuo na wengine wakimaliza vyuo hatuoni hii ni hatari hasa kwa kizazi kinachokuja na inabidi kiongozwe na hawa vijana??
●Leo mtu wa chuo kikuu matumizi ya kompyuta hajui hata kuchapa barua kwa kutumia kompyuta na sababu anasema kwetu hatuna kompyuta nimekuja kuijulia chuo na wengine wanamaliza hawajui kwa kuwa waliwalipa pesa watu wa steshenari wawafanyie kazi za darasani
●Leo mwanachuo mwenye shahada yake hajui kufanya tafiti yoyote kwa kuwa amesoma mda wa miaka 3 kwa mawazo mawazo hana ubobezi hata wa alichosoma akimaliza anasubili ajila au aamua kutafuta tena mtaji kwa kutumia nguvu wakati hizo nguvu angetumia kwa miaka 25-30 aliyokaa shuleni hapo tunamzungumzia tajiri aliyejiwekeza sawa sawa.
 
Back
Top Bottom