Miaka 5 katika NDOA!

Naungana na wewe kuwatakia maisha mema ya ndoa mwenyezi mungu aendelee kuwalinda na kuwapa maisha marefu muendelee kuifurahia ndoa yenu

Nanyi akina baba msiwachokoze watoto wenu bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana. Efeso 6: 1 – 4..........................
 
Hongera sana mkuu. Hakika una sababu kumshukuru Mungu kwa neema zake kwenu. Mungu awabariki muweze kuadhimisha miaka 10, 25, 50, 75, nk ya ndoa yenu; mkizidi kumpenda na kumcha Bwana kwa kila kitu. Mubarikiwe sana. Amen!

Amen!

Asante!
 
Hongera sana.
Ndugu maskini jeuri kwa faida ya wana JF wote,
hebu tueleze changamoto moja kubwa ambayo hutoisahau uliyokutana nayo ndani ya miaka hiyo mitano ya ndoa yako.
 
mimi nina siku hamsini hivi kwenye ndoa......!

dah!

dah,timepishana siku kumi tu kaka!mi leo siku yangu ya sitini yaani miezi miwili 'taslimu'.eeh Mungu naomba unisaidie na mimi baada ya miaka hiyo mitano nikushukuru wewe na kuwajulisha wadau hawa wa JF tushukuru pamoja siku hiyo ikifika,aamen.hongera sana mkubwa MJ na Mungu akupe miaka mingi ya ndoa njema.
 
Hongera sana kwako pia kwa mama junior , mungu awaongezee miaka mingi ya upendo na baraka tele.
Mimi niko kwenye ndoa miaka nane sasa.
 
MJ,

Hongera sana kwa kufikisha miaka mitano ndani ya jela linaloitwa ndoa. Ni muda mrefu kwa kweli na si haba!

Binafsi na kupongeza wewe na shemeji kwani maneno uliyoyasema hapo juu yanatia moyo na yanaonesha kuwa kuna matumaini ya kusonga mbele. Kipindi mlichopita ni kigumu sana kwani ndio muda ambao watu bado wanachanga karata zao kabla ya kuukubali mchezo (ama wamepigwa bao au wamewini). Naona nyie mmewini na mtaendelea kuwini.

Mungu awabariki na kuwalinda, na awapatie uzao ulio mwema, musaidie katika kuijaza hii dunia! DC
 
Watoto wa baba paroko utawajua tu!! hahahahah.

Usiwacheke wenzio. Babu wa leo alikuwa kinda wa jana. Wape moyo tu na uwakaribishe kwenye club.
nawapa moyo tu,wasijione kwamba hawawezi:D

MJ,

Hongera sana kwa kufikisha miaka mitano ndani ya jela linaloitwa ndoa. Ni muda mrefu kwa kweli na si haba!

Binafsi na kupongeza wewe na shemeji kwani maneno uliyoyasema hapo juu yanatia moyo na yanaonesha kuwa kuna matumaini ya kusonga mbele. Kipindi mlichopita ni kigumu sana kwani ndio muda ambao watu bado wanachanga karata zao kabla ya kuukubali mchezo (ama wamepigwa bao au wamewini). Naona nyie mmewini na mtaendelea kuwini.

Mungu awabariki na kuwalinda, na awapatie uzao ulio mwema, musaidie katika kuijaza hii dunia! DC
ujumbe mzito huo
 
Hongera sana.
Ndugu maskini jeuri kwa faida ya wana JF wote,
hebu tueleze changamoto moja kubwa ambayo hutoisahau uliyokutana nayo ndani ya miaka hiyo mitano ya ndoa yako.

Nashukuru

Changamoto ya kwanza kabisa ilikuwa ni Dini zetu kuwa tofauti; Mimi Mkristo yeye alikuwa Muislam! baadhi ya ndugu pande zote hawakuridhika na hili ikiwa ni pamoja na Mama yangu mdogo aliyekuwa akininilea huko Dar! Mimi nilikuwa tayari kufunga ndoa kwa Mkuu wa wilaya. But She was bold ; kuna siku alikuja na kuniambia twende kanisani akabatizwe! Hatimaye ndoa yetu ilifungwa Kanisani pale Karikaoo Lutheran Church!

mnamo mwezi November 2005 tulibahatika kupata mtoto wa kiume; na mjuavyo shida ya wasaidizi hasa ukiwa na mtoto mdogo kwa jiji la Dar. Ilibidi nimshauri aache kazi (Stationery Office) ili amlee kijana wetu. Mwanzo ilikuwa ngumu lakini through trial and error yeye mwenyewe akaja kuungana nami kuwa ilikuwa ni vyema kwetu sote na kwa mwanetu! Thats why we have a healthy todler and quite energetic!

Mikakati yangu ya kiuchumi ilinisababishia kuhamishia shughuli zangu mikoani (nashughulika naIT hasa mambo ya networking) na kwa wakati mwingi mwenzangu amekuwa peke yake huko Dar; Mimi nachanja mbuga mikoani. Hapa palikuwa pazito wakati mwingine hata kiimani; kwni unaeza kupanga kurudi dar lakini kapita week 2 hujafanikiwa! na niliimiss sana familia lakini kwa upande mwingine tulikuwa tunapigana na dhana ya elimu bora kwa junior na biashara yake ya saloon zilizoko huko Dar. Limetuchukua muda na eseach ya kutosha mpaka sasa tumekubaliana yeye akaongeze ujuzi wa mambo ya decorations ili impe wigo mpana kwa hapa Dodoma na shule ya kijana tumepata pale Canon Andrea Mwaka; I'm told it among the best in Dodoma.

Kwenye mahusiano hapakosi wachafuaji; kuna brother wa rafikiye wa kike alikuwa anaitaka ngoma kabla lakini bahati mbaya mie nikalamba dume huyu jamaa amekuwa akitusumbua sana kwa msgs na simu hata namba zilipobadilishwa mpaka tukajua kuwa dada yake ndiye humpa namba zetu. Kiasi kwamba kuna wakati nikaaamua kufanya uchunguzi wa kina; Namshukuru mke wangu alinielewa na kunipa ushirikiano mpaka jamaa akapatika na kukemewa mbele ya nduguze. ila nasikitika nilitumia mbinu chafu kwa kweli cunajua tena ukihisi mali inataka kuyeyuka!:D

Na nasikitika kuwa kwa namna mmoja lilituanika kwa namna moja ila lilikuwa somo kubwa sana kwetu!

Namshukuru mke wangu for being supportive and understanding!
 
Hongera sana kwako pia kwa mama junior , mungu awaongezee miaka mingi ya upendo na baraka tele.
Mimi niko kwenye ndoa miaka nane sasa.

Hongera mkuu na Asante sana ubarikiwe; Hapo kwenye bold panahusika tunakuafuatieni kwa jirani kidogo!

Nadhani tunayohaki ya kumshukuru mungu kwani changamoto ktk maisha ya ndoa kwa sasa ni nyingi na complicated mno! hasa ukilinganisa na maisha ya Baba zetu!
 
Nawapenda pia (hasa ww)mkeo na mwanao juniour,duh but (tunanong'ona)hukuwahi kutoka nje?hongera sana na Mungu mwingi wa rehema na kusamehe akusamehe makosa yako yote uliotenda nje ya ndoa pia awazidishie miaka mingine 5550
 
Yaani wewe ni mchokozi siku zote. Kwa nini unaleta hizo hadithi wakati tunasherekea miaka 5? Kama ungemuuliza Xpin naamini angekupatia jibu zuri sana,

Mbona umeadimika hivyo?
 
Back
Top Bottom