Miaka 5 katika NDOA!

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
6,829
1,296
Wana JF!

Namshukuru Mungu kwa kutujaalia uzima na afya njema! Sifa na Utukufu ni vyake yeye!
Namshukuru Mungu kwa zawadi ya pekee mwanetu Junior hapo kwenye avatar! Mungu mlinde na umpe uhai hata naye aje asherehekee kama mimi leo!

Wapendwa wana JF napenda kuwashirikisha kuwa ifikapo tarehe 4 April 2010 mimi na shemeji/wifi yenu tutatimiza miaka 5 ya kuishi kama Mke na mume!

Miaka 5 sio mingi ni kweli lakini pia ni mingi katika maisha ya ndoa; Wangapi hawajafika? na siwafichi it was not a smooth ride always! Ila kwa msaada wa Mungu tumepita katika milima na mabonde na leo hii kwa ushujaa tunafurahi kuwa tulivuka na tutavuka yajayo mbele yetu kwa msaada wake yeye atutiaye nguvu! Jina la Bwana Yesu libarikiwe!

Naomba nichukue nafasi hii pia kuwaombeni kila mtu kwa imani yake; Jamani tuziombee ndoa zetu na tuwaombee wanandoa wote; NDOA ndio msingi wa Familia zetu; kuanguka kwake ni anguko la Familia na mmomonyoko wa society yetu! Familia imara zitaleta Watanzania imara wa baadaye na wenye uwezo wa kuijenga nchi yao!

Kwa nini ninaituma leo hii; Nitakuwa mapumziko kuanzia kesho kwangu mimi hii ni Double celebration ; Pasaka na Miaka 5 ya ndoa!

Nawapenda nyote

Mungu awabariki!
 
Umesahau kitu kimoja: kuelekeza lokesheni ya nyumbani kwako ili tuweze ku'navigate huko na kuleta mazawadi!
 
haaa kuna kipande hapo kimenigusa, ubarikiwe sana na nakutakia kila la kheri, kuna kipande kimenikumbusha mbali sana.
 
Umesahau kitu kimoja: kuelekeza lokesheni ya nyumbani kwako ili tuweze ku'navigate huko na kuleta mazawadi!

Wazo la kutaka kunipa zawadi tu kwangu ni zawadi tosha; Nitasherehekea mjini Dodoma na amabko familia yangu itakuwako kwa sasa! Kutokana na mimi kuhamishia mihangaiko yangu kanda ya kati.

Asante mkuu
 
Hongera sana kaka.

Mungu akupe nguvu zaidi na ndoa yenu idumu.Miaka 5 si mchezo,hapo mimi nilikua namaliza form six.

You have my prayers bro,mtuombee na sisi pia tupate wachumba wazuri

Mbarikiwe sana ndugu

haaa kuna kipande hapo kimenigusa, ubarikiwe sana na nakutakia kila la kheri, kuna kipande kimenikumbusha mbali sana.

Kiseme kipande kipi kwa faida ya wana JF wote; thts why I shared with you!
Amina Sista; Amina ubarikiwe nawe pia!

Asante!
 
Hongera sana kaka.

Mungu akupe nguvu zaidi na ndoa yenu idumu.Miaka 5 si mchezo,hapo mimi nilikua namaliza form six.

You have my prayers bro,mtuombee na sisi pia tupate wachumba wazuri

Mbarikiwe sana ndugu

Asante Brother!

Ni kwa Neema yake Mungu!

Tutawaombea ni mpango tuliojiwekea katika kuadhimisha tukio hilo!
 
mimi nina siku hamsini hivi kwenye ndoa......!

dah!

Usijali wako ambao wanatarajia; ww hata ukinyakuliwa leo obituary itasomeka "Ameacha mke!":D

Hawatasoma kuwa ulikaa 50 dayz!

Stop worrying you in already Hommie!
 
Usijali wako ambao wanatarajia; ww hata ukinyakuliwa leo obituary itasomeka "Ameacha mke!":D

Hawatasoma kuwa ulika 50 dayz!

Stop worrying you in already Hommie!
fact!
mtu kama georgie-porgie akifa leo watasema MAREHEMU ALIKUWA TOWASHI:D:D:D
 
fact!
mtu kama georgie-porgie akifa leo watasema MAREHEMU ALIKUWA TOWASHI:D:D:D

Hommie usinialike kwenye ugomvi na Georgie Porgie! Ngumi niliacha kupigana tangu primary na siku hizi mahanjumati ya shemejio yamefanikiwa kunifanya niwe mchache wa mbio ndefu!:D:D
 
Hommie usinialike kwenye ugomvi na Georgie Porgie! Ngumi niliacha kupigana tangu primary na siku hizi mahanjumati ya shemejio yamefanikiwa kunifanya niwe mchache wa mbio ndefu!:D:D
mtu kama fidel akidondoka leo watasema MAREHEMU ALIKUWA MSEJA:D:D
 
Hongera sana mkuu. Hakika una sababu kumshukuru Mungu kwa neema zake kwenu. Mungu awabariki muweze kuadhimisha miaka 10, 25, 50, 75, nk ya ndoa yenu; mkizidi kumpenda na kumcha Bwana kwa kila kitu. Mubarikiwe sana. Amen!
 
Back
Top Bottom