Miaka 35 huna familia, gari, nyumba wala mashamba... Unategemea miujiza gani kutoka Mbinguni?

ila kuwa na 35, kutomilki nyumba, viwanja, mashamba, gari au kuoa, Mimi naona sio tatizo, ila tatizo ni kuishi bila dira, kukaa bila kazi endelevu katika maisha yako ya mbeleni, yenye uwezo wa kukufanya millionaire after 5 Or 10 years to come!
Mleta mada ni muajiriwa anategemea mshahara. Hawezi kuwa milionea. Labda awe salarionea.
 
The World is not fair at all.

Kijana una miaka 35 lakini bado unakaa kwa wazazi au shemeji yako na huna nyumba, gari, familia , mashamba wala kamradi kokote… unategemea nini ?

Na kutoboa siku hizi si kama zamani ndugu zangu, ni lazima tujipinde sana. Tusilale kabisa, tupambane hadi kufa.

Usikate tamaa… anza sasa.
Na usipopambana ukaogopa.kufa unaweza kuwa umelala kwa shemeji ukang'atwa na mbu ukapata malaria ukafa
 
Mkuu ni kweli miaka 35+ inatakiwa mtu awe na vitu hivyo lakini kila mtu anamuda wake wa kufanikiwa huwezi mpangia Mungu awahishe baraka juu yako never.... Utakuta jamaa wa kitaa 38 hana hata kazi kutana nae 43 ananyumba ya mil 100 huko pia maisha ni bahati unaweza ukajituma sama mwisho ukajikuta mraji unachoma pesa yako yote
Kwa Africa nikawaida Sana,humu humu jamii forum wapo wengi sema tatizo kila mdau wahapa anajifanya mambo Safi!
 
Vijana wanabweteka sana, unakuta mtu huyo ana nguvu ya kufanya kazi yoyote ya kujiingizia kipato lakini yeye hajishughulishi kabweteka bweteee. Ili mradi anakula na kulala bure ,ye amesharidhika. Asee nikija kuwa na mtoto wa aina hii mi namfukuza akajitegemee mana ni mzigo tu

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Ukimzoezesha kazi tangu utotoni hatabweteka. Kila mtoto anahitaji uelekeo wa mzazi na kusaidiwa kukua kimwili, kiakili na kiroho.
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Ukimzoezesha kazi tangu utotoni hatabweteka. Kila mtoto anahitaji uelekeo wa mzazi na kusaidiwa kukua kimwili, kial
Hatuzungumzii kusaidia kazi za nyumbani,tunazungumzia umri mkubwa wa mtoto huku bado akiwa anategemea wazazi kiuchumi. Yani anakua hana direction kuhusu life lake yeye kama yeye bila utegemezi wa wazazi
 
Hapo mungu hali chumvi sjaelewa "tehehe
Pia mi nadhani kunaweza kuwa na mgawanyo maridhawa zaidi wa mali, kusiwepo asiye nacho kabisa, wazungumzia gari na nyumba, kuna watu hawajui jioni hii anakula wapi
Israel, Libya nk watu wanapewa kiinua mgongo cha kujikimu, pia kuna utaratibu wa nyumba za bei nafuu
Serikali, viongozi, siasa na Sera zinazopenda watu wao, na kuthamini utu wao. Lakini mweusi ye adhalilika kila mahali duniani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom