Rorscharch
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,431
- 3,071
Miaka 18, umemaliza kidato cha sita. Umebeba ndoto zako zote mgongoni kama mzigo mwepesi, macho yako yanang’aa kwa matumaini. Unajiambia, “Nikimaliza chuo nitayabadilisha maisha ya familia yangu.” Miaka 22, degree mkononi, lakini huna pa kwenda.
Dunia haijakukaribisha kama ulivyotarajia. Umebahatika kupata internship—huna mkataba, hulindwi na sheria, hulipwi vizuri. Laki mbili kwa mwezi, elfu sita kwa siku. Na bado unapaswa kula, kuvaa, kutuma pesa nyumbani, kutabasamu japo moyo umejaa huzuni.
Miaka miwili inapita kimya kimya. Unatumika, unajitoa, unajitahidi—kama kuna mtu anayeona. Lakini hakuna. Unapigwa chini bila huruma, nafasi yako inachukuliwa na kijana mwingine aliyejaa matumaini yale yale uliyokuwa nayo. Naye atatumiwa, atachoka, atatupwa. Mfumo unajirudia, kama mdundo wa nyimbo ya huzuni isiyo na mwisho.
Miaka 24, hujui tena unakoelekea. Kila siku ni kivuli cha ile nyingine. Hakuna kazi, hakuna kipato, hakuna matumaini. Na kama hiyo haitoshi—unaachwa na uliyempenda. Si kwamba hukumpenda vya kutosha, bali huna uwezo wa kumnunulia hata chakula cha mchana. Anaenda kwa mtu mwenye umri wa baba yako—aliye na pesa, gari, na uwezo. Unabaki na machungu. Mapenzi yanageuka kuwa kiwewe cha nafsi. Unaanza kuumia ndani kwa ndani. Kila picha ya harusi, kila post ya "baecation", kila story ya mafanikio Instagram inakukata moyo kama kisu. Unaanza kuamini hujatosha. Unaanza kujichukia.
Miaka 27. Sura yako imechoka. Macho yako hayang’ari tena. Unatembea kama kivuli cha mtu uliyokuwa. Hakuna shughuli. Hakuna ndoto. Hakuna hamasa. Njaa imekuwa rafiki. Hali yoyote inakufaa, bora tu ije. Unakubali kazi ya mshahara wa laki tatu—unaishi chumba cha laki moja, kilichojaa joto na mbu. Unakula chakula cha bei rahisi, unaandamana na marafiki wa hovyo, unafanya mazungumzo yasiyo na tija. Huna tena misimamo. Huna tena hofu. Maadamu siku inaisha, basi inatosha.
Na sasa, pombe ni faraja yako. Bangi ni kimbilio. Sigara ni rafiki. Udaku ni starehe. Dopamine ya bei rahisi imekuwa chakula cha akili yako. Unawaangalia waliopiga hatua kama maadui. Unawachukia, si kwa sababu wamekosea—bali kwa sababu wewe umeachwa nyuma. Unagonga miaka 30, huna ndoa, huna mtoto, huna hata mtu wa kuzungumza naye kwa kweli. Upo tu—mtu mzima aliyejaa utupu ndani ya nafsi yake.
Lakini yote haya hayakuanza jana. Yalianza miaka 22, pale ulipomaliza chuo na maisha yalikunyamazisha bila huruma. Ndoto zako zilianza kufa polepole, bila hata kelele.
USHAURI WA MWISHO KWA KIJANA WA MIAKA 20
Kijana, tafadhali usidanganyike. Usitamani maisha ya watu wa Instagram, usitamani mishahara ya laki nne yenye maumivu ya rohoni. Wengi wao ni waathirika wa mfumo. Wanavaa tai lakini ndani wamevunjika. Wanacheka ofisini lakini wanalia chooni. Wanapokea mishahara isiyotosha kulipa hata matumaini yao. Wanaishi maisha ya kujificha—hawana furaha, hawana upendo, hawana amani.
Kama una miaka 20, jifunze. Tafuta ujuzi. Kuwa bora kwenye jambo moja. Jenga mitandao ya watu wema. Linda heshima yako. Usiongozwe na njaa. Jenga msingi wa maisha imara. Tenga akili yako na kelele za mitandao. Siyo kila anayepiga picha nzuri ana maisha mazuri. Wengine wanapiga picha ili kusahau huzuni zao.
Na juu ya yote—chunga akili yako. Ipe nguvu, ilinde, ifunze. Kwa sababu, ikiwa itavunjika, hakuna mtu atakayekutengeneza.
–Makala hii ni kilio cha wengi waliovaa tabasamu la bandia. Kwa kijana wa Kitanzania. Kwa kijana wa Kiafrika. Kwa yule ambaye hajawahi kusikilizwa.