Miaka 30 Bila Ramani: Hujafa, Lakini Umechoka

Miaka 30 Bila Ramani: Hujafa, Lakini Umechoka

G
Maisha hayana formula mkuu, mim wakat najitafuta huko mererani kwa marehemu Erasto kuna watu walikuwa wanamiliki mabilioni, ila sasa hawana kitu na kuna watu wazima kwenye 50s ndio wamejipata saivi. Umri ni namba tu unaeza fanikiwa ukiwa mdogo, kijana, mtu mzima au hata uzeeni. Chamsingi nikuendelea kupambana.
N.B JAY Z AMEPATA MTOTO WA KWANZA AKIWA NA 40 same to J Lo na Mariah Carey.

Fact
 
Yeah, maisha yana mengi sana.. unaweza kuwa kwenye "right track" ila ukakosea kidogo mambo yakaharibika.

Many are struggling to be honest, na hasa wazazi waliosomesha wakiwa na hope kwa ajili ya watoto wao. Leo hii graduate anahaha kila kona kutafuta shughuli ya kufanya, mzazi alitumia rasilimali zote kupeleka mtoto shule, hana kilichobaki tena.

Kuna namna tunatakiwa kuwaza, kadri tunavyowapeleka shule, tuwaze namna watakavyoishi baada ya hivyo vyuo, ni kama shule haina tija kabisa kwa sasa.
 
Kabisa tuandae mazingira baada ya watoto kugraduate.
 
Miaka 18, umemaliza kidato cha sita. Umebeba ndoto zako zote mgongoni kama mzigo mwepesi, macho yako yanang’aa kwa matumaini. Unajiambia, “Nikimaliza chuo nitayabadilisha maisha ya familia yangu.” Miaka 22, degree mkononi, lakini huna pa kwenda.

Dunia haijakukaribisha kama ulivyotarajia. Umebahatika kupata internship—huna mkataba, hulindwi na sheria, hulipwi vizuri. Laki mbili kwa mwezi, elfu sita kwa siku. Na bado unapaswa kula, kuvaa, kutuma pesa nyumbani, kutabasamu japo moyo umejaa huzuni.

Miaka miwili inapita kimya kimya. Unatumika, unajitoa, unajitahidi—kama kuna mtu anayeona. Lakini hakuna. Unapigwa chini bila huruma, nafasi yako inachukuliwa na kijana mwingine aliyejaa matumaini yale yale uliyokuwa nayo. Naye atatumiwa, atachoka, atatupwa. Mfumo unajirudia, kama mdundo wa nyimbo ya huzuni isiyo na mwisho.

Miaka 24, hujui tena unakoelekea. Kila siku ni kivuli cha ile nyingine. Hakuna kazi, hakuna kipato, hakuna matumaini. Na kama hiyo haitoshi—unaachwa na uliyempenda. Si kwamba hukumpenda vya kutosha, bali huna uwezo wa kumnunulia hata chakula cha mchana. Anaenda kwa mtu mwenye umri wa baba yako—aliye na pesa, gari, na uwezo. Unabaki na machungu. Mapenzi yanageuka kuwa kiwewe cha nafsi. Unaanza kuumia ndani kwa ndani. Kila picha ya harusi, kila post ya "baecation", kila story ya mafanikio Instagram inakukata moyo kama kisu. Unaanza kuamini hujatosha. Unaanza kujichukia.

Miaka 27. Sura yako imechoka. Macho yako hayang’ari tena. Unatembea kama kivuli cha mtu uliyokuwa. Hakuna shughuli. Hakuna ndoto. Hakuna hamasa. Njaa imekuwa rafiki. Hali yoyote inakufaa, bora tu ije. Unakubali kazi ya mshahara wa laki tatu—unaishi chumba cha laki moja, kilichojaa joto na mbu. Unakula chakula cha bei rahisi, unaandamana na marafiki wa hovyo, unafanya mazungumzo yasiyo na tija. Huna tena misimamo. Huna tena hofu. Maadamu siku inaisha, basi inatosha.

Na sasa, pombe ni faraja yako. Bangi ni kimbilio. Sigara ni rafiki. Udaku ni starehe. Dopamine ya bei rahisi imekuwa chakula cha akili yako. Unawaangalia waliopiga hatua kama maadui. Unawachukia, si kwa sababu wamekosea—bali kwa sababu wewe umeachwa nyuma. Unagonga miaka 30, huna ndoa, huna mtoto, huna hata mtu wa kuzungumza naye kwa kweli. Upo tu—mtu mzima aliyejaa utupu ndani ya nafsi yake.

Lakini yote haya hayakuanza jana. Yalianza miaka 22, pale ulipomaliza chuo na maisha yalikunyamazisha bila huruma. Ndoto zako zilianza kufa polepole, bila hata kelele.

USHAURI WA MWISHO KWA KIJANA WA MIAKA 20

Kijana, tafadhali usidanganyike. Usitamani maisha ya watu wa Instagram, usitamani mishahara ya laki nne yenye maumivu ya rohoni. Wengi wao ni waathirika wa mfumo. Wanavaa tai lakini ndani wamevunjika. Wanacheka ofisini lakini wanalia chooni. Wanapokea mishahara isiyotosha kulipa hata matumaini yao. Wanaishi maisha ya kujificha—hawana furaha, hawana upendo, hawana amani.

Kama una miaka 20, jifunze. Tafuta ujuzi. Kuwa bora kwenye jambo moja. Jenga mitandao ya watu wema. Linda heshima yako. Usiongozwe na njaa. Jenga msingi wa maisha imara. Tenga akili yako na kelele za mitandao. Siyo kila anayepiga picha nzuri ana maisha mazuri. Wengine wanapiga picha ili kusahau huzuni zao.

Na juu ya yote—chunga akili yako. Ipe nguvu, ilinde, ifunze. Kwa sababu, ikiwa itavunjika, hakuna mtu atakayekutengeneza.

–Makala hii ni kilio cha wengi waliovaa tabasamu la bandia. Kwa kijana wa Kitanzania. Kwa kijana wa Kiafrika. Kwa yule ambaye hajawahi kusikilizwa.
This is bullshit thread

Age is just a number.

Kuna nini umeambiwa ukifika umri Fulani you need to have it .?

Mnawapa vijana pressure kwa upumbavu Kama huu
 
Yeah, maisha yana mengi sana.. unaweza kuwa kwenye "right track" ila ukakosea kidogo mambo yakaharibika.

Many are struggling to be honest, na hasa wazazi waliosomesha wakiwa na hope kwa ajili ya watoto wao. Leo hii graduate anahaha kila kona kutafuta shughuli ya kufanya, mzazi alitumia rasilimali zote kupeleka mtoto shule, hana kilichobaki tena.

Kuna namna tunatakiwa kuwaza, kadri tunavyowapeleka shule, tuwaze namna watakavyoishi baada ya hivyo vyuo, ni kama shule haina tija kabisa kwa sasa.
Umeandik pumba
 
This is bullshit thread

Age is just a number.

Kuna nini umeambiwa ukifika umri Fulani you need to have it .?

Mnawapa vijana pressure kwa upumbavu Kama huu
Mtumishi Mungu niguse .

Aging is not just a number. It is real.
Pia mtoa mada hajabagua mtu kwa kusema kuwa ndani ya Miaka hii usipokuwa hivi au hivi bas haujafanikiwa. (Najua ndio ulichowaza na kikakupelekea kuandika).

Yeye ametoa mtazamo wake na akasema nini kijana wa 20's afanye na kabla hajatika 30's.

Maana age kweli ina matter.
Una 40's yrs,
Huna familia, huna mtoto, huna kazi wala biashara.

Ww unaona ni sawa? Ila ukiwa na 20's na huna vyote hivyo watu wanasema unajitafuta.

This proved age is Real.
 
This is bullshit thread

Age is just a number.

Kuna nini umeambiwa ukifika umri Fulani you need to have it .?

Mnawapa vijana pressure kwa upumbavu Kama huu
Ndugu yangu, mwili wako ukianza kukongoroka (mgongo kuuma, knee caps kusuguana unavyochuchumaa etc) haujali kama hujajenga, haujari huna akiba kwenye akaunti
30 - 40s kwa asilima kubwa ni last chance kwa wengi
 
Maisha magumu kila sehemu, ila ni kupambana sana mpaka kieleweke.

Watoto wana hangaika kwa sababu hawana wazazi wa kuwashika mkono.
Kama mzazi katengeneza njia nzuri kwa wanae (sio kusoma tu)
Bali hata pindi mtoto anapokwama lazima mzee asimame nae kwa hali na mali
Huu utaratibu waswahili wengi hawana

Inabidi mjifunze haya kwani kesho mtakuwa na watoto pia au nyie muwaze kesho mkizeeka mtafanya nini

Mtu anakuambia maisha hayana formula, sawa kwa hiyo unakaa miaka 5 au zaidi huna muelekeo huku ukisema ipo siku

Wanangu wakiwa wadogo tayari nimewaandalia maisha pa kuanzia pindi wakikua
Tangu wanazaliwa nimewawekea senti kidogo kila mwezi na hii imewasaidia sana kupambana na maisha

Na bado wakihitaji sasa nawapa na sitegemei chochote kutoka kwao zaidi ya upendo
Lazima kujiandaa na kuwaandalia watoto ila sio kulazimisha usemi wa "Maisha hayana formula
 
Kwa hili Ww ni mfano wa Baba Bora.
Na mfano wa Wanaume wanaohitajika kwenye jamii.

Ilikuwepo hii toka zaman, baba zetu na babu zetu waliwatunza sana watoto hasa wa kiume.
Kuwapa mashamba, na asset nyingne.
Ila hapa katkat, kuna wababa wamesoma wakaelimika, na wao wakasomesha pia .

Ila sasa Kuwarithisha watoto hawana huo mpango,
Wanasema nimekusomesha.(ndio urithi wako🙃🙃🙃)

Elimu hii kuna namna inaweza isimtoe/kumtoa huyo msomi (hata kama ana akili au hana )

Plan A iwepo,
Plan B na C iwepo,
 
Age is just a number you can beat the odds at any time you don't need to count ur age .

Hata Kama Una miaka 30 unaweza kwenda chuo ukapata degree

Hata Kama Una miaka 40 unaweza kuoa ukapata Mtoto.

Don't pressurized the youths .

Kwakuwa tomorrow is Riddle
Hii ni kweli mm naitafuta 40 stil jobless but naamini any day nitatoboa .Mr never give up
 
Hii ni kweli mm naitafuta 40 stil jobless but naamini any day nitatoboa .Mr never give up
Age is Real bro.

Na pia kabla hujanijibu, hebu tulia na soma tena mtoa mada ametoa hoja gani.

Ndio utagundua pia na kuelewa age ina maana sana kama kuna mambo fulan hayajaenda sawa.

Na ndio maana Kijana wa 20's hawez kudefense namna mwenye 40's atakavyodefense hii hoja...

AGE is REAL deal

Pengne (sijui) in your 20's na ushaur kama huu wa Rorscharch ungeuona na kuufuata mambo yangekuwa mengine (sina uhakika pia).
 
Back
Top Bottom