Miaka 21 baada ya kifo cha Baba wa Taifa, mgombea yupi anabeba maono ya Mwl. Nyerere?

Team JPM

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,074
1,608
Leo ni takribani miaka 21 tangia kifo cha muasisi wa Taifa letu, Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Tangia kifo cha Baba wa Taifa mnamo Oktoba 14, 1999, Swali kubwa kwa watanzania lilikuwa ni 'Nani atabeba maono ya Baba wa Taifa katika kuiendeleza Tanzania?.'

Huu ni mwaka wa uchaguzi na watanzania tunapenda kumpata kiongozi mbeba maono ya mwl. Nyerere ambaye ni mzalendo, mchapa kazi, mpinga rushwa kwa vitendo, asiyefungamana na mabeberu, mwenye kuzilinda rasilimali za nchi kama madini, wanyama pori, misitu, ardhi, bahari na nyinginezo.

Watanzania tunapenda kumpata kiongozi mbeba maono ya Mwl. Nyerere katika kufufua viwanda ili kuongeza ajira, pato LA Taifa kitokana ns uzalishaji na fedha za kigeni kutokana na mauzo ya nidhaa zetu nje ya nchi.

Watanzania tunapenda kumpata kiongozi mbeba maono ya Mwl. Nyerere katika kufufua na kuyaendeleza mashirika ya umma ili kuboresha huduma kwa wananchi, Uhuru na usalama wa nchi kupitia huduma za usafiri wa Anga, reli, barabara na majini kutokana na tija ya mashirika ya usafirishaji kama ATCL, TAZARA, TRC, NASACO na kuboresha huduma za mawasiliano kupitia TTCL, TCRA na POSTA.

Watanzania wanapenda kumpata kiongozi mbeba maono ya Mwl. Nyerere katika kutetea Uhuru na hadhi ya Tanzania kama Taifa Huru, lenye kujipangia na kujiamlia mambo yake yenyewe bila kushurutishwa na mataifa mengine.

Watanzania wanapenda kumpata kiongozi mbeba maono ya jukumuyerere kwa kuhimiza watanzania kuchapa kazi, kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo wao wenyewe na Taifa kwa ujumla.

Watanzania wanapenda kumpata kiongozi mbeba maono ya Mwl. Nyerere kwa ushupavu na ujasiri wa kuliongoza Taifa na kulivisha katika majanga ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Watanzania wanapenda kumpata kiongozi mbeba maono ya Mwl. Nyerere kwa kuzibaini hila na hujuma za mabeberu na kukabiliana nazo kwa weledi.

Watanzania wanapenda kumpata kiongozi mbeba maono ya Mwl. Nyerere kwa kusimamia makusanyo ya kodi ili kugharamia miradi mikubwa ya kimkakati kwa maendeleo ya Taifa.

Watanzania wanapenda kumpata kiongozi mbeba maono ya Mwl. Nyerere kwa kulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kulinda umoja wa Kitaifa na kuifanya Tanzania Taifa Imara, lenye Umoja na Mshikamano.

Kumbukizi ya miaka 21 tangia kifo cha Baba wa Taifa letu tuitumie kama Fursa ya Kuwatathmini wagombea wote katika nafasi ya URAIS ili TUMCHAGUE KIONGOZI MBEBA MAONO YA MWL. NYERERE KATIKA UCHAGUZI MKUU 2020.
 
Unajua kwanini Mwalimu aliamua Kung'atuka wakati nchi ikiwa hoi?

Naona umekuja na porojo za Magufuli hapa.
 
Back
Top Bottom