Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums...

Nianze kwa kumshukuru sn Nyani Ngabu kwa thread hii ya pekee iliyotuibua wengi toka kwenye machimbo.

Kwa mimi binafsi kazi zangu za sasa hazinipi nafasi ya kutosha kuingia huku mtandaoni.

Lakini pia niushukuru uongozi mzima wa JF kwa kazi kubwa ya kutuunganisha wadau mbalimbali kwa kipindi cha miaka 10 sasa.

Nilijiunga JF 2009. Hakika kipindi hicho JF ilikuwa bado ina nguvu ya juu sn, na ilikuwa na watu makini sn kwenye siasa na MMU.
Sitarudia kuwataja waliokwishatajwa, lakini nawa'salute sn wote, maana mmeweka alama za kudumu 'Landmarks' katika nyaja ya mijadala ya mitandao. Lkn ni lazima nimtaje mtu maarufu sn ambaye hajatajwa hapa, ambaye amewasaidia watu wengi sn kwenye nyanja muhimu ya afya, akijulikana kama MziziMkavu, Salamu sana ndugu.

Mimi binafsi nina mchango wa kutosha ktka hii miaka 10. Enzi hizo ilikuwa ngumu sn kwa members wa JF kuonana kwa kuhofia usalama wao.

Lkn taratibu mimi ni mmoja wa watu walioanza kuhudhuria kwenye social gatherings kama misiba na kuugua kwa members hasa pande za huku Arusha.
Nakumbuka mwaka 2011 nilimtembelea member mkongwe kabisa aliyekuwa mgonjwa anaitwa Lunyungu, akashangaa sn.

Taratibu baadaye ikaonekana kuwa members wanaweza kuonana na kujadili mambo ya msingi, tofauti na kujificha nyuma ya screen.

Mwaka 2010 nilifiwa na Baba mzazi huko Dar, nilishangaa kuona kundi kubwa la wanaJF, wakanifariji sana na kuniwezesha, chini ya Bwana Teamo, wakati huo akijiita Geoff Asprin, bht na wengineo wengi.

Sisi wa huku kanda ya Kaskazini tukaanzisha kambi iliyoitwa ArushaWing, ikapata nguvu sn kiasi cha kuitikisa Dar, na kuwa mfano na Icon ya JF nzima kwa mshikamano

Nakumbuka tulifanya safari za kutembelea vivutio vya nchi yetu kama Tarangire, Ngoro2 Duluti Amboni Tanga, etc.
Safari ya Tarangire ilivutia hisia kali kiasi cha kuwafanya wanaJf toka Dar kumiminika Arusha jioni hiyo kuungana na sisi kwa blast la hatari na tukakesha.

Kilele kilifikiwa pale Mkuu Maxence Melo alipoungana na hao members wa Dar na kuwasili Arusha na kutangaza kuwa wazo la kuanzisha JF lilikuwa conceived huku Arusha, yeye akiwa katika hali ya mzozo na dola akiwakimbia Polisi na kuishi maisha ya kujifichaficha.
Siku hiyo tulifahamiana, tulikula na kunywa, tukacheza muziki sana na mengine mengi ambayo siwezi kuyasema.

Baadaye watu wa MMU Dar nao wakajikongoja na kuanza kuonana phyisically kwa organization za akina Babu Asprin na wengineo. Wakaanza kufanya safari za outing kwa kuogopana sana, na baadaye walikuja kuorganize tukio lililoitwa White Party.

Kwa ufupi ni kwamba tulisaidia sn kubadili mitazamo ya members, na kuwezesha urafiki wa mitandaoni kubadilika kuwa wa wazi, na mengi mengineyo.

Ukiacha mijadala ya siasa, JF imekuwa ni site ya msaada sn na imebadili maisha ya wengi.

Kuna marafiki zetu wengi walipata biashara, kazi, mbinu za ujasiriamali, ujuzi, wengine wamepona magonjwa kupitia JF Doctor, na zaidi sn kuna wadau wengi niwajuao ambao hatimaye walioana na tumecheza sana harusi zao na hadi leo wana watoto na maisha yanaendelea.

ArushaWing ya wakati huo tulipata wageni wengi sana toka nchi nzima. Ilikuwa kila mdau wa Jf akipata Fursa kuja Arusha basi anapata mapokezi ya daraja la kwanza toka kwa members!
Hapa nawakumbuka watu maarufu sn kama DARKCITY Mwita Maranya, @Woman of Substance TIMING na watu kibao.

Tuliripoti sn matukio ya siasa za Arusha kwa kupangana ili kupata coverage nzuri. Ilikuwa mmoja anakuwa internet cafe, mwingine eneo la tukio, na wengine wanarusha kwa simu kila bit ya matukio. Hapo ndio utajua kazi ya Saharavoice na Crashwise.

Mwisho kabisa nakumbuka JF Dar ilipata kuanzisha kitu kama Saccos, wadau wakawa wanakutana , wakafungua Bank account, sijajua ile kitu inaendeleaje ndani ya hii miaka 10, au kama ilitumbuliwa sina ufahamu. Naomba ajuaye atujuze.

Jf imetupanua ufahamu sn na hizi taarifa za juzi kwamba wanalazimishwa kutaja wanaogenerate habari ni mbinu chafu za wachache kuitoa makali. Kwa taaluma zetu na michango ya hali na mali tupigane kuhakikisha frontliners wanashinda na haki inaibuka Bingwa.

Mungu awabariki sn.
PakaJimmy.
Hatimae Uzi umekutoa mafichoni teh

Salute kwako bro,nakumbuka wewe ndio ulikua mtu wa1 kunikaribisha Arusha wing pale narock pub mwezi huo nilipokua na siku chache tu tangu nijiunge JF,hiyo siku sitaisahau kwenye historia hii maana nilikua nakimuhe muhe hatari cha kuwaona lol...

Mengi tumeshare na tutaendlea kushare kwa kadri tutakavyojaliwa
 
Jf nilijiunga 2013 na nilivutika zaidi na jukwaa la siasa....

Nakumbuka kipindi hicho jukwaa hili halikua jepesi jepesi kama sasa,watu walikua wanamwaga nondo mpaka unafurahi mwenyewe. Ilikua kabla hujaachia post yako yabidi ujiridhishe kwanza,ukikaa vibaya unapewa za uso ha haa....

Jukwaa la2 kunivutia ni MMU na chit chat... Nilivutika sana na kina @Preta,@Hearven on Earth na lara 1.

Nimeelimika kupitia JF,imeniongezea wigo wa marafiki ambao wengine muda si mrefu tunakwenda kufanya kitu cha kupiga hatua na imekua sehemu ya maisha yangu sasa.

Ninaombi kwa uongozi wa JF ikiwezekana trh husika kama bado haijapita tufanye kitu cha kutukutanisha. Miaka10 si haba jamani, haikua kazi rahisi.
Sorry, hapo kwenye Bold; Baby na wewe umechumbiwa humu? Ujue nilikuaga siamini kama online charting inaweza kuleta mahusiano ya kudumu? Hongera sana kama itakua kweli.
 
Ha haa asante....

Ingawa nilimaanisha kitu kingine
Huwezi kua open on the issue sijui kwasababu gani? Look, wazazi wetu walikutana wengine kwenye kwaya makanisani, wengine kwenye ngoma za asili na wengine shule au makazini, kama kungekuwepo na mitandao ya namna hi may be some of them nao wangekuta through this media as well, huna sababu ya kuona aibu. Muhimu ni kuishi pamoja kwa AMANI na sio meeting place ilikua wapi!
 
Jf napenda sana ....wakati naanza nilikuwa nikiperuzi kama mgeni tu sikuwa na Id......nilipenda sana jukwaa LA MMU.....lakini kwa sasa navutiwa zaidi na Jukwaa LA siasa.
 
Kuhusu JokaKuu umenigusa kidogo. Huyu ndugu yangu anakumbu kumbu za muda mrefu na ni mwepesi sana wa kuunganisha kumbu kumbu hizo na wakati uliopo, ni kati ya wakubwa tunaowatumaini sana katika ujenzi wa kutumia vichwa na ulezi wa kizazi hiki kilichosahau debate
...Ni kweli.

...Nguruvi3, nikushukuru nawe, kwa mada zako zilizojaa tathimini muhimu za mambo mbalimbali yanayojiri nchini. Pamoja na kwamba nyingine huwa siwezi changia -kwa kuwa ni za kundi maalum- lakini huzisoma na kutafakari.

...Namkosa Mchambuzi ambaye siku hizi ameadimika na zile mada zake, zenye kuhitaji tafakari kabla ya kuchangia au kujibiwa.
 
Back
Top Bottom