Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa JamiiForums...


Ahlan wa sahlan!
 
Nilikuwepo miaka hiyo hila kwa kuwa ujuzi wa komputer kuwa ndogo nilipoteza id yangu ya awali kila nikjaribu recovery ilikataa nikakaa miaka kibao baadaye nikaibuka upya. asanteni wachangiaji le Mutuz big show, na yule mbeba box wa UK aliyehama CHDEMA (LUKOS)walikuwa ni vinara wa mtandao
 
Mkuu Nyani Ngabu umenikumbusha mbali sana enzi za darhotwire, enzi za jambo forums na hata ze utamu!!

Kusema kweli inabidi tuwapongeze sana akina Maxence na Mike kwa jinsi ambavyo walijitoa kuhakikisha JF inakuwepo. Nadhani kuna wakati walitumia raslimali zao kuhakikisha JF inakuwepo na walipoona mambo yanakuwa magumu walikuja kwetu wanachama na tukajitoa kusaidia kwa tulichokuwa nacho.

Tangia wakati huo JF imekuwa kwelikweli japo kukuwa kwake nako kumekuwa na changamoto zake. Makala motomoto zimepungua kidogo, zile ban hazionekani siku hizi post zenye ukakasi nazo zimezidi! Lakini kwa ujumla wake JF bado ndio mtandao bora wa habari hapa TZ.

Kuna wenzetu siku hizi hawaonekani sana humu akina Mwita Maranya sijui wapo wapi!!

Nadhani ni vyema uongozi wa JF ukaandaa maadhimisho rasmi ya kutimiza miaka 10.
 
Hadi wewe umefufuka, hongera Nyani Ngabu, this turned out to be my favourite thread 2016
 
Hapana nitake radhi siwezi kuwa na akili kama za Malaria Sugu unapigwa ban JF unakwenda kushitaki kwenye gazeti la Mwanahalisi.
Mkuu upo? Hii habari ya malaria sugu kupigwa ban na kukimbilia kwenye magazeti nimeiandika kwenye thread moja nakuja huku naikuta nawe umeiandika!!
 
Mkuu upo? Hii habari ya malaria sugu kupigwa ban na kukimbilia kwenye magazeti nimeiandika kwenye thread moja nakuja huku naikuta nawe umeiandika!!
Ahahahah mkuu Kimbunga fikra zetu zipo sawa, juzi nilikusoma kwenye uzi wa Msafiri Mwita kaimu balozi wa UK mtoto wa Mzee Mwita meneja wa zamani Mwatex nilicheka sana.
 
Sura mkuu hata mimi niliambiwa da same ting ma men..... Siasa kajadilie Jamboforums ila mada zilikuwa chache sikuelewa aliyekuwa anazianzisha nilijaribu one day kujibu hoja nikaambiwa nijiregister kwanza nikawa na mashaka maana nishazea kuchange nick kila siku DHW na Marafiki Chat nakaipotezea kwa muda like wiki mbili nikakuta mada zile zile nikashangazwa why na mada yenyewe ilimhusu Mkapa... nikajiunga ili niponde nikapost hadi leo sikumbuki id yangu... wala pass but kama ingekuwepo am sure ningejaribu na ningekumbuka kwenye trying maana manick huwa yanakuja tu nikishika pc.... but Jambo chat ilikuwa poa sana baada na machungu ya Mwingereza Snickly wa chatzone... Sijapata ona mzungu mkuda kama Yule.... ever and ever ndie aliiua chatzone kudadeki... akamrisisha Mufti... mara anaweka limit mwisho watu 24 mara no flood blah blah kibao
 

Kuna watu hapo wamepotea kabisa!
 
leo ni miaka 10 naamini safari inaendelea siku itakua miaka 100 ya uhai wa jf licha ya misukosuko mingi hususani baada ya uchaguzi mkuu,jf kushambuliwa nilikosa amani sana,mwenye link aweke hapa nijikumbushe tafadhari
 
Nianze kwa kumshukuru sn Nyani Ngabu kwa thread hii ya pekee iliyotuibua wengi toka kwenye machimbo.

Kwa mimi binafsi kazi zangu za sasa hazinipi nafasi ya kutosha kuingia huku mtandaoni.

Lakini pia niushukuru uongozi mzima wa JF kwa kazi kubwa ya kutuunganisha wadau mbalimbali kwa kipindi cha miaka 10 sasa.

Nilijiunga JF 2009. Hakika kipindi hicho JF ilikuwa bado ina nguvu ya juu sn, na ilikuwa na watu makini sn kwenye siasa na MMU.
Sitarudia kuwataja waliokwishatajwa, lakini nawa'salute sn wote, maana mmeweka alama za kudumu 'Landmarks' katika nyaja ya mijadala ya mitandao. Lkn ni lazima nimtaje mtu maarufu sn ambaye hajatajwa hapa, ambaye amewasaidia watu wengi sn kwenye nyanja muhimu ya afya, akijulikana kama MziziMkavu, Salamu sana ndugu.

Mimi binafsi nina mchango wa kutosha ktka hii miaka 10. Enzi hizo ilikuwa ngumu sn kwa members wa JF kuonana kwa kuhofia usalama wao.

Lkn taratibu mimi ni mmoja wa watu walioanza kuhudhuria kwenye social gatherings kama misiba na kuugua kwa members hasa pande za huku Arusha.
Nakumbuka mwaka 2011 nilimtembelea member mkongwe kabisa aliyekuwa mgonjwa anaitwa Lunyungu, akashangaa sn.

Taratibu baadaye ikaonekana kuwa members wanaweza kuonana na kujadili mambo ya msingi, tofauti na kujificha nyuma ya screen.

Mwaka 2010 nilifiwa na Baba mzazi huko Dar, nilishangaa kuona kundi kubwa la wanaJF, wakanifariji sana na kuniwezesha, chini ya Bwana Teamo, wakati huo akijiita Geoff Asprin, bht na wengineo wengi.

Sisi wa huku kanda ya Kaskazini tukaanzisha kambi iliyoitwa ArushaWing, ikapata nguvu sn kiasi cha kuitikisa Dar, na kuwa mfano na Icon ya JF nzima kwa mshikamano

Nakumbuka tulifanya safari za kutembelea vivutio vya nchi yetu kama Tarangire, Ngoro2 Duluti Amboni Tanga, etc.
Safari ya Tarangire ilivutia hisia kali kiasi cha kuwafanya wanaJf toka Dar kumiminika Arusha jioni hiyo kuungana na sisi kwa blast la hatari na tukakesha.

Kilele kilifikiwa pale Mkuu Maxence Melo alipoungana na hao members wa Dar na kuwasili Arusha na kutangaza kuwa wazo la kuanzisha JF lilikuwa conceived huku Arusha, yeye akiwa katika hali ya mzozo na dola akiwakimbia Polisi na kuishi maisha ya kujifichaficha.
Siku hiyo tulifahamiana, tulikula na kunywa, tukacheza muziki sana na mengine mengi ambayo siwezi kuyasema.

Baadaye watu wa MMU Dar nao wakajikongoja na kuanza kuonana phyisically kwa organization za akina Babu Asprin na wengineo. Wakaanza kufanya safari za outing kwa kuogopana sana, na baadaye walikuja kuorganize tukio lililoitwa White Party.

Kwa ufupi ni kwamba tulisaidia sn kubadili mitazamo ya members, na kuwezesha urafiki wa mitandaoni kubadilika kuwa wa wazi, na mengi mengineyo.

Ukiacha mijadala ya siasa, JF imekuwa ni site ya msaada sn na imebadili maisha ya wengi.

Kuna marafiki zetu wengi walipata biashara, kazi, mbinu za ujasiriamali, ujuzi, wengine wamepona magonjwa kupitia JF Doctor, na zaidi sn kuna wadau wengi niwajuao ambao hatimaye walioana na tumecheza sana harusi zao na hadi leo wana watoto na maisha yanaendelea.

ArushaWing ya wakati huo tulipata wageni wengi sana toka nchi nzima. Ilikuwa kila mdau wa Jf akipata Fursa kuja Arusha basi anapata mapokezi ya daraja la kwanza toka kwa members!
Hapa nawakumbuka watu maarufu sn kama DARKCITY Mwita Maranya, @Woman of Substance TIMING na watu kibao.

Tuliripoti sn matukio ya siasa za Arusha kwa kupangana ili kupata coverage nzuri. Ilikuwa mmoja anakuwa internet cafe, mwingine eneo la tukio, na wengine wanarusha kwa simu kila bit ya matukio. Hapo ndio utajua kazi ya Saharavoice na Crashwise.

Mwisho kabisa nakumbuka JF Dar ilipata kuanzisha kitu kama Saccos, wadau wakawa wanakutana , wakafungua Bank account, sijajua ile kitu inaendeleaje ndani ya hii miaka 10, au kama ilitumbuliwa sina ufahamu. Naomba ajuaye atujuze.

Jf imetupanua ufahamu sn na hizi taarifa za juzi kwamba wanalazimishwa kutaja wanaogenerate habari ni mbinu chafu za wachache kuitoa makali. Kwa taaluma zetu na michango ya hali na mali tupigane kuhakikisha frontliners wanashinda na haki inaibuka Bingwa.

Mungu awabariki sn.
PakaJimmy.
 
Asante sana mkuu Nyani Ngabu kwa kutupa historia fupi ya jf. Binafsi ningependa kuipongeza timu nzima ya uongozi wa jf kwa juhudi zao za dhati kuhakikisha wanyonge kupata pa kusemea. Pamoja na yote nasikitika sana kuona jf inahujumiwa na watu wenye mabavu (mamlaka?) waliodhamiria kuipoteza ktk uso wa Tanzania.

Kama sheria zingelikua hazijawekwa kwa ajiri ya kubana tabaka tawaliwa, basi kesi iliyoko mahakamani kwa sasa ingekua nyepesi ila tatizo kwa sasa sheria nyingi zimekua zikianzishwa kukandamiza tabaka tawaliwa na ikiwezekana kulinyamazisha kabisa.

Tumwombe Mungu atujalie afya njema wananchi wote wakiwemo watoto wetu, ndugu zetu, kaka zetu hata shemeji zetu bila kuwasahau mapolisi ambao wanalipwa kwa kodi zetu ila wanatuona malofa (mnisamehe).

Naomba kuwasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…