You Got It.... Apige QT apate cheti cha sekondari kwa jina lake...... aende amahakamani aape kuwa jina lake alotumia chuoni lifute na litambuke jina lake halisi na ikiwezekana afanye taratibu na vyeti vyake vibadilishwe baada ya kiapo(cjui kama inawezekana hapa)...v ikifanikiwa akamshukuru yule dada alomfanizia na maisha yasonge.... ajifunze kutokana na makosa..!!! wazo tu..Aende mahakamani akale kiapo abadilishe jina liw jina la kwenye cheti.
Ushauri wa hapa utapeleka kuleeee . . . Au itakuwaje?
Aende mahakamani akale kiapo abadilishe jina liw jina la kwenye cheti.
Nakushauri usifakamie Vyeti, tafuta elimu.. Hicho Kiswakinge ulivyokiandika unaonekana muhuni .. Eleweka Na lugha unayotumia sio unachanganyachangaya wewe umekuwa Waziri mkulu.. Pinda!
mimi nimecopy tu na kupaste kaka
sio mimi smile
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 25,
nilimaliza form four miaka kadhaa iliyopita kwa bahati mbaya sikuweza kufaulu kuendelea na kidato cha 5,
nilipata division four ya mwisho
i have to admit uwezo wangu ulikuwa mdogo darasani,
nikakaa one year home bila issue yoyote
baadaye kaka yangu ambaye alikuwa chuo mwaka wa 2 akaniambia amenitafutia cheti cha mtu niingie chuo,
kweli akanitafutia nafasi CBE nikaanza kusoma certificate ya accounts kwa kutumia cheti cha huyo dada ambaye nilikuwa simjui later nilikuja kufahamu kumbe alikuwa girlfriend wake,
basi nikamaliza certificate, nikasoma diploma, mpaka advance diploma,
wakati niko Advance diploma mwaka wa mwisho kakangu akaoa
lakini hakumuoa yule girlfriend wake nayemjua mimi na ambaye natumia cheti chake
akamuoa dada mwingine tofauti,
kwakweli mpaka leo sijui kwanini hakumuoa yule dada na siwezi kumuuliza,
basi yule dada alikasirika sana na akaninyang'anya cheti chake
yeye wakati huo alikuwa mwaka wa mwisho Institute of Accountancy Arusha,
kwakweli nilichanganyikiwa ila sikujua kama impact yake itakuja kuwa kubwa hivi
, nilipomaliza chuo nikapata kazi shirika moja Arusha
sasa hapo ndo mchezo ulipobadilika after 6 months wakaniambia nipeleke original certificates zangu,
Duuh nilidata nikampigia kaka simu akaniambia omba likizo njoo Dar tudiscuss nikarudi tukahauriana nikaamua niache kazi maana ntapeleka vyeti gani wakati cheti cha form four sina.
nikakaa home kama one year my cousin sister akanifanyia mpango nikapata cheti cha kuchonga mtaani akanitafutia kazi Bank moja hapa Dar,
nikaanza kufanya kazi sijafikisha hata mwaka last month nikaitwa HR naambiwa nisubmit my original certificates, nikasema ni nini tena hiki, basi nikapeleka kile cheti cha kuchonga na vile vingine original vya chuo but natumia jina la yule dada, after a week nikasimamishwa kazi ili kupisha investigation nikaambiwa nimeforge vyeti na mimi sio mwenye hvyo vyeti,
as am speaking to you am just home sijui la kufanya, naona kama kakangu ameniponza ningejua ningerisit by then imagine vyeti vyangu vyote vya chuo vina jina la huyo dada,
naomba mnielewe wakati huo nilikuwa mdogo sikujua impact ya kutumia cheti cha mtu but i think my brother did so msinihukumu kwa hilo, nimepoteza 6yrs kusoma with all my effrots amd energy na nilijitahidi sana nikapata lower second na sikuwahi kusupp,
i have i feeling huyu dada ananifatilia kila napoenda na kuniharibia,
hivi naanzia wapi jamani, nirudi tena kurisit form four, naona siwezi that means another 7 yrs za kurudi shule by then ntakuwa na 32yrs ntazeekea shule jamani,
yani sijui hata la kufanya nawaza mpaka nafika mwisho, naishia kulia sipati hata usingizi.
ndugu zangu wananishauri nirudi shule nianze moja but nahisi siwezi kusoma tena, naombeni mnishauri labda naweza pata options hapa ambazo hazitahitaji kutumia muda mwingi
Its me a frustrated lady
sometimes tatizo lipo kwenye system yetu.. kama mtu anauwezo wa kufanya kazi vizuri kabisa stil unafatilia vyeti vya kazi gani.!? matokeo yake ndo kupata mafisadi yaliyosoma..
bak to the topic, hamna kurudi nyuma talk na huyo mdada mmalizane vizuri ka ye ndo huwa anakualibia if not huwe unawapoza mabosi wako ata kwa ten percent ya salary, hope hawatakua wanoko tena.!!
Nenda kwa huyo dada, mwumbe msamaha,mwambie wewe huna kosa kama ni kosa la kakayako akuonee huruma japo kakako hakumwonea huruma.