Jamani hivi nyie wenzangu vipi katika hili, maana mie muda unavyozidi kwenda mbele naona naboreka si kawaida na huduma za ATMs za kibongo hata sijui iweje wajirekebishe yaani ama so so bored 100% na kuzidi!!!! Yaani imeshanikuta mara nyingi sana mi-ATM haifanyi kazi tena wakati mwingine ni ya aina tofauti inagoma kutoa pesa kwa wakati huo huo! yaani leo nimeboreka sana Ubungo oilcom nimeenda ATM za umoja-zote mbili hola, nikahamia NMB nayo hola, bahati mbaya nikawa sinayo ya Baclays (ambapo ningetumia VISA) ambayo kwakweli naweza kuwapongeza sana kwakuwa sijawahi kupata nayo shida hata siku moja! ila haya ma-ATM mengine yananiuzi sana sina jinsi kwasababu ni kwasababu maalum ndo maana naendelea kuwa nayo, siku moja tena nipo msasani li-atm la umoja likagoma, nikaenda manyanya hola, nikaenda mwananyamala nalo pia, wakati huo nina shida balaa tena kipindi hicho ndo mipromo kibao ya umoja, kweli inauzi! tena huwa najitahidi sana kupiga simu call centres zao na kuwaambia why this why this ila hayajirekebishi..!!! Yaani mi-ATM ya kibongo mnaboa sina tu jinsi...