Waziri Ummy: Nimeona Clip ya Mtumishi wa Afya Hospitali ya Kivule akiosha vifaa na kuanika juani. Tunalifanyia kazi!

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya Kijamii ikiwemo JamiiForums, ikimuonesha Mtumishi wa Afya katika Hospitali ya Kivule Mkoani Dar akisafisha na kuanika juani vifaa ya Afya. Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametolea maelezo suala hilo.

Waziri amesema :

Nimeona clip inayohusu Mtumishi wa Afya akichambua, kusafisha na kuanika vifaa vya Hospitali katika Hospitali ya Kivule Mkoani Dar es Salaam.

Kitendo hiki ni kinyume na taratibu na miongozo ya Kanuni za Udhibiti wa Maambukizi (Infection Prevention and Control). Tayari Viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam wanalifanyia kazi suala hili na watatoa Taarifa Rasmi.

Ninamshukuru mwananchi alierekodi na kuisambaza clip hii. Nitoe wito kwa wananchi kutoacha kuibua mambo kama haya yanayotokea katika vituo vyetu vya kutoa huduma za Afya vya umma na binafsi ili kuongeza uwajibikaji katika Utoaji wa Huduma za Afya nchini kwa kuwa Afya zetu ni wajibu wetu.

Aidha, nitoe rai kwa wataalamu wa afya kuzingatia mafunzo na miiko ya kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. Wizara ya Afya kwa kushirikiana na OR Tamisemi tutaendelea kuchukua hatua ili kuimarisha ubora wa huduma #MtuNiAfya @wizara_afyatz


Screenshot 2023-07-08 124841.png


Pia, soma
 
Waziri acha kauli za ovyo....kabla ya kuhukumu fuatilia ndio utoe kauli.....Tukiibua changamoto zote zinazotokea vitu vyote vya afya nchi utatatua? Maana vituo vingi hali ni mbaya na havina vifaa..Hata huyo mtumishi sidhani kama kafanya kwa makusudi means nyenzo hana...bora hata huyo anavianika at least...wengine wanafanya bora liende hakuna cha kuanika...
 
Waziri acha kauli za ovyo....kabla ya kuhukumu fuatilia ndio utoe kauli.....Tukiibua changamoto zote zinazotokea vitu vyote vya afya nchi utatatua? Maana vituo vingi hali ni mbaya na havina vifaa..Hata huyo mtumishi sidhani kama kafanya kwa makusudi means nyenzo hana...bora hata huyo anavianika at least...wengine wanafanya bora liende hakuna cha kuanika...
Kuna mada humu kuwa tucheke sana,na tule raha sana ILA siku ikifika ukaugua na kulazwa kwenye hizi nyumba zilizopewa majina ya hospital, ndio utakumbuka kuwa wewe ni nothing, royal families check up UK,India au Mill park, kuna mmoja wapo alienda USA kupasuliwa tezi dume!minor operation hata hapa lingusenguse unaweza fanyiwa
 
Back
Top Bottom