Mkurugenzi amvua madaraka Mganga Mfawidhi hospitali ya Kivule

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,026
1,621
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Jomari Satura, amemvua madaraka Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Kivule kwa kushindwa kusimamia majukumu yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Julai 8, 2023 na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano, Tabu Shaibu, hatua hiyo imefikiwa baada ya kushindwa kuhakikisha utoaji wa huduma za afya katika kituo hicho unazingatia ubora, miongozo, taratibu na sheria za afya.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba Satura ameelekeza muuguzi kiongozi wa wodi ya wazazi kuondolewa kwenye nafasi yake na kupangiwa majukumu mengine.

Hatua hizo zinakuja baada ya kusambaa kwa video iliyomuonyesha mtumishi wa hospitali hiyo akisafisha na kuanika juani vifaatiba nje ya jengo la hospitali, kitendo ambacho hakikubaliki kwa kuwa ni kinyume na taratibu na miongozo ya afya.

Kwa niaba ya uongozi wa jiji, Satura ameomba radhi kwa mamlaka na umma wote wa Watanzania kwa kitendo hicho kilicholeta usumbufu na taharuki.

Satura amemuagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kuhakikisha anasimamia kwa karibu utoaji wa huduma bora katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali na binafsi.

“Ofisi ya Mkurugenzi inakemea vikali vitendo kama hivi na itahakikisha havijirudi tena na kuwataka watumishi wote wa sekta ya afya na sekta nyingine kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kwa kuzingatia miongozo na taratibu zote,” ameeleza Tabu kupitia taarifa hiyo.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma:

mbona wanaotuibia hela zetu kweny kutupiga picha za uongo kwenye MAEGESHO tunalalamika na hamchukui hatua! je mkurugenzi nawewe MPIGAJI?
mtu upo tabata unaandikiwa upo posta mpya hata haujaenda hata huko mjini!! tukilazmisha muweke kaeatasi mnagoma! na msg haziji kwenye simu zetu! je Mkurugenzi ni mwizi?
 
Nimeiona video, vifaa vilikuwa stoo, so alivichambua vilivyokuwa vinafaa kutumika kisha kuviosha... So havina infections, pili vp angeosha vikakakauka kisha akaenda kuvichemsha? Au akafuata ile IPC protocol kabla ya kuchemsha?
 
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Jomari Satura, amemvua madaraka Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Kivule kwa kushindwa kusimamia majukumu yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Julai 8, 2023 na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano, Tabu Shaibu, hatua hiyo imefikiwa baada ya kushindwa kuhakikisha utoaji wa huduma za afya katika kituo hicho unazingatia ubora, miongozo, taratibu na sheria za afya.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba Satura ameelekeza muuguzi kiongozi wa wodi ya wazazi kuondolewa kwenye nafasi yake na kupangiwa majukumu mengine.

Hatua hizo zinakuja baada ya kusambaa kwa video iliyomuonyesha mtumishi wa hospitali hiyo akisafisha na kuanika juani vifaatiba nje ya jengo la hospitali, kitendo ambacho hakikubaliki kwa kuwa ni kinyume na taratibu na miongozo ya afya.

Kwa niaba ya uongozi wa jiji, Satura ameomba radhi kwa mamlaka na umma wote wa Watanzania kwa kitendo hicho kilicholeta usumbufu na taharuki.

Satura amemuagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kuhakikisha anasimamia kwa karibu utoaji wa huduma bora katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali na binafsi.

“Ofisi ya Mkurugenzi inakemea vikali vitendo kama hivi na itahakikisha havijirudi tena na kuwataka watumishi wote wa sekta ya afya na sekta nyingine kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kwa kuzingatia miongozo na taratibu zote,” ameeleza Tabu kupitia taarifa hiyo.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma:

Kwa nini wamewajibishwa ilhali mkurugenzi alitoa taarifa kwa umma akidai kinachoonekana sio kinachofikiriwa, kwamba vifaa vile vilitolewa stoo?!!
Mkurugenzi naye atolewe!!
 
Hii kitu nlisema juzi. WATakuja kufkuza fkuza watu tu af hakuna la maana instead ya kujua how to solve the problem
 
muuguzi-pic.jpg

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Jomari Satura, amemvua madaraka Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Kivule, jijini Dar es Salaam kwa kushindwa kusimamia majukumu yake.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kipande cha video kumuonesha mtumishi wa hospitali hiyo, Deborah Chacha akisafisha vifaa vya kuhudumia wagonjwa vya hospitali hiyo na kuvianika juani.

Hatua hiyo, iliibua sintofahamu huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji hilo, Jomari Satura ametoa taarifa akisema vifaa hivyo vilivyoonekana kupitia video hiyo havikuwa vimetumiwa na wagonjwa na kwamba tukio lililoonekana ni jukumu la kawaida la uchambuzi na usafi wa kawaida wa vifaa hivyo kutoka stoo ya kuhifadhia vifaa.

Hata hivyo, kupitia mtandao wake wa Twitter, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu juzi aliandika,"nimeona clip inayohusu mtumishi wa afya akichambua, kusafisha na kuanika vifaa vya Hospitali katika Hospitali ya Kivule Dar es Salaam.

Kitendo hiki ni kinyume na taratibu na miongozo ya Kanuni za Udhibiti wa Maambukizi (Infection Prevention and Control). Tayari viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam wanalifanyia kazi suala hili na watatoa taarifa rasmi,” ameandika.

Wakati taarifa hiyo ya Mkurugenzi ikifafanua, baadaye ilitolewa taarifa nyingine na Msemaji wa jiji hilo, Tabu Shaibu ikieleza kuwa uamuzi wa kumvua umetokana na kushindwa kuhakikisha utoaji wa huduma za afya katika kituo hicho unazingatia ubora, miongozo, taratibu na sheria za afya.

Taarifa hiyo inaeleza Satura ameelekeza muuguzi kiongozi wa wodi ya wazazi kuondolewa kwenye nafasi yake na kupangiwa majukumu mengine.

Amesema kwa niaba ya uongozi wa jiji, Satura aliomba radhi kwa mamlaka na umma wote wa Watanzania kwa kitendo hicho kilicholeta usumbufu na taharuki.

“Ofisi ya Mkurugenzi inakemea vikali vitendo kama hivi na itahakikisha havijirudii tena na kuwataka watumishi wote wa sekta ya afya na sekta nyingine kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kwa kuzingatia miongozo na taratibu zote,” amesema Shaibu.

Waziri Ummy, katika andiko lake kuhusu video hiyo, alitoa rai kwa wataalamu wa afya kuzingatia mafunzo na miiko ya kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Amesema Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tamisemi zitaendelea kuchukua hatua ili kuimarisha ubora wa huduma za afya.

“Ninamshukuru mwananchi aliyerekodi na kuisambaza clip hii.

Nitoe wito kwa wananchi kutoacha kuibua mambo kama haya yanayotokea katika vituo vyetu vya kutoa huduma za Afya vya umma na binafsi, kuongeza uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya nchini kwa kuwa afya zetu ni wajibu wetu,” ameandika.

chanzo. Kuanika vifaa juani kwamponza Mganga Kivule

Back
Top Bottom