Mhitimu wa degree ya sheria auza mihogo baada ya kukosa ajira

mkuu,
wakati wewe ulikuwa unafanya hicho kibarua kama kazi ya kuzugia ukisikilizia michongo mengine uliyo itega(yawezekana tayari ulishaacha baada ya kuajiriliwa),wengine hufanya kama life time career with bigger dreams ahead.bila shaka huyu neema ni mmoja wapo.

watu kama hawa ndio mwisho wa siku huja kuwa kama akina KFC,Walt Disney, Bakheresa na wengineo.
Ni kweli wakati ule sikua na direction mkuu, hivyo sikukubali kukaa bure nyumbani bila kupata ela ikanibidi nifanye kazi hiyo, najua hata Neema anafanya hivyo wakati huu ambapo hajui hatma yake but akishapata mchongo nina hakika hiyo kazi ya mihogo ataacha.
Wahitimu wengine waige mfano wafanye chochote kujiingizia kipato ili mradi wasivunje sheria za nchi.
Mhitimu usikubali kula bure unalemaa akili fight tafuta ela kwa jasho lako uonje ladha ya kupanga bajeti na mipango thabiti.
 
Safi Sana .. Umetia nguvu Neema nisonge mbele. Wapo akina neema wengi.. Cha muhimu kuwa na vision kubwa
 
Neema mhitimu wa shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipomaliza Chuo hakufanikiwa kupata ajira lakini ameona asikae bure tu nyumbani ameamua kuwa mfano wa vijana wenye uthubutu kabisa kuwa tofauti! kwenye shughuli kubwa zenye mikusanyiko huwa anafanya biashara ya kuuza mihogo ya kukaanga pamoja na kachumbari nzuri yenye viungo inavutia sana na mihogo yake ni mitamu haswaaaaa sana!
Source: Clouds Media
NB: Tunakoelekea ni kugumu na vijana inabidi kukaza mkanda..

15492542_1280583835318365_8166818150006743384_n.jpg
15541117_1280583845318364_4704867959592455352_n.jpg
Dah,huyu mdada anafaa kuoa kweli,inaonekana sio mtu wa majivuno,ivi anapatikana maeneo gani huyu mdada niende kumuungisha,heshima yake sana mdada Neema
 
Kumbe kusoma sio muhimu ...mnataka kuliangamiza Taifa eti KFC au Bakharesa...hivi hao walisomea nini?Mary kusomea fani yake alafu hasiitumie kwenye jamii au hasituke kwenye hiyo fani sio jambo zuri.Mnatumia neno kujiajiri kama ascape goat
 
Huyu mdada muda sio mrefu sana atakuwa maarufu,ipo siku mkulu atampatia tenda ya kulisha ikulu mihogo,safi sana Neema
 
Naona kawaida mbona wapo wengi tu wanafanya mishemishe maisha yasonge mbele, huyo katangazwa ila ambao hawajatangazwa na hawahitaji kutangazwa ndo wengi zaidi.
Nakumbuka kabla ya kupata kitu cha kufanya baada ya kumaliza chuo kikuu (CoNAS-UDSM) nilikua msaidizi wa fundi ujenzi mitaa ya majohe na hakuna aliyekua anajua kama mimi graduate isipokua ndugu yangu ambaye alikua fundi, alinipa support sana kila akipata tenda ananipigia simu nadamka asubuhi na mapema.
Maisha ni safari ndefu sana jamani acheni tu

Wadogo zangu mlioko vyuoni, mnaosubiri ajira, mnaoteseka hamjui hatma yenu, fanyeni kazi maisha yaende mbele hata kama ni ujenzi fanyeni life ni tight sana msibweteke hata kidogo.
Wengine unaweza kua huna hata ndugu yako diwani wala mtu serikalini aisee ukilemaa utateseka sana tafuta ishu ya kufanya hata kuuza kuku wa kukaanga we fanya.
Ni kweli kabisa usemayo
 
Back
Top Bottom