YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,911
- 51,889
Anahitaji kupongezwa sana kwa kuona fursa na kuitumia.good girl bravoooo
Watanzania kelele kila siku.Chukulia bishara ya kuchoma chips kuku iko kila kona Tanzanaia ukiangalia unaweza sema huoni fursa.Lakini wenzetu wazungu mfano KFC wakagundua kuwa Tanzania kuna fursa kubwa ya kuuza biashara ya chips kuku sababu wanaofanya hiyo biashara haiko kwenye viwango vya kumvutia mtu wa kipato cha kati na cha juu kuzila.Wakaja na hoteli za chips kuku tu lakini za HIGH QUALITY kama wawekezaji na wanauza kama nini.Mtanzania waweza kuta anapiga yowe hamna fursa na utaletaje mwekezaji auze chips kuku? Huyo analipa kodi serikalini kubwa tu na anatoa ajira kibao na anaajiri hadi wasomi wa madgrii kibao wakati huyo mwingine kodi tu kupata ya halmashauri hadi ngumi zitembee amwagiwe chips ndipo alipe.
Huyu dada kaona fursa kaichukua chap chap hongera zake.