Mheshimiwa Zitto, vijana tunakupenda lakini mambo haya yanatutia wasi wasi juu yako

Status
Not open for further replies.
Bila shaka Zitto hawezi kusahaulika katika historia ya Mabadiliko ya kifikra katika Bunge. Zitto ndie mbuge wa kwanza alieweza kuhoji au kusema direct bungeni kwamba Waziri kasema uongo, yeye ndie alieondoa zana ya uoga bungeni, pia kwa kujiamini alisimamia hoja zake. Nakumbuka baada ya kufukuzwa bungeni, mimi nilitembea kwa miguu kupokea msafara wako kuelekea jangwani. Lakini mimi nina wasiwasi na wewe kama ifuatavyo.

Baada ya ule mkutano wa Jangwani, kwa muda mfupi Mheshimiwa Zitto alijiondoa katika harakati za kueneza chama. Chadema ilifanya mikutano mingi ya kueneza chama kwa slogan mbali mbali, ikiwemo Operation Sangara, M4C nk, katika harakati zote hizi Zitto Kabwe hakuonekana kabisa. Wakati Viongozi wa Chadema wakiangaika kueneza chama huku wakipigwa mabomu Arusha, Morogoro, Iringa nk, Mheshimiwa Zitto kastarehe tu. Mimi binafsi nilikuwepo katika matukio kadhaa ya kupigwa mabomu, hata pale Soweto Arusha nilikuwepo

Wengi tulijiuliza, kwanini Zitto kapotea ghafla?, je katika mafanikio ya Chadema ya sasa mpaka kuweza kusimamisha wagombea kwa mitaa na vijiji vingi na kufanikiwa kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, je Zitto umehangia nini? Unaweza ukasimama ukawaambia Watanzania kuwa katika uenezaji wa Chadema hadi vijijini umechangia ukilinganisha na cheo ulichokuwa umepewa ndani ya chama?

Mimi nasema hivi, vijana wengi tunakupenda lakini kwa dalili hizo nilizozielezea, ukitaka ondoka bwana, maisha yanaweza songa mbele bila wewe. Hata ukiwa na mwanamke mzuri wa sura na umbo, kama akiwa na tabia mbaya, kwa roho ngumu utamwambia kwakheri nakutakia maisha mema.

Chadema Blog: CHADEMA Kufanya mkutano mkubwa wa operation sangara leo ifakara

Baada ya zengwe walilowekewa na polisi pale morogoro,na kuwazuiwa kufanya mikutano ya hadhara, leo chadema watafanya mkutano wa kufa mtu hapa mjini ifakara. Kwa mujibu wa radio pambazuko na vipeperushi, operation sangara maalum ya kukipanga chama tayari kukabidhiwa dola inazinduliwa leo 8/8/2012. Viongozi wote wa kitaifa ,kamanda Freeman Mbowe, mpiganaji Dr Wilbrod Slaa,makamu mwenyekiti Said Afri,mbunge wa kigoma kaskazini Zitto kabwe, J.J Mnyika na mwanasheria Mabere Marando wote watakuwepo. Pia wabunge wote wa cdm watakuwepo. Mkutano utafanyika viwanja vya polisi maarufu kama kiungani. Mapokezi ni pale kibaoni saa 7:00 mchana, yakifatiwa na maandamano kuelekea viwanjani. Mkutano utaanza saa 8:30. ITV, STAR TV na Chanel ten watakuwepo. Ntakuwa up 2 date. Kwa sasa ni mzuka pikipiki zinapita mitaani zikipeperusha bendera za cdm.
 
kweli wewe punguani ulitaka aende akapigwe mabomu shika adabu yako bwana umpeleke mtu kwenye kifo? zzt utamkumbuka tu bado ulishaambiwa ukitaka kumpiga mbwa unampa jina baya mlisha mpa jina hilo tulieni basi mnyolewe ninyi vipi?

Sasa hapa mbona ww ndo waonekana punguani?
 
nkobe fuatilia historia tangu 2009 zitto alipotaka kugombea uongozi....walimtenga! hizo operation zote.....walimtenga! zitto kavumilia mengi sana

then mnatumia kutokuonekana huko kama fimbo!!

Nani waliomtenga? kwani kura zinapigwa na Mbowe?
 
nkobe fuatilia historia tangu 2009 zitto alipotaka kugombea uongozi....walimtenga! hizo operation zote.....walimtenga! zitto kavumilia mengi sana

then mnatumia kutokuonekana huko kama fimbo!!

hata jimboni kwake alitengwa...je unaweza kuwaambia wana JF jimboni Kwa zitto kuba madiwani wangapi Wa Chadema, wenyeviti Wa vijiji, vitongoji,mitaa wangapi...
je alitengwaje maana moja ya vitu alivyokuwa analalamikiwa Ni kutokufika ofisini yaani makao makuu ya chama...
 
Ndugu mimi huwa nasema sikizote hakuna kitu nisichokipenda kama unafiq,Zitto ni mtu wa Kigoma mwenzangu lakini tuseme ukweli havumiliki huyu dogo,tunamfahamu sana tangu anaingia kwenye siasa kwa sababu tulimpokea sisi.Alitengwa nanani kama sio yeye kujitenga?.Alianza matatizo muda mrefu sana huyu.Lakushangaza nipale eti anamlaumu Mh Mbowe eti anampiga vita'mbona alipomtoa Ujerumani kumleta kugombea ubunge huku akimfadhiri kuanzia hela yakula mpaka akampa bure gari yakufanyia kampeni Zitto hakumuona Mbowe mbaya?.Nayasema haya kwa sababu namfahamu Zitto na hayo ya Mbowe niliona au mumuulize Zitto ile gari aliyopewa bure na Mh Mbowe alimludishia?

Hata kama mbowe alimsaidia ndio anataka zitto amlambe miguu?
 
wenzake walipotoka bungeni km ishara ya kupinga matokeo ya uchaguz 2010 hakushiriki

harakati nyng za chama alizitosa na kusimama mwenyewe
 
hata jimboni kwake alitengwa...je unaweza kuwaambia wana JF jimboni Kwa zitto kuba madiwani wangapi Wa Chadema, wenyeviti Wa vijiji, vitongoji,mitaa wangapi...
je alitengwaje maana moja ya vitu alivyokuwa analalamikiwa Ni kutokufika ofisini yaani makao makuu ya chama...

Kigoma hawachagui chama wanachagua mtu, kama chadema waliweka wagombea matutusa unataka wananchi wawachague tu? kigoma sio viazi kama arusha wako radhi kuchagua JIWE mradi liko chadema.
 
nkobe fuatilia historia tangu 2009 zitto alipotaka kugombea uongozi....walimtenga! hizo operation zote.....walimtenga! zitto kavumilia mengi sana

then mnatumia kutokuonekana huko kama fimbo!!
Kuna wakati unafiki na mahaba yanatakiwa kuwekwa pembeni. Chadema wamechelewa mno kumtimua Zitto. Ni mtu wa ajabu sana huyu. Wenzake wanafanya kampeni za ubunge Arusha kumpigia kampeni Nasari, yeye anaenda Kigoma kutangaza eti atagombea urais. Huyu hakutaka maendeleo ya kisiasa ya Chadema. Alifanya hivyo ili kuondoa attention ya kampeni za kumwingiza ubunge Nasari. Kwanza timing mbovu, na vilevile katiba ilikuwa haimruhusu kwa umri wake kugombea urais. Alifanya makusudi ili Chadema ishindwe ubunge ARUMERU. Lakini hila za msaliti huyu hazikufaniikiwa na sasa Chadema inapepea serikali za mitaa n.k. bila Zitto. Huyu alikuwa ni kirusi kilichotakiwa kuondolewa mapema sana. Hafai kabisa na anachefua mno.
 
wenzake walipotoka bungeni km ishara ya kupinga matokeo ya uchaguz 2010 hakushiriki

harakati nyng za chama alizitosa na kusimama mwenyewe

Mdee mbona hakuwepo? Tatizo chadema kila atakachosema mfalme mbowe mnataka kiwe sheria hata kama ni upuuzi
 
Ukitaka uzi wako upate mvuto hapa jf mzungumzie zitto, lakini uzi kuhusu slaa ,mbowe,lema,tundu lisu hazipati wachangiaji kabisa kwa sababu wamepoteza mvuto, Zitto ndio mwanasiasa pekee wa upinzani anaependwa na watanzania

Chadema ni zaidi ya haka kakipandikizi kenu.Moto upo mwaka huu october.Na mafisadi yenu ya makengeza,mboga za m10,na ikulu iliyo chafu yote ile.
 
Kuna wakati unafiki na mahaba yanatakiwa kuwekwa pembeni. Chadema wamechelewa mno kumtimua Zitto. Ni mtu wa ajabu sana huyu. Wenzake wanafanya kampeni za ubunge Arusha kumpigia kampeni Nasari, yeye anaenda Kigoma kutangaza eti atagombea urais. Huyu hakutaka maendeleo ya kisiasa ya Chadema. Alifanya hivyo ili kuondoa attention ya kampeni za kumwingiza ubunge Nasari. Kwanza timing mbovu, na vilevile katiba ilikuwa haimruhusu kwa umri wake kugombea urais. Alifanya makusudi ili Chadema ishindwe ubunge ARUMERU. Lakini hila za msaliti huyu hazikufaniikiwa na sasa Chadema inapepea serikali za mitaa n.k. bila Zitto. Huyu alikuwa ni kirusi kilichotakiwa kuondolewa mapema sana. Hafai kabisa na anachefua mno.

Yaani mtu alikuwa kigoma ndio alete athari Arusha? kwa hiyo ulitaka kila kitu kisimame kisa nasari anagombea ubunge? hoja ya kipuuzi sana hiyo
 
hata kwenye hizi changuzi za serikali za mitaa sijaona mchango wa kiongozi wa juu wa chadema . zitto kachangia kiasi kwamba tumepata mitaa mingi. tena Kwa nchi nzima zitto kawa na mchango huo. mtakumbuka swala la escrow limetokea kipindi tunaelekea uchaguzi na hapo ndipo nguvu ya zitto kupitia kamati yake ilipoonekana. tulitembea mtaani Kwa hoja ya kutokuwapa kura wezi wa fedha za umma za escrow. tena zitto kasaidia sana kwani macho yote ya watanzania yalisubili report ya zitto

Ebu tuache akili za kuazima. Escrow ni hoja ya Kafulila wala siyo Zitto, Zitto ni mwanyekiti wa kamati ya PAC yenye wana CCM pia, alichokifanya yeye na kamati yake ni kwenda kuangalia ukweli ukioibuliwa na Kafulila. Kazi ya Zitto ilikuwa ni kuwasilisha tu, hata mtu yeyote angewasilisha pia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom