Ombi Maalum kwa Rais Magufuli: Mteue Zitto Kabwe kuwa Mbunge wa Bunge la JMT, ndiye mpinzani pekee mzalendo, Capable kuongoza PAC!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,964
2,000
Wanabodi

Anza na kumsikiliza

Kufuatia kilichotokea tokea leo Zanzibar kwa Maalim Seif kuapishwa kuwa Makamu wa Kwanza wa rais Zanzibar, nimefarijika sana, na kurudisha matumaini kuwa angalau Tanzania japo hatuna any serious and credible opposition, lakini angalau tunao responsible opposition ambao the most credible ni ACT Wazalendo, kwa sisi tunaomjua Maalim Seif, akisusa!, hakuna Mzanzibari yoyote angeweza kumweleza kitu, hivyo kitendo cha kumuona Maalim Seif amelainika!, hadi akukubali kurejea SUK, amini nakuambia, hiyo ni kazi ya the one and only Zitto!.

Nimemtaja Zitto, kwasababu mselewa jinsi Maalim Seif alivyo mtu wa misimamo, akisusa, amesusa!. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, alisusa jumla, hivyo hii change of mind this time, is contributed to none other than Zitto Zuberi Kabwe, na hii ndio faida kwa wanasiasa ma extremists kama Maalim Seif kujinga na vyama vya contemporary politics kama ACT Wazalendo as opposed to vyama extremist kama CUF-Maalim Seif ya enzi zile, iliyokuwa ngangari, ukiachana na hii CUF-Lipumba iliyopo sasa ambayo ni mlenda au uji kabisa!.

Hii ni kufuatia ACT Wazalendo ndicho chama pekee cha upinzani nchini Tanzania, chenye vision and a mission to accomplish ambacho ni capable kinachofanya responsible opposition kinachokwenda kuwa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, kufuatia Chama kikuu cha upinzani huku Bara, Chadema, kuonyesha dalili zote za immaturity hivyo is not a capable opposition ya kufanya responsible opposition bungeni. Kuhusu Chadema kutokuwa na uwezo, hili tumelizungumzia Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?. Lakini kwa upande wa ACT, tangu mwanzo kimejibainisha ni responsible party Kiukweli, Kama Sio Nguvu ya Soda, Then ACT ni Tishio. Hawa ni The Underdogs, Huwezi Kuwapuuza

Baada ya Maalim Seif kuapishwa na kuwa Makamu Zanzibar, chama cha ACT Wazalendo, ndicho chama kikuu cha upinzani Zanzibar, hivyo ili kukamilisha responsible opposition kwa pande zote za muungano, hili ni ombi maalum kwa Rais wa JMT, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, amteue Zitto Zuberi Kabwe, kuwa Mbunge wa Bunge la JMT, kupitia zile nafasi zake kumi za uteuzi wa wabunge wa kuteuliwa na rais, kwa sababu Zitto atamsaidia sana kwa kuifanya Tanzania kuwa na upinzani wa kweli, maana upinzani wa kweli ni upinzani wa kushindanisha hoja kwa hoja mbadala na unafanyikia Bungeni, na sio upinzani wa kupiga kelele mitaani, hivyo kitendo cha Chadema kupata wabunge 20, halafu chama kinawafuta uanachama ili wafutwe ubunge ni uthibitisho wa watu wasiojitambua, hivyo kwa vile Zitto anajitambua na anauwezo wa kujenga hoja zenye nguvu za hoja, badala ya hoja za nguvu, hivyo Zitto mmoja tuu, akiingia Bungeni, atalisaidia sana Bunge letu, kufuatia yeye, kupitia chama chake cha ACT Wazalendo, ndie mpinzani pekee mzalendo, wa kweli anayefanya responsible opposition, ambaye ni capable kuongoza kamati ya Bunge ya PAC.

Ingawa rais wa JMT hapangiwi na yeyote, kitu chochote cha kufanya, lakini anaweza kushauriwa na yeyote, jambo lolote lenye manufaa na maslahi kwa taifa letu katika mustakabali wa upinzani, ila rais anakuwa yuko huru kupokea ushauri, kuupuuza, na akiamua kuupokea, then yuko huru kuutekeleza, au kuupokea na kuupuuza, na hata akiutekeleza, uamuzi huo ataifikia yeye mwenyewe, sio kwa kushauriwa au kushinikizwa.

Japo haijaandikwa popote, na sio wengi wanajua, maadam nchi ya Tanzania ni nchi ya vyama vingi siasa, Mlezi Mkuu wa Upinzania, ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutumia vyombo vyake, na ndio maana vyama capable, vinalipwa ruzuku na fedha za kodi zetu, hivyo siku ile lile jarida la mabeberu la The Economist liliposema Rais Magufuli amedhamiria kufuta upinzani Tanzania ufikapo mwaka 2020, mimi nilikanusha nikasema jarida ni waongo na wanasema uongo. The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja
Sasa kunapotokea uongo kama huo kusemwa, halafu ukaja kutokea kweli kwa Watanzania kuwakataa wapinzani, hivyo wakakichagua CCM pekee, hawa mabeberu wataendelea kutupigia kelele. Japo hawatutishi, na kelele zao hazitukoseshi usingizi, lakini kelele ni kelele tuu zikizdi zina disturb!.

Japo nchi inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu, na kanuni, lakini pia inaongozwa kwa tabia na desturi za utangulizi, precedent, sasa kwa vile tangu tumeanza mfumo wa vyama vingi, tumeongozwa na marais watatu, Ben Mkapa, (RIP), Jakaya Kikwete na sasa John Pombe Magufuli. Hao watangulizi wake wote wawili, waliteua wabunge angalau wawili wa upinzani kwenye kila awamu, kwa Mkapa kuwateua Hamad Rashid na Juma Duni, Kikwete kuwateua James Mbatia na ..., hivyo desturi ni kama tabia, hakuna ubaya na JPM awa hii akateua angalau wapinzani wawili, napendekeza mmoja awe Zitto Zuberi Kabwe na mwingine yule Dada aliyegombea urais, Quuen Sendiga, ili kuwafunga vilimilimi mabeberu kuwa JPM hapendi wapinzani.

Kufuatia Wapinzania kukataliwa na Watanzania, baada ya uchaguzi, kwanza tulipendekeza Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Wapinzani waliposusa, nao tuliwaelimisha Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane! elimu hii ilimwingia Zitto Zuberi Kabwe hivyo nikaona Ziito pekee yake hataweza kuwashawishi Wanzanzibari kuelewa somo, ndipo nikamwandikia barua ya wazi rafiki yangu na mwana fani mwenzangu Mzanzibari Barua ya Wazi Kwa Comrade Ally Saleh, Uchaguzi Umekwisha, Yaliyopita Si Ndwele, Tugange Yaliyopo na Yajayo, Pelekeni Majina, Muijenge Zanzibar Yenu!
Kwa barua hiyo, somo likaeleweka na matokeo sote tunayajua.


Nimempendekeza Zitto kwasababu namfahamu his abilities and capabilities, Zitto ni mzalendo wa kweli Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya...
hivyo waliopanga kamati za oversight ziongozwe na opposition, wana maana yao, Zitto akiingia Bungeni na kuongoza PAC, kiukweli atasaidia sana Bunge, ataisaidia serikali na atalisaidia taifa.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,120
2,000
Kwanini Mheshimiwa Rais asikuteue wewe bwana Paskali kuingia Bungeni na kutetea haki za Waandishi wa Habari?

JPM anaweza kufanya kweli akawatest Zitto na Mbowe ili kuuonyesha Umma namna gani watu wapo tayari kuzikimbia kauli zao hasa pale maslahi yao yanapohusika kwa 100%
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,612
2,000
Sasa ndio umemharibia, kama ni kweli unamtakia mema Zitto Kabwe ungekaa kimya, unafikiri kwa nini Makonda aliachwa muda wote huo bila ya kutumbuliwa ? Ni kwa sababu mlimtaka amtumbue, ...
 

NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,321
2,000
Paschal, nisamehe lakini wewe ni opportunists (msakatonge) tu kama wengine wengi. Unayoita “responsible au credible” opposition ni subjective. Kila jambi ni baya au zuri kutokana na mtizamo. Mtizamo wako huu umekuja baada ya Zitto kushindwa kwenye uchaguzi na hukupenda ashide. Leo unapendekeza achaguliwe! Ni wewe huyu ukichukizwa na Zitto kuandika barua WB na ikawa si mzalendo.

Kuwa na kiwango katika uzandiki na fitna, la sivo utakosa heshima katika jamii kwa sababu hutaeleweka una msimamo gani. Weka msingi katika mambo unayoamini!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom