Mheshimiwa Zitto, vijana tunakupenda lakini mambo haya yanatutia wasi wasi juu yako

Status
Not open for further replies.

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,161
3,157
Bila shaka Zitto hawezi kusahaulika katika historia ya Mabadiliko ya kifikra katika Bunge. Zitto ndie mbuge wa kwanza alieweza kuhoji au kusema direct bungeni kwamba Waziri kasema uongo, yeye ndie alieondoa zana ya uoga bungeni, pia kwa kujiamini alisimamia hoja zake. Nakumbuka baada ya kufukuzwa bungeni, mimi nilitembea kwa miguu kupokea msafara wako kuelekea jangwani. Lakini mimi nina wasiwasi na wewe kama ifuatavyo.

Baada ya ule mkutano wa Jangwani, kwa muda mfupi Mheshimiwa Zitto alijiondoa katika harakati za kueneza chama. Chadema ilifanya mikutano mingi ya kueneza chama kwa slogan mbali mbali, ikiwemo Operation Sangara, M4C nk, katika harakati zote hizi Zitto Kabwe hakuonekana kabisa. Wakati Viongozi wa Chadema wakiangaika kueneza chama huku wakipigwa mabomu Arusha, Morogoro, Iringa nk, Mheshimiwa Zitto kastarehe tu. Mimi binafsi nilikuwepo katika matukio kadhaa ya kupigwa mabomu, hata pale Soweto Arusha nilikuwepo

Wengi tulijiuliza, kwanini Zitto kapotea ghafla?, je katika mafanikio ya Chadema ya sasa mpaka kuweza kusimamisha wagombea kwa mitaa na vijiji vingi na kufanikiwa kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, je Zitto umehangia nini? Unaweza ukasimama ukawaambia Watanzania kuwa katika uenezaji wa Chadema hadi vijijini umechangia ukilinganisha na cheo ulichokuwa umepewa ndani ya chama?

Mimi nasema hivi, vijana wengi tunakupenda lakini kwa dalili hizo nilizozielezea, ukitaka ondoka bwana, maisha yanaweza songa mbele bila wewe. Hata ukiwa na mwanamke mzuri wa sura na umbo, kama akiwa na tabia mbaya, kwa roho ngumu utamwambia kwakheri nakutakia maisha mema.

Mkuu umenena maneno ya busara sana,
wengine wanajitoa ufahamu kwa kulaumu tu zzk kafukuzwa bila kutambua side effects za usaliti wa zzt ktk wakati huu muhimu wa ukombozi wa inchi yetu toka kwa mafisadi!..,what if akisamehewa leo angali kesha anzisha chama chake?,,,haivumiliki
 
Umeomgea vyema mkuu

Ila nina hakika wanazi wake watakuja ni mistari kibao hapo, "cdm bila zitto imekufa" wanasahau kuwa cdm na zitto walishatengana mda mrefu sana na chama kinasonga mbele
 
Inaonekana ni tabia zao hawa wazee wa kigoma,nakumbuka kabulu aliapa cwez kwenda ccm kamwe lakn leo yuko wap?zito nawe rudi kwako ccm.
 
Umeomgea vyema mkuu

Ila nina hakika wanazi wake watakuja ni mistari kibao hapo, "cdm bila zitto imekufa" wanasahau kuwa cdm na zitto walishatengana mda mrefu sana na chama kinasonga mbele

Sawa mkuu, mimi namkubali Zitto lakini ushirikiano wake na Chadema umekuwa ukinitia shaka
 
Bila shaka Zitto hawezi kusahaulika katika historia ya Mabadiliko ya kifikra katika Bunge. Zitto ndie mbuge wa kwanza alieweza kuhoji au kusema direct bungeni kwamba Waziri kasema uongo, yeye ndie alieondoa zana ya uoga bungeni, pia kwa kujiamini alisimamia hoja zake. Nakumbuka baada ya kufukuzwa bungeni, mimi nilitembea kwa miguu kupokea msafara wako kuelekea jangwani. Lakini mimi nina wasiwasi na wewe kama ifuatavyo.

Baada ya ule mkutano wa Jangwani, kwa muda mfupi Mheshimiwa Zitto alijiondoa katika harakati za kueneza chama. Chadema ilifanya mikutano mingi ya kueneza chama kwa slogan mbali mbali, ikiwemo Operation Sangara, M4C nk, katika harakati zote hizi Zitto Kabwe hakuonekana kabisa. Wakati Viongozi wa Chadema wakiangaika kueneza chama huku wakipigwa mabomu Arusha, Morogoro, Iringa nk, Mheshimiwa Zitto kastarehe tu. Mimi binafsi nilikuwepo katika matukio kadhaa ya kupigwa mabomu, hata pale Soweto Arusha nilikuwepo

Wengi tulijiuliza, kwanini Zitto kapotea ghafla?, je katika mafanikio ya Chadema ya sasa mpaka kuweza kusimamisha wagombea kwa mitaa na vijiji vingi na kufanikiwa kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, je Zitto umehangia nini? Unaweza ukasimama ukawaambia Watanzania kuwa katika uenezaji wa Chadema hadi vijijini umechangia ukilinganisha na cheo ulichokuwa umepewa ndani ya chama?

Mimi nasema hivi, vijana wengi tunakupenda lakini kwa dalili hizo nilizozielezea, ukitaka ondoka bwana, maisha yanaweza songa mbele bila wewe. Hata ukiwa na mwanamke mzuri wa sura na umbo, kama akiwa na tabia mbaya, kwa roho ngumu utamwambia kwakheri nakutakia maisha mema.

kweli wewe punguani ulitaka aende akapigwe mabomu shika adabu yako bwana umpeleke mtu kwenye kifo? zzt utamkumbuka tu bado ulishaambiwa ukitaka kumpiga mbwa unampa jina baya mlisha mpa jina hilo tulieni basi mnyolewe ninyi vipi?
 
nkobe fuatilia historia tangu 2009 zitto alipotaka kugombea uongozi....walimtenga! hizo operation zote.....walimtenga! zitto kavumilia mengi sana

then mnatumia kutokuonekana huko kama fimbo!!
 
Umeomgea vyema mkuu

Ila nina hakika wanazi wake watakuja ni mistari kibao hapo, "cdm bila zitto imekufa" wanasahau kuwa cdm na zitto walishatengana mda mrefu sana na chama kinasonga mbele

Mfumuko wa kukua kwa kasi kwa Chadema ni katika miaka hii kabla kidogo na uchaguzi mkuu 2010 mpaka sasa. Tumeona kweli operation nyingi za chama na mfululizo wa mikutano mingi. Haya yote yamefanyika kwa viongozi,wanachama na wapenzi wa Chadema ku sacrifice maisha na mali zao katika harakati hizo. Sasa jee huo ushiriki wa huyu jamaa unaingia katika lipi la kupigiwa mfano? Hakuna.
 
Ukitaka uzi wako upate mvuto hapa jf mzungumzie zitto, lakini uzi kuhusu slaa ,mbowe,lema,tundu lisu hazipati wachangiaji kabisa kwa sababu wamepoteza mvuto, Zitto ndio mwanasiasa pekee wa upinzani anaependwa na watanzania
 
Bila shaka Zitto hawezi kusahaulika katika historia ya Mabadiliko ya kifikra katika Bunge. Zitto ndie mbuge wa kwanza alieweza kuhoji au kusema direct bungeni kwamba Waziri kasema uongo, yeye ndie alieondoa zana ya uoga bungeni, pia kwa kujiamini alisimamia hoja zake. Nakumbuka baada ya kufukuzwa bungeni, mimi nilitembea kwa miguu kupokea msafara wako kuelekea jangwani. Lakini mimi nina wasiwasi na wewe kama ifuatavyo.

Baada ya ule mkutano wa Jangwani, kwa muda mfupi Mheshimiwa Zitto alijiondoa katika harakati za kueneza chama. Chadema ilifanya mikutano mingi ya kueneza chama kwa slogan mbali mbali, ikiwemo Operation Sangara, M4C nk, katika harakati zote hizi Zitto Kabwe hakuonekana kabisa. Wakati Viongozi wa Chadema wakiangaika kueneza chama huku wakipigwa mabomu Arusha, Morogoro, Iringa nk, Mheshimiwa Zitto kastarehe tu. Mimi binafsi nilikuwepo katika matukio kadhaa ya kupigwa mabomu, hata pale Soweto Arusha nilikuwepo

Wengi tulijiuliza, kwanini Zitto kapotea ghafla?, je katika mafanikio ya Chadema ya sasa mpaka kuweza kusimamisha wagombea kwa mitaa na vijiji vingi na kufanikiwa kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, je Zitto umehangia nini? Unaweza ukasimama ukawaambia Watanzania kuwa katika uenezaji wa Chadema hadi vijijini umechangia ukilinganisha na cheo ulichokuwa umepewa ndani ya chama?

Mimi nasema hivi, vijana wengi tunakupenda lakini kwa dalili hizo nilizozielezea, ukitaka ondoka bwana, maisha yanaweza songa mbele bila wewe. Hata ukiwa na mwanamke mzuri wa sura na umbo, kama akiwa na tabia mbaya, kwa roho ngumu utamwambia kwakheri nakutakia maisha mema.

Chama kakikuta kimemlea kimemkuza sasa kakua kaota mapembe ngoja akafunzwe na ulimwengu chadema itaendelea kuwepo .
 
kweli wewe punguani ulitaka aende akapigwe mabomu shika adabu yako bwana umpeleke mtu kwenye kifo? zzt utamkumbuka tu bado ulishaambiwa ukitaka kumpiga mbwa unampa jina baya mlisha mpa jina hilo tulieni basi mnyolewe ninyi vipi?

Kama wangeogopa mabomu ya Polisi wa CCM leo hii CHADEMA ingefahamika hadi vijijini? Punguani ni wewe unaedhani mapinduzi yanakuja kwa uoga
 
Ukitaka uzi wako upate mvuto hapa jf mzungumzie zitto, lakini uzi kuhusu slaa ,mbowe,lema,tundu lisu hazipati wachangiaji kabisa kwa sababu wamepoteza mvuto, Zitto ndio mwanasiasa pekee wa upinzani anaependwa na watanzania

Mchango wake ndani ya Chama?
 
Ukitaka uzi wako upate mvuto hapa jf mzungumzie zitto, lakini uzi kuhusu slaa ,mbowe,lema,tundu lisu hazipati wachangiaji kabisa kwa sababu wamepoteza mvuto, Zitto ndio mwanasiasa pekee wa upinzani anaependwa na watanzania

Eti mvuto mbona unamkosea heshima mkubwa mwenzio awe na mvuto kwani kawa malkia? Tatizo la miafrika kuwajibika mnaona kama ni uasi mpaka uwajibishwe na lawama kibao na ndio maana katika katiba wale walafi na waroho wa madaraka kitu maadili hawakutaka kabisa kukisikia kwa vile wote wanajijua wanaudhaifu kumbuka lusifer ambae ndie mkubwa wa mashwetani alikuwa malaika muimbaji mzuri sana wa Mungu alipokosa maadili na kutaka kujikweza zaidi na kuasi Mwenyezi Mungu alimtupa duniani na kulaaniwa ni mfano tu akili za kuambiwa changanya na zako.
 
hata kwenye hizi changuzi za serikali za mitaa sijaona mchango wa kiongozi wa juu wa chadema . zitto kachangia kiasi kwamba tumepata mitaa mingi. tena Kwa nchi nzima zitto kawa na mchango huo. mtakumbuka swala la escrow limetokea kipindi tunaelekea uchaguzi na hapo ndipo nguvu ya zitto kupitia kamati yake ilipoonekana. tulitembea mtaani Kwa hoja ya kutokuwapa kura wezi wa fedha za umma za escrow. tena zitto kasaidia sana kwani macho yote ya watanzania yalisubili report ya zitto
 
Chadema mpaka wakuone uko kwenye maandamano unapigwa virungu na polisi ndio wakukubali
 
nkobe fuatilia historia tangu 2009 zitto alipotaka kugombea uongozi....walimtenga! hizo operation zote.....walimtenga! zitto kavumilia mengi sana

then mnatumia kutokuonekana huko kama fimbo!!

Ndugu mimi huwa nasema sikizote hakuna kitu nisichokipenda kama unafiq,Zitto ni mtu wa Kigoma mwenzangu lakini tuseme ukweli havumiliki huyu dogo,tunamfahamu sana tangu anaingia kwenye siasa kwa sababu tulimpokea sisi.Alitengwa nanani kama sio yeye kujitenga?.Alianza matatizo muda mrefu sana huyu.Lakushangaza nipale eti anamlaumu Mh Mbowe eti anampiga vita'mbona alipomtoa Ujerumani kumleta kugombea ubunge huku akimfadhiri kuanzia hela yakula mpaka akampa bure gari yakufanyia kampeni Zitto hakumuona Mbowe mbaya?.Nayasema haya kwa sababu namfahamu Zitto na hayo ya Mbowe niliona au mumuulize Zitto ile gari aliyopewa bure na Mh Mbowe alimludishia?
 
Status
Not open for further replies.
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom