Mheshimiwa Mwakyembe Jiandae Kuchukua Nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mheshimiwa Mwakyembe Jiandae Kuchukua Nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fredrick Sanga, Feb 8, 2011.

 1. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135


  Pamoja na kwamba huna mkuu, ni mtu wa staha, na ni mapema sana, lakini kwa kanzi ya kwanza nzito uliyopewa ulionyesha uzalendo wa hali ya juu. Najua kazi ile ya kamati ya umeme ilikuwa hatari sana, lakini uliifanya kwa umakini na uaminifu kwa umma. inawezekana kwa usalama mengine hayakusemwa lakin ulifanya. Unafaa kuchukua uraisi 2015.

  Vigezo:
  Umri unakuruhusu
  Umeshapewa ujiko wa uwaziri, kunjua makucha
  Kule kyela watakataa jinsi wanavyokuhitaji, anza kupiga debe
  Wako wengine wenye sifa lakini umewazidi kielimu Dr.
  Hata CDM wanakuogopa
  Ni mcha Mungu
  Huna Mkuu
  Mtoto wa mkulima
  Unaujua ukweli pamoja na kwamba umebanwa

  Hawa wengine, bahati mbaya watakuwa wamwchoka
  Dr Slaa. Six, Mwandosya, Makamba, Lowasa NK

  tafadhali anza mbele kwa mbele, tena staili ya Magufuli.


  Mwalimu alisema hivi, kama kiongozi amechaguliwa na watu, halafu anasimamia haki za watu waliomchagua basi ana haki ya kuwa kiongozi, lakini kama au hakuchaguliwa na wananchi au amechaguliwa halafu akaacha kusimamia haki za wale waliomchagua, basi anakuwa amepoteza haki ya kuwa kiongozi. huyu alikuwa mwana wa fdilisophia. Alimwambia mtu mmoja aliyekuwa TYL kuwa ni mchafu na hafai kuwa kiongozi, ana tamm ya mali, bado kijana mdogo lakini ana mali nyingi sana, huyu!. Mambo haya ni juu ya wana wa nchi, CCM, CUF, CDM, UDP, TLP, NCCR, NLD NK kuchambua pumba ni ipi na mchele ni upi.

  Tatizo huwa ni kukubali kununuliwa. Vyama inabidi vifute kabisa dhana ya kununua wanachama. Kwani chama ni wanachama, na kinaendeshwa na wanachama. Kama kuna mtu anafikiri kwa visenti vyake atanunua wanachama wote amekwisha. asome alama za nyakati. kuna watu waligombea ubunge kwa pesa nyingi wameshindwa na watu waliokuwa wakichangiwa na wapiga kura.

  Alama za nyakati, zinaonyesha Mheshimiwa Mwakyembe haitaji kuonga hata senti tano kwa mtanzania. Ila ajue kwamba asiposhughulikia swala hili hata nbinguni ataulizwa.
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hizo zenye red ni vigumu kudhibitisha

  mfano unajuaje ucha mungu wa mtu? (wewe mungu?)

  Kuogopwa na cdm? siyo sifa hata kidogo na hata mtoto wa mkulima siyo sifa hata kidogo!
   
 3. czar

  czar JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona hujui au umesahau namna ccm wanavyompata mgombea wao. Pia utakuwa hukumbuki namna wajumbe wanaopiga kura wanavyopatikana ccm.
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  umetumwa? mbona siasa na fitina zimehamia bungeni saizi wee unaandika wehu?
   
 5. i

  ibange JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  dr mwakyembe akitaka kuwa rais agombee kwa tiketi ya chadema
   
 6. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Wanafikiria kumtemesha huo uwaziri namba 2 sembuse urais!
   
 7. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Dalili zinajionesha wazi!!!
   
 8. Ndaki

  Ndaki Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: May 5, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  huwezi kuwa mchapa kazi katikati ya wavivu, kama thithiem walivyo ndivyo utakavyokuwa! Thi mwakyembe wala magufuli wote sisitimu inawakataa!
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ndio Naelewa kwamba kupenya ndani ya SISIMU ni ngumu sana, lakini kuna namna mbili kuu za kupenya.
  1. Kurubuni kwa kutumia mapesa
  2. Kufanya mamboyanayokubalika na umma

  Hiyo ya pili ilitumika na Mhe Sarwati kule Babati, Dr Slaa, Shibuda na wengine. Issue sio chama. ukishakuwa tayari, na watu wamekukubali watakuita cdm au kwingine. Lakini ningependa aelewe anakubalika na hata akitemwa na chama fulani anakubalika.

  Hapa ni Tanzania kwanza sio Chama kwanza
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wehu is a relative term, usijali sana.
   
 11. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  [QUOTE=Topical;1599596]Hizo zenye red ni vigumu kudhibitisha

  mfano unajuaje ucha mungu wa mtu? (wewe mungu?)
  Mungu anajua

  Kuogopwa na cdm? siyo sifa hata kidogo na hata mtoto wa mkulima siyo sifa hata kidogo![/QUOTE] kama Dr anavyogopwa na CCM ni sifa

   
 12. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mkuu hiyo ni kweli kabisa Ndg yangu Mwakyembe changamka ndo kumekucha hivyo!!!!!!!!!!Kwa uadilifu huna mpinzani jipange uokoe hili jahazi linazama. Huyu nahodha wetu hajui cha omo wala, tezi wala ngamani. Linazama dalili ni za wazi kabisa. Kila sifa unayo, kama ni kutumikia wananchi ni Tanzania yote siyo watu wa Kyela peke yao. Okoa jahazi wote wamelala usingizi wa pono, hawaoni mbele tutakwama , shika usukani mabaharia uwape mwelekeo !!!!!!!
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi watanzania wenzangu, mnajua ya kwamba ni vizuri kuwa na mawazo ya mbeleni, kwani mambo ni mabaya sana. Angalieni upinzani unavyokwenda, tuahitaji Raisi atakyeweza kuishi na upinzani. Raisi anayechukia mafisadi, raisi anayependa bunge makini. Najua sasa hivi kunawanaolia na kufurahi, lakini tuangalie dhamiri zetu.

  Nilisema Salim anazeeka, mwandosya kachoka, Ole labda sijui, Slaa nae anazeeka, Lipumba amechoka. Mimi nasema katika Waheshimiwa wa umri wa kati, Huyu ndiye.
   
 14. mwanaharakati m

  mwanaharakati m Member

  #14
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HAIWEZEKANI...........labda MAFISADI wote wawe wameuawa by 2015
   
 15. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Uzee wa mtu au kuchoka kwa mtu kunatokana na nini?
   
 16. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hata Makamba yuko akilini mwako kwamba anaweza kuwa rais wa Tanzania? Au unamaanisha Makamba Jr?
   
 17. Lakitaa

  Lakitaa Member

  #17
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nadhani mwenzetu amekurupuka sana awe rais kupitia ccm , labda hizo ni njozi tu alizo nazo!
   
 18. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kumbe umeona? Makamba au magurudumu? majatani /? hili jina ni chafu sana wala halihitajiki kusikika kwa watz
   
 19. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,493
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe na Magufuli ni majoka ya kibisa ......waoga mno ...! yaani wako tayari Yusuf makamba achokue fomu za urais lakini si waoo... mie baado siwaami...,
  Ni watu wa kujikomba tuuuu ili wapate uwaziri, jawana ujasiri wa kugombea uraisi hao....utaona...
   
 20. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hapo red
  Unajua hakuna mtu anayeweza kujielewa asilimia 100 kwamba anaweza kukubalika katika mfumo wetu huu ambao akili nyingi, busara na maarifa vimelala makaburini bila kutumika. Sasa wanapotokea watu jasiri, wakafanya mambo ya kupendeza basi ni sisi wananchi tunaweza kuanza kuwapamba ili ijasiri uweze kukua.

  Ujasiri unazaliwa, unakua na unaweza kufa vilevile.

  Wako wengine wazuri, laki tayari tunae huyu. Watu wanaojikomba hawawezi kuriski nafasi zao. Nafikiri umeona mfano wa Mzee Six, Mhe Ole, na Dr Weapon jinsi walivyojitoa bile uoga. Lakini huyu mwakyembe alirisk maisha yake. Hebu jiweke wewe kwenye nafasi yake.

  Mwamdosya = old but modarate
  Pombe = Middle but is going old
  Ole = Is getting quet
  Pius, John, Salim, Ana are getting old though wise

  I see Mwakyembe very potential, even if need be through CDM or CUF etc
   
Loading...