Mheshimiwa Mwakyembe Jiandae Kuchukua Nchi

Mheshimiwa Mwakyembe Jiandae Kuchukua Nchi

kumbe umeona? Makamba au magurudumu? majatani /? hili jina ni chafu sana wala halihitajiki kusikika kwa watz
Yeye akipewa atakubali, lakini mimi sijampendekeza na nafikiri wewe unamjua vizuri. mimi simjui.:clap2:
 
Pamoja na kwamba huna mkuu, ni mtu wa staha, na ni mapema sana, lakini kwa kanzi ya kwanza nzito uliyopewa ulionyesha uzalendo wa hali ya juu. Najua kazi ile ya kamati ya umeme ilikuwa hatari sana, lakini uliifanya kwa umakini na uaminifu kwa umma. inawezekana kwa usalama mengine hayakusemwa lakin ulifanya. Unafaa kuchukua uraisi 2015.

Vigezo:
Umri unakuruhusu
Umeshapewa ujiko wa uwaziri, kunjua makucha
Kule kyela watakataa jinsi wanavyokuhitaji, anza kupiga debe
Wako wengine wenye sifa lakini umewazidi kielimu Dr.
Hata CDM wanakuogopa
Ni mcha Mungu
Huna Mkuu
Mtoto wa mkulima
Unaujua ukweli pamoja na kwamba umebanwa

Hawa wengine, bahati mbaya watakuwa wamwchoka
Dr Slaa. Six, Mwandosya, Makamba, Lowasa NK

tafadhali anza mbele kwa mbele, tena staili ya Magufuli.
Anaweza kufaa, lakini katika sisiem sidhani kama atapata nafasi.
 
hivi ni kweli mwakyembe ana huruma na nchii? au baada ya kampuni yake ya kufua umeme kupigwa bao na richmond ndo nae akajifanya kuwa na hasira??

nahisi undumilakuwili mwingi sana nchini kwetu, angalikuwa mpiganaji wa kweli angetshatoka ccm, angekataa uwaziri au angemsapoti zito kipindi kile cha buzwagi, ila kwa kua maslahi yake by then hayakuguswa hakupiga kelele

tuliona uingereza jinsi mawaziri waliokuwa wakimpinga tony blair kwenye suala la uingereza kujiunga na vita vya iraki, mfano robin cook, wakijiuzulu nafasi zao kwa kua hawakuridhishwa na maamuzi mabovu ya blair, sasa huyu mwakyembe kwa nini aendelee kuwemo kwenye baraza la kikwete kama hakubaliani na maamuzi ya kikwete??kuna mambo mengi nyuma ya pazia!!!!
 
Pamoja na kwamba huna mkuu, ni mtu wa staha, na ni mapema sana, lakini kwa kanzi ya kwanza nzito uliyopewa ulionyesha uzalendo wa hali ya juu. Najua kazi ile ya kamati ya umeme ilikuwa hatari sana, lakini uliifanya kwa umakini na uaminifu kwa umma. inawezekana kwa usalama mengine hayakusemwa lakin ulifanya. Unafaa kuchukua uraisi 2015.

Vigezo:
Umri unakuruhusu
Umeshapewa ujiko wa uwaziri, kunjua makucha
Kule kyela watakataa jinsi wanavyokuhitaji, anza kupiga debe
Wako wengine wenye sifa lakini umewazidi kielimu Dr.
Hata CDM wanakuogopa
Ni mcha Mungu
Huna Mkuu
Mtoto wa mkulima
Unaujua ukweli pamoja na kwamba umebanwa

Hawa wengine, bahati mbaya watakuwa wamwchoka
Dr Slaa. Six, Mwandosya, Makamba, Lowasa NK

Tafadhali anza mbele kwa mbele, tena staili ya Magufuli.

Hana uwezo wa kuwa raisi ingawa ana Phd, Rais mtarajiwa ni Dr. John Pombe Magufuli
 
Mwakyembe akichukua nchi itakuwa Zimbabwe.Je Watanzania mko tayari kumpa Mwakyembe Nchi?Hawa watu wa aina hii hawana asili wala fasili!
 
Lile la ripoti limetuthibitishia bila shaka, sasa tusubiri kipindi hiki cha mpito

Anaweza!
 
Nani alikwambia Richmond iliipiga bao kampuni ya Mwakyembe, na hiyo kampuni inaitwa nini. Sio vizuri kubeza watu wanaojiheshimu, mnawakatisha tamaa na kuwaachia nchi mafisadi. Eti kwamba mwakyembe akichukua nchi itakuwa kama Zimbabwe si kweli, huyu kiumri ni mdogo ukilinganisha na Mgabe Robert, ndio maana sipendi Raisi Mzee au Kijana sana. Kinachomsumbua Mugabe ni Uchovu. Nimekuwa zimbabwe wakati Robert akiwa na umri wa wastani,Zimbabwe ilikuwa bomba kwelikweli. Wewe umefika Zim.

Mhe Pombe anaweza uwazuri mkuu, akiwa na mwakyembe mambo yataiva kwelikweli. Lakini sasa naona JF mmeanza kuja na mawazo mazito.

Kukataa uwaziri: Hili lisingekuwa jambo la maana, hata Sokoine angeweza kukataa uwaziri, nafikiri hii ni nafasi ya kutumikia umma mzima wa Tanzania. Ila ukiingiliwa katika kutekeleza wajibu wako you tender resignation kama Mh Lyatonga.

Bado Mwakyembe yuko juu.
 
Ahamie CHADEMA basi. Akija tutampa hiyo nafasi na kwa kweli atashinda. Ila with CCM, hapana...
 
Ahamie CHADEMA basi. Akija tutampa hiyo nafasi na kwa kweli atashinda. Ila with CCM, hapana...

Mimi ninajua kwamba akija chadema mtampa nafasi ya kugombe, kwa sababu mpaka sasa kuna nani ambaye amesimama katika nafasi nzuri kama yeye.

Ana msimamo
Msomi
Mnyenyekevu kwa watu wa kawaida
Mkali sana kwa mafisadi, lakini kwa lugha ya staha
Anasoma riport zake na kuzielewa
Anapenda siasa safi

Tatizo hajapewa rungu 100%.
 
Mkuu hiyo ni kweli kabisa Ndg yangu Mwakyembe changamka ndo kumekucha hivyo!!!!!!!!!!Kwa uadilifu huna mpinzani jipange uokoe hili jahazi linazama. Huyu nahodha wetu hajui cha omo wala, tezi wala ngamani. Linazama dalili ni za wazi kabisa. Kila sifa unayo, kama ni kutumikia wananchi ni Tanzania yote siyo watu wa Kyela peke yao. Okoa jahazi wote wamelala usingizi wa pono, hawaoni mbele tutakwama , shika usukani mabaharia uwape mwelekeo !!!!!!!

Mkuu sisiemu ni sikio la kufa. Watu wenye muelelekeo wa kuiokoa ccm na pia safi hawawataki. Unamuongelea mwakyembe, wakati wenzako sisiemu wanakesha kufikiri jinsi ya kumrudisha Lowasa dimbani.
 
Mkuu sisiemu ni sikio la kufa. Watu wenye muelelekeo wa kuiokoa ccm na pia safi hawawataki. Unamuongelea mwakyembe, wakati wenzako sisiemu wanakesha kufikiri jinsi ya kumrudisha Lowasa dimbani.
Ngoja nikwambie, CCM hata uchaguzi uliopita cha moto wamekiona, pamoja na mbinu zao zote, ruzuku imepungua. Sababu kubwa ni huyo unayamtaja. Sasa tunahitaji kuwatia moyo wazalendo kwamba iwe ndani au nje ya CCM mambo ndo yanaanza. Tusingoje 2013, tuanze kupiga debe kwelkweli sasa hivi ili tuone chama gani kitamwai, Huyu Mheshimiwa, Dr. H Mwakyembe.
 
Naomba Mwakyembe aongezewe ulinzi, kwa sababu ndio anakwenda sasa kuchukua nchi 2015. Mashehe, Maaskofu muanze kumuombea dua akomae zaidi.
 
hapo red
unajua hakuna mtu anayeweza kujielewa asilimia 100 kwamba anaweza kukubalika katika mfumo wetu huu ambao akili nyingi, busara na maarifa vimelala makaburini bila kutumika. Sasa wanapotokea watu jasiri, wakafanya mambo ya kupendeza basi ni sisi wananchi tunaweza kuanza kuwapamba ili ijasiri uweze kukua.

Ujasiri unazaliwa, unakua na unaweza kufa vilevile.

Wako wengine wazuri, laki tayari tunae huyu. Watu wanaojikomba hawawezi kuriski nafasi zao. Nafikiri umeona mfano wa mzee six, mhe ole, na dr weapon jinsi walivyojitoa bile uoga. Lakini huyu mwakyembe alirisk maisha yake. Hebu jiweke wewe kwenye nafasi yake.

Mwamdosya = old but modarate
pombe = middle but is going old
ole = is getting quet
pius, john, salim, ana are getting old though wise

i see mwakyembe very potential, even if need be through cdm or cuf etc

kwa kweli huyu muheshimiwa anafaa, anastahili kuwa na yeye ni mgombea, lakini kwa chama chake kilivyo kwa sasa cjui....kama hili linawezekana....kile chama kimekamatwa na majambazi cmnakumbuka walivyomkosasa na lory wammalize...lile genge ni ngumu ndani ya chama kile kuruhusu mtu mwadilifu amabaye hanunuliki ashike hatamu za uongozi wao wakiwa hai...kwasababu ni hatari kwa maslahi yao, wamefanya madudu sana, na wanajua kitendo cha wao kuondoka kwenye madaraka ni kwamba na wao watafute nchi ya kuishi hawatakubali kupitia chama chao atoke mtua ambaye hatakuwa tayari kulinda maslahi yao haiwezekani hata kidogo.....basi kama watampitisha na akapita mwakyembe ujue na yeye kashanunuliwa..........hii ndio hali halisi kwa sasa ndani ya hili genge ovu. Mwakyembe anafaa akiwa nnje ya hili genge na si vinginevyo......
 
Mhe Dr. Mwakyembe na Chama Chake:

Kwanza napenda kuwapongeza wana JF kwa kuwa makini kuona kwamba chama cha mgombea kinaweza kuwa ni kikwazo, kwa yeye binafsi kupenya. tuliona kwa Dr salim A mara mbili. Ila tatizo lingine ni watanzania, huwa sio wanaharakati wa mambo haya mpaka dakika za mwisho halafu inakuwa ngumu sana. Tukianza kuimba mapema tutawavunja nguvu Mafisadi.

CDM najua ya kwamba wapo makini
CCM wanhitaji kurejea vission, mission, philosophy and main objective za chama
CUF wabalance composition
Na wengine wajiandae

lakini, kimsingi tunakubaliana kwamba, sasa tuanze na viomgozi bora, kiliko bora viongozi wa chama fulani. "Chama sio baba yako wala mamayako" JK:msela:
 
MZAHA WA CUF KUWA 'CHAMA TAWALA' NA 'CHAMA CHA UPINZANI' KWA WAKATI MMOJA KWA KIPINDI KILE KILE NDANI YA TAIFA MOJA!!!




22.JPG

525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.

Mtu asitfute njia ya mkato wa kutafuta CHADEMA kusaidia kusafisha uchafu wa utawal wa kisheria na kidemokrsia kama ambavyo CCM na CUF walivyojisababishia kwa MWAFAKA WA MAKAMBA kule Visiwani na sasa Mwafaka huo ulivyowaletea mikanganyiko ndani ya bunge la Muungano na hata kutishia kuvunja muungano wetu misingi ya kisheria itakapolazimika kuzingatiwa.

Kwa mtaji wa kitendo tu cha bunge letu tukufu kule Dodoma ITAKAPOSHAWISHIKA KULAZIMISHA KUBADILISHWA KWA KANUNI YA BUNGE inayozungumzia sifa na muundo wa chama rasmi cha Upinzani bungeni basi moja kwa moja tangu hapo tujue kwamba taifa letu litakua limeingia moja kwa moja KATIKA MGOGORO WA KIKATIBA ambayo matokea yake huenda yasipendeze sana kwa wengi wwetu.

Hakika mara baada ya CCM kulazimisha ndoa kati ya CUF na CHADEMA huku bara wakati wakijua kwamba kula Zanzibar ndoa ni kati ya CUF na CCM basi naona kuna uwezekano mkubwa wa WA KUZUKA KWA MISURURU YA KESI JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA NA KUHITAJIKA KWEPO KWA MAHAKAMA YA KIKATIBA NCHINI AU WATU NA VIKUNDI VISIVYOAFIKI HIYO HALI KULAZIMIKA KWENDA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUTAFUTA HAKI ILI KUNUSURU MUUNGANO WETU TANZANIA.

Mhe Kafulila, ulichukua angalau muda wako kuyafikiria haya kabla ya kuanza na mazungumzo yako kule bungeni???????????? Jamani tusipende kuleta majibu rahisi sana kwa swala ngumu kama hili.

Mwafaka wa Zanzibar ulikua na nia nzuri kwa kutulete utulivu kule visiwani lakini kwa kuwa wahusika huenda walikosa ushauri mzuri kisheria na matokeo ya utekelezaji wa mwafaka wenyewe ndani ya muungano wetu hasa kwa vyama vingine ambavyo havikuhushishwa kwenye mwafaka huo ndio leo hii imetufikisha hapa.

Nakumbuka sana Mhe James Mbatia alilipigia sana kelele wakati ule akitaka vyama vyote vya upinzani vihusishwa lakini kwa bahati maya sana hakusikilizwa na CCM. Inamaana Mbatia hakumpa briefing mbunge wake Kafulila juu ya ukwel huo???

Kwa mantiki hii hata mtu akilazimisha kubadilisha kanuni za mchezo bungeni wakati timu tayari ziko uwanjani tayari kucheza, jamba ambalo kwanza si la kawaida na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi ndani ya himaya ya nchi za jumuiya ya madola, pamoja na yote CUF bado haingii kisheria ndani ya kambi ya upinzani mpaka kwanza ama:

(1) CUF kijivue kutoka ndani ya mwafaka na CCM kule visiwani.

(2) au Serikali itangaze wazi kwamba kwa mwafaka wa CCM na CUF basi tayari walishavunja Muungano wetu na Zanzibar ili Watanzania tujue kabisaa kwamba kumbe mpaka sasa hatuna muungano ndipo CUF ipate kukubalika Bara kama chama cha upinzani bila kutupa jicho kwamba kule Visiwani chama hiki kimekaeje bungeni huko.

(3) Na kama hoja namba mbili ndio ukweli wa mambo ulivyo nchini mwetu basi kabla CUF haijavuka sakafu la bunge letu la muungano kule Dodoma kuja upande wa upinzani, kwa maana ya kwamba yanayoendelea bunge la Zanzibar sasa ionekane kana kwamba haituhusu huku Bara, basi kwanza ni sharti wabunge wote wa Zanzibar waondoke bungeni hapo bila kujali chama kilichomleta hapo bungeni.

Watanzania tuliowengi sana hatupendi hata kidogo tunu letu 'Muungano' kuvunjwa na mtu yeyote lakini mantiki hoja yenyewe inatuelekeza hivyo kwamba CUF kuingia kambi ya upinzani huku bara basi maana yake Muungano ulishavunja na wabunge wote kutoka Visiwani ni sharti waondoke bungeni Dodoma.
 
Ndio Maana ni vizuri kuamuangali kiongozi kwa dhamira sio maneno tupu, Kafulila mineno mirefu sana bila analysis. Viongo vijana wana hitaji malezi sana.

Ndio maana nilisema watu wa makamu ya kati, waliopitia misukosuko mingi ndio wanafaa kuongoza nchi.

Kiongozi Mzuri
Akipewa jukumu analifanya kimakini
Ana falsafa fulani
anasimama kwenye falsafa (rationality between charisma and character)
Si mlafi wa mali
Ana Utu
Sio Mroho wa Madaraka
Ana staha
Huonyesha watu kwa mfano (Hujitoa muhanga)
NK

Jamani tusipo mlinda na kumconvince Dr, H Mwakyembe tutaliwa, ana nguvu ya umma. Hii ni ujumbe kwa wazalendo wote.:embarrassed:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom