Mhe. Rais Magufuli, naomba kila mwisho wa mwezi tupate hotuba zako

Hotuba zako zinatufunza mengi. Hotuba zako zinatupa hamu ya kuchagua vyema 2020 ndani ya CCM na hata kwenye uchaguzi mkuu. Hotuba zako-na ukweli wako zinatufikirisha na kutuongoza kwenda kwenye tafakari kali.

Hotuba zako zinatuonesha picha tuliyoichora wenyewe mwaka 2015. Hotuba zako zinatukumbusha push-ups zako na hata ahadi zako. Hotuba zako zinatufariji; zinatukereketa;zinatuwasha hasira; zinatuburudisha; zinatupa mwanga wa kuona anga.

Natoa pendekezo kuwa Rais Magufuli atuhutubie kila mwisho wa mwezi ili tuendelee na tafakuri yetu ya kitaifa. Napendekeza asiandike hotuba zake ili iwe rahisi kuzungumza mambo tofautitofauti na kwa watu mbalimbali.

Nawasilisha hoja ya haja!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Bora anyamaze kwa kauli zile za Bukoba ndio atazidi kuharibu. Maana mie kwenye ziara ile nimeambulia mambo makuu yafuatayo, Serikali haiwezi kuwasidia waathirika, Mbunge kama anatakaa nafuu ya vifaa vya ujenzi kwa wananchi ajenge kiwanda chake, Katerero na mto ngono.
 
Ulicho elewa sio sahihi kiongozi, mh rais hajakataa serikali kusaidia wahanga wa Bukoba, hoja ya msingi ya mh. Rais ni baadhi ya watu wanatumia ishu ya tetemeko kuhalalisha madai ya siyo na msingi kwa serikali, watu wengine wanapotosha jamii ya watanzania kupitia kauli za rais
 
HOJA YAKO NI UTENDAJI KAZI WA RAIS AU MAMBO MENGINE?? TUJENGE HOJA ZA MSINGI tusuzungumze kwa kigezo cha kuzungumza
 
Magufuri ni mkweli na tatizo LA Watanzania ni kutokupenda kuambiwa ukweli.......tunapenda snaa blah blah....

Magu we Rais mpka 2035
 
Wewe ni nani hadi umpangie rais cha kufanya. We si kila siku unamtukana hapa wewe, au umeamua kusilimu
 
Hotuba zako zinatufunza mengi. Hotuba zako zinatupa hamu ya kuchagua vyema 2020 ndani ya CCM na hata kwenye uchaguzi mkuu. Hotuba zako-na ukweli wako zinatufikirisha na kutuongoza kwenda kwenye tafakari kali.

Hotuba zako zinatuonesha picha tuliyoichora wenyewe mwaka 2015. Hotuba zako zinatukumbusha push-ups zako na hata ahadi zako. Hotuba zako zinatufariji; zinatukereketa;zinatuwasha hasira; zinatuburudisha; zinatupa mwanga wa kuona anga.

Natoa pendekezo kuwa Rais Magufuli atuhutubie kila mwisho wa mwezi ili tuendelee na tafakuri yetu ya kitaifa. Napendekeza asiandike hotuba zake ili iwe rahisi kuzungumza mambo tofautitofauti na kwa watu mbalimbali.

Nawasilisha hoja ya haja!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
SIKU HIZI HAUIPONDI SERUIKALI YA MAGUFULI UMEKUWA MSHAURI WAKE?
 
Back
Top Bottom