Mhe. Rais Magufuli, naomba kila mwisho wa mwezi tupate hotuba zako

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
18,727
2,000
Naomba ombi langu afikishiwe Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe John Magufuli.

Sisi kama wananchi unaotuongoza kila mwisho wa mwezi tungependa kusikia japo kwa muhtasari hotuba kutoka kwako kama mkuu wa nchi na tuweze kufanya tathmini nzuri kuhusiana na yanayojiri katika utawala wako pia uelekeo wa nchi yetu kwa Ujumla.

Huu utamaduni tuliuona katika tawala zilizopita na tungependa pia uendelezwe hata katika utawala wako huu,

Tunaamini hili litafanyiwa kazi ama hata kutolewa ufafanuzi.

Nawasilisha ombi kama Mwananchi wa kawaida!!
 
cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,812
2,000
Itakuwa poa hata ya kila baada ya miezi 3, maana Mkuu wetu naona yupo busy kutumbua na kunyanyua nchi.

Ila pia alitoa ahadi ya kuita mapaparazi kuongea nao kila baada ya muda.
 
Andrew Nyerere

Verified Member
Nov 10, 2008
3,010
2,000
Ni wazo zuri. Lakini siyo lazima.
Utamletea presha rais afikirie jambo la kusema.
Matukio yanapotokea raise atakuwa na jambo la kusema. Kama kwa mfano yule Kamanda wa Majeshi wa Malawi alivyozungumza Jana.
Akiendelea kuzungumza namna ile sooner or later rais itabidi ajibu.
Inatosha rais isemwe Leo atahutubia au leo ataongea na waandishi wa habari.
Regular talks zitasababisha rais atumbue watu ambao hakupanga kuwatumbua.
 
Jimmy George

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,738
2,000
Unataka uwe unasikia yale yale ya kuwa tumenunua ndege na tuna mpango wa kununua zingine wala hasemi ajira vipi na suala la kuachia hela mtaani atafanyaje
 
accused

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
2,506
2,000
Mkuu unataka kukata tamaa na nchi yako? Tumuache tu maana comedy zake zinatuumiza wengine.
 
shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
7,904
2,000
Naomba ombi langu afikishiwe Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe John Magufuli.

Sisi kama wananchi unaotuongoza kila mwisho wa mwezi tungependa kusikia japo kwa muhtasari hotuba kutoka kwako kama mkuu wa nchi na tuweze kufanya tathmini nzuri kuhusiana na yanayojiri katika utawala wako pia uelekeo wa nchi yetu kwa Ujumla.

Huu utamaduni tuliuona katika tawala zilizopita na tungependa pia uendelezwe hata katika utawala wako huu,

Tunaamini hili litafanyiwa kazi ama hata kutolewa ufafanuzi.

Nawasilisha ombi kama Mwananchi wa kawaida!!
Magufuli angekuwa ANASHAURIKA hilo angelitendea kazi tangu mwanzo.
"Inachokesha"
Afanye apendavyo!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom