Mhe. Rais Magufuli, naomba kila mwisho wa mwezi tupate hotuba zako

Naomba ombi langu afikishiwe Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe John Magufuli.

Sisi kama wananchi unaotuongoza kila mwisho wa mwezi tungependa kusikia japo kwa muhtasari hotuba kutoka kwako kama mkuu wa nchi na tuweze kufanya tathmini nzuri kuhusiana na yanayojiri katika utawala wako pia uelekeo wa nchi yetu kwa Ujumla.

Huu utamaduni tuliuona katika tawala zilizopita na tungependa pia uendelezwe hata katika utawala wako huu,

Tunaamini hili litafanyiwa kazi ama hata kutolewa ufafanuzi.

Nawasilisha ombi kama Mwananchi wa kawaida!!
Badala ya kuomba maisha bora zaidi ya hayo ulionayo,unataka hotuba,watu wengine ni wa ajabu sana
 
Maisha bora tiyari ninayo mkuu wala sisubirii Magufuli aniletee, mimi nimetamani ule utamaduni uliokuwepo awali uendelee kuwepo.

Pole sana kwako kama bado unasubiria maendeleo uletewe na Wanasiasa
 
Aisee nitafurahi maana kila mwezi walau nitakuwa na uhakika wa siku moja ya kucheka sana na kuondoa stress!! Nakuunga mkono mtoa hoja.

Imagine kila mwezi mtu upewe offer ya kufurahi sana kwa siku moja.
Najua upendi kumsikia lakini huna namna maana yule mwizi uliyemtegemea hakushinda pole sana vumilia mpaka 2025
 
Huwa ananichekesha mkuu, mimi huwa namsikilizaga ili nicheke na kwakweli huwa sibanduki kwenye tv akiwa anahutubia.
 
Kwenye hizo hotuba zake za mwisho wa mwezi ataongea nini zaidi ya kuwapa maneno mabaya ya kuwakarahisha.
 
Maisha bora tiyari ninayo mkuu wala sisubirii Magufuli aniletee, mimi nimetamani ule utamaduni uliokuwepo awali uendelee kuwepo.

Pole sana kwako kama bado unasubiria maendeleo uletewe na Wanasiasa
Huo utaratibu ulikusaidia nini??mie umenipa pole kama nasubiri maendeleo niletewe na wanasiasa,halafu unamuomba rasmi mwanasiasa awe anakuhutubia kila mwezi!
 
Haunisaidii chochote mkuu, hata hivyo napenda kusikia kutoka kwa viongozi waliopewa dhamana hata kama sikuwachagua mimi
 
Kama hotuba zenyewe ndio zile, bora akae tu kimya hadi 2020
 
Naomba ombi langu afikishiwe Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe John Magufuli.

Sisi kama wananchi unaotuongoza kila mwisho wa mwezi tungependa kusikia japo kwa muhtasari hotuba kutoka kwako kama mkuu wa nchi na tuweze kufanya tathmini nzuri kuhusiana na yanayojiri katika utawala wako pia uelekeo wa nchi yetu kwa Ujumla.

Huu utamaduni tuliuona katika tawala zilizopita na tungependa pia uendelezwe hata katika utawala wako huu,

Tunaamini hili litafanyiwa kazi ama hata kutolewa ufafanuzi.

Nawasilisha ombi kama Mwananchi wa kawaida!!
Tehteheh! Una nia ya kuiangamiza Lumumba wewe sio bure, hujui kama hotuba moja ya huyo mheshimiwa inapukutisha wanachama na wapenzi wa ccm zaidi ya 200,000. Akihutubia miezi 40 katika miezi yake iliyobaki ni 200000*40=8,000,000+; hii ni idadi ya kura alizopata 2015. Sasa wazo lako likikubaliwa then 2020 atapigiwa kura na nani? Jecha? Sisi wana ccm hatutakubali wazo lako.
 
""Wafanyakazi hewa,wanafunzi hewa,wakulima hewa, waathirika wa tetemeko hewa, wafugaji hewa, haiwezekani, Mungu ibariki Afrika, mungu ibariki tanzania.""
 
Kweli mkuu ngoja nijinyamazie maana kung'olewa fizi na plaizi unapata maumivu na uchungu mkali kuliko ule wapatao mama zetu huko leba.
Mkuu angalie wasije wakaku wilimboka maana ni soga za mtikisiko wa pwani kwelikweli
 
Naomba ombi langu afikishiwe Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe John Magufuli.

Sisi kama wananchi unaotuongoza kila mwisho wa mwezi tungependa kusikia japo kwa muhtasari hotuba kutoka kwako kama mkuu wa nchi na tuweze kufanya tathmini nzuri kuhusiana na yanayojiri katika utawala wako pia uelekeo wa nchi yetu kwa Ujumla.

Huu utamaduni tuliuona katika tawala zilizopita na tungependa pia uendelezwe hata katika utawala wako huu,

Tunaamini hili litafanyiwa kazi ama hata kutolewa ufafanuzi.

Nawasilisha ombi kama Mwananchi wa kawaida!!
Unataka kusikia nini?
 
Back
Top Bottom