Rais Samia anafanya vizuri ila kuna mambo anatakiwa kurekebisha

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Naomba nizungumzie Mama wa Taifa, Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania kama nionavyo mimi;

1. Tabia binafsi
Mama Samia Suluhu Hassan ameumbwa na hofu ya Mungu, ameumbwa na utashi wakuona baya kwake laweza kuwa baya kwa wengine hivyo hana sababu ya kuhukumu.

Ameumbwa na moyo wa kusamehe huku akijaaliwa wingi wa huruma ya mama kwa watoto na familia yake, familia ya jirani, na familia hata za asiowajua. Ni mama kama walivyo wamama wengine walioandikwa kwenye vitabu vitakatifu wakiwemo waliolia na kwenda kaburini kwa Yesu.

2. Tabia ya kisiasa
Mhe. Samia Suluhu Hassan ni mwanasiasa aliyekuzwa na siasa; ni mwanasiasa anayependa siasa za mrengo wa wastani mwenye mbinu za kutokuonyesha dhahiri shahiri kuwa siasa ni chuki. Anao uwezo mkubwa wa kumficha mpinzani wake asiweze kujua kama ipo chuki ndani yake.

Amelelewa na chama cha siasa ambacho kimekwama kutafsiri maisha ya wananchi katika kesho na hivyo pamoja na maono yake, pamoja na ucha Mungu, pamoja na kuwa mama amejikuta sehemu ya tabia zake binafsi nzuri zimefutwa na aina ya wanasiasa wanaomzunguka ndani ya chama chake.

Kwa upande mwingine, mama anayo huruma, anao watu wengi waliomfanya afike hapo alipo kisiasa, ni kwa muktadha huo ndipo amekwama kutenganisha kati ya ufanisi wa baba na ufanisi wa watoto. Amejikuta akishindwa kutengeneza safu nzuri ya kisiasa badala yake amezungukwa na safu nzuri ya watoto na ndugu wa walezi wake kisiasa.

Amejikuta anapata wasaidizi wasio na sifa na ambao wanaona mchango wa wazazi wao kwa mama ni lazima urejeshwe kama fadhila

3. Katika uongozi mkubwa wa nchi
Mama anafanya vizuri sana kama Rais wa nchi, amebalance sana siasa za nchi kufikia mahali anaelekea kufikia kiwango cha juu cha uvumilivu kwenye mishale ya kisiasa. Amesimama wakati wote kama Mama, Baba, Mlezi na Mkuu wa nchi.

Amejitahidi sana hata kama si kutoka moyoni ila anatamani uwepo uhuru wa kisiasa nchini utakaoponya majereha ya mtangulizi wake. Changamoto aliyonayo katika nafasi ya Urais ni kuongoza watu wasiopenda kufanya kazi, wasiopenda kujisomea na wasio na mfumo rasmi wa kupima ufanisi.

Mhe. Rais Magufuli alipotaka nchi isonge mbele aliamua kusoma sana hivyo watendaji waliochini yake nao wakawa wanalazimika kuongeza umakini kwenye shughuli zao, japo aliwajengea uoga usio na tija. Mama yetu Samia katika nafasi ya juu aliyonayo analazimika kusoma sana. Analazimika kuwa mrasimu kwenye maamuzi ili walio chini yake wajipe muda wa kusoma nakuwasilisha kwake jambo lenye tija. Wasiwasi wangu nilionao ni endapo Mhe. Rais ataweza kuvaa uhusika huu wakufanya analysis has kwenye mambo nyeti?

Tumeona suala la bandari, mama anaona maendeleo mbele lakini mkataba haionyeshi maendeleo mbele, tumeona leo uwanja Taifa unakarabatiwa kwa bilion 30 katika taifa ambalo hatuna madawati, tumeona fedha za maendeleo zinavyopigwa lakini haya yote hayafanywi na Mhe. Rais yanafanywa na wasaidizi wake. Kuondoka hapa lazima avae nafsi ya JPM katika upitishaji wa miradi mikubwa.

Wapi aboreshe
Kwanza, akubali kuteua watu kwa vigezo vya ufanisi siyo kigezo cha historia ya familia.

Pili, aamue sasa kumpa kazi Makamu wa Rais na Waziri Mkuu waungane naye angalau kila Mwezi kusoma na kujadili maamuzi makubwa ya miradi yanayopita mbele ya utawala wake.

Naamini mzee Mpango anasoma sana, makatibu wakuu wakigundua kwamba Mhe. Rais, Makamu na Waziri Mkuu wanakaa kupitia jambo lolote nyeti na wakibaini upo uzembe watawatumbua basi makatibu wakuu watafanya kazi yao na definatly hata watendaji ngazi nyingine watawajibika.

Tatu, aamue sasa kufanya kazi na jamii, jamii ikilia anyooshe sikio kupitia chanzo cha kilio. Mfano jamii inapolia kuhusu wizara ya michezo kutumia bilioni 30 awahoji na kuleta ufafanuzi kupunguza fikra za upigaji.

Nne, afute kauli zilizotolewa na zinazotolewa na wasaidizi wake hasa wakisiasa ikiwemo wabunge kwamba Watanzania hawawezi kufanya hiki wala kile. Hizi kauli zinawaondolea watanzania sovereignty na kukabidhi uhuru wao kwa wageni.

Ni kauli za kutengeneza jamii ya kitumwa. Atoke adharani na kuwapa moyo Watanzania kwamba wanaweza na awape kipaombele. Akiweza kukemea huu udhalilishaji ataweza pia kuwaona watanzania waliobobea wanaoweza kuchukua nafasi za wanaotuaminisha kwamba hatuwezi.

Tano; abadili mfumo wa upandishwaji vyeo huko kwenye utumishi wa umma. Aamue sasa kuacha kusogeza watendaji kutoka ngazi moja kwenda nyingine. Moja ya factor iliyoua Taifa letu ni watumishi wa umma kujengewa fikra kwamba hata wasipofanya kazi kwa ufanisi watapandishwa vyeo. Atoke adharani avuruge utumishi wa umma kwa kuchukua watu regardless of rank kuwapeleka juu endapo wamezaliwa na brain.

Mwalimu Nyerere aliweza, kwenye siasa tumeweza sasa twende kwenye utumishi wa umma. Watumishi wa umma wakiona wanaofanya vyema wabavushwa vyeo ushindani utakuwepo na ufanisi utaonekana. As long as watu wanataka ukubwa waonyeshe kwamba wakifanya kazi vyema watakuwa wakubwa naamini mtaona ushindani wa utoaji huduma ukiongezeka ikiwemo ubunifu.

Mwisho nikutakie kila la kheri Mhe. Rais Samia katika kuyaishi mema na kuimarika palipo na madhaifu.
 
Exposure na experience ya kuongoza NGO hazijatosha kabisa yeye kuongoza hili shirika kubwa lenye wafanyakazi 60+m
 
Kiujumla kwangu mimi mama viatu vya urais havimtoshi baadala ya kuongoza inaonekana kabisa anaongozwa, angekuwa anajitambua baadhi ya mawiziri kama january wangekuwa walishafukuzwa, hii inchi anayeiongoza ni kikweta na familia yake,
Inaonekana wao ndiyo wanufaika wakubwa wa kifo cha mwendazake, lakini ipo siku yatakuja julikana yote
 
tutolee ujinga. mama yupo vizuri mnoo
 
tutolee ujinga. mama yupo vizuri mnoo
Labda kwa machawa kama wewe, yaani utamfananisha huyo mama na magufuli? Hivi unaakili kweli wewe? Huoni tu waliochini yake wanavyoiba sababu wanajua hana uwezo wa kuwafanya chochote?

Kama hujui inawezekana mama kuna baadhi ya mawaziri hata wangeharibu vipi hana uwezo wa kuwafanya chochote, sababu wao ndiye waliyemuweka hapo alipo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom