Mhe. Rais Kikwete na ziara ya Mabwepande

Mhe. Rais Kikwete na ziara ya Mabwepande

Napenda kuwajulisha kuwa kichwa cha habari original kilikuwa:

JJ MNYIKA ANAVYOJICHEKESHA KWA JK
Wamebadilisha title? hahahaaaa... siwa maindi kabisa CCM lakini tuseme ukweli hili forum ni CHADEMA mwanzo mwisho!

Truth be told, Mnyika kajichekesha kupita kiasi kukutana na Rais.
 
Kitu gani hapa kipya cha kushangaa.

Tatizo Watanzania wengi kwenye siasa wanakuwa kama ng'ombe wanaopelekwa kunywa maji.

Kama watanzania hawazezi kujitambua na wakatambua nafasi yao katika jamii wataendelea kushangaa wanapokumbana na picha kama hizi.

Kwa mawazo kama haya, haishangazi kuona kuna kesi mahakamani za kutaka kudhuru au kuua kwa sababu ya mlengo tofauti wa kisiasa.

kila mtu anataka watu wawe kama yeye, hata vyama navyo vinataka kila mtu awe kama wao. Kukataa kuwa kama wao ni kuhatarisha maisha yako.

Kwa Tanzania, different opinions inaitwa mawazo mgando. This is Tanzania.
 
siasa sio uadui wa vita,ila kwa wana ccm wenye akili ndogo kama wewe unadhani ni vita kama mnavyobambikia watu kesi na kuua!
Aise nimeamin cdm ni zaid ya uijuavyo! Juzi tu mh.ZITTO kapiga picha na mheshimiwa ilipoletwa hapa jamvin weng wenu mlisema msaliti huyooo!! Leo hii kwa Mnyika alowatamkia watanzania kuwa JK dhaif anapiga picha akiwa na huyo dhaif mnasema siasa si UADUI?
 
Siasa sio vita su
uadui.Kuwa vyama tofauti haimaanishi mnuniane au msisalimiane.Huo sio
ukomavu wa siasa ni utoto.Sisi sote ni watanzania uzalendo
kwanza

Ni kweli kabisa,hasa linapotokea swala la maendeleo kwa wananchi,hilo daraja lililozinduliwa na Mh.Rais watapita watu wote bila kujali itikadi za vyama vyao.
 
Mwanzo ooooh hatumtambui...leo ohhh karibu mheshimiwa utufungulie mradi

hawa watu hawajaingia serikalini hawaishi kufanya U Turn, wakiingia je?

Akili yako fupi kama G string
 
Sina unafiki nimepinga sababu nina ushahidi wa Mnyika kushabikia mambo ya ovyo kuhusu kukutana kwa JK na ZZK tuache fitna na tuwe wakweli kwa nafsi zetu.

Tupe ushahidi wa ulicho kiandika
 
Hawa wote wakifika kwa JK hawana lolote, mnakumbuka Lissu alivyokenua meno walivyoenda Ikulu?
 
HOJA ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) kuhusiana na suala la tatizo la upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Dar es Salaam, inaelekea kupata ufumbuzi kutokana na Rais Jakaya Kikwete kumuita Ikulu mbunge huyo Jumatatu wiki ijayo.

Wengine walioitwa kukutana na rais ni Mkuu wa Mkoa, Mecky Sadick, wakuu wote wa wilaya pamoja na wabunge na wataalamu kutoka Wizara ya Maji.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa daraja la Mtaa wa Golani, Kata ya Saranga, Rais Kikwete alisema kuwa kutokana na wananchi wa kata hiyo kupiga kelele kuhusiana na suala la maji ameamua kukutana na viongozi hao ili kupatiwa ufumbuzi.

Kikwete pia alitaka kuwepo na mfumo maalumu wa mabomba ya maji yatakayojengwa kwa saruji kutoka Ruvu Chini na kuja jijini Dar es Salaam moja kwa moja bila kuchepuliwa sehemu yeyote.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alikiri kuwepo kwa wizi wa maji katika maeneo ambayo mabomba ya maji yamepita.

“Watu wasifanye ukanjanja katika masuala ya maji, mabomba yanatandazwa na watu wanaiba maji, shida inayotokea ni maji hayo kutokufika jijini Dar es Salaam,” alisema.

Alifafanua kuwa lita milioni 65 zinahitajika ili kukabiliana na tatizo la maji na kwamba upanuzi wa Ruvu Juu na Chini ujenzi wake utakamilika Julai na kutaka hatua za haraka kuchukuliwa kuhakikisha maji yanapatikana kwa haraka ili kumaliza tatizo.

Hatua ya Mnyika kuitwa Ikulu imetokana na kusimama kidete katika suala la maji ambapo Aprili 4, mwaka huu aliwasilisha hoja binafsi na kuitaka serikali kuchukua hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es Salaam hoja ambayo ili iliondolewa bungeni kibabe.

Wakati huo huo, Rais Kikwete amemaliza kilio cha muda mrefu kwa wakazi 604 wa mji mpya Mabwepande Manispaa ya Kinondoni kwa kumpa kila mmoja mifuko 100 ya saruji itakayogharimu sh milioni 840.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Home Shopping Center (HSC), Ghalib Mohamed, aliahidi kutoa mabati 30 kwa kila mkazi ili waondokane na kuishi kwenye mahema yaliyotoboka.

Rais alikuwa katika mwendelezo wa ziara yeka mkoani hapa kukagua shughuli za maendeleo ambapo pia alifungua shule ya msingi, kituo cha polisi, nyumba za walimu na polisi vilivyojengwa kwa ushirikiano wa Kampuni za HSC na TSN katika mji.

Wakazi hao ni wale ambao nyumba na mali zao zilizolewa na mafuriko mwaka 2011.

Rais alisema serikali imeamua kufanya hivyo baada ya kutembelea mahema ambayo wanaishi kwa sasa na kubaini kuwa yametoboka na kwamba wakati wa mvua wamekuwa wakiishi kwa taabu.

Alisema fedha hizo leo zitakuwa zimefika kwa mkuu wa mkoa ili waweze kununuliwa saruji hiyo ambapo pia wakazi 21 kati yao walikabidhiwa hati za makazi na rais huku akiagiza hati nyingine ziweze kukamilika haraka iwezekanavyo.

Naye Mkurugenzi wa HSC, alisema kupitia sera ya kampuni yao watatumia sehemu ya faida kuwasaidia wananchi mbalimbali waliokumbwa na matatizo kwani ni vema kugawana na wasio nacho.
 
Kwani aliposema Tatizo la Maji Dar litakuwa historia alikuwa Hana mpango wowote? Kweli Rais tunaye!!!!
 
Siasa bwana tamu kusoma tu ili mtu ujifurahishe lakini utekelezaji wake, pumba nyingi, uwongo usio na sababu, wasema ukweli kumwagiwa tindi kali, mwisho wa siku nothing happens tunarudi pale pale mwaka 1947 kwa kutembea kilomita 200 kuchota ndoo moja tu ya maji huku viongozi wakitusanifu kwa kutupa visingizio vya hajabu.
 
Kafungua kituo cha polisi huko mabwepande wafanye mazoezi maalum mle..
 
tena kwa kuonyoshea kuwa hayuko pamoja na wenzake kaamua kuvaa sare kama alivyovaa bosi.



Ksbb unafikiri kwa kutumia MACHO ndio maana UNATOA MAELEZO TU BILA KUFIKIRI KUTUMIA UBONGO.....!!!

.... Ukitumia MACHO kufikiri that is shuleless behaviour.....!!
 
Back
Top Bottom