kajima
JF-Expert Member
- Dec 5, 2009
- 1,289
- 514
- Thread starter
- #141
wakati mwingine natamani nisiitwe Mtanzania kutokana na fikra za baadhi ya wananchi wenzangu. Muda wote tunawaza uhasama, vita, kupandikiziana vitu, visasi. Hivi hatupigi hatua nawambieni. Utakuta hata bungeni mtu anatoa hoja nzuri kwavile ni upinzani watu wazima unaodhani wana heshima zao watazomea, watapiga meza ni karaha tu. Mnyika ulitaka afanye nini hapo? Rais kaja jimboni kwake watu wake wanapata huduma kwa hela ya kodi zetu wote unataka avimbe ili iwe nini? Tubadilike bwana yaani hapa kwetu upinzani utadhani ni uhaini. watu badala ya kufanya shughuli za maendeleo kutwa kucha wanahangaika kudhibitiana. hatufiki popote namna hii.
Pole mtazamo hasi, Mimi nimekua katika jiji la dar es salaam mpaka kumaliza chuo kikuu, tatizo la maji nimekua nalo, muda mrefu Serikali ya chama tawala limefumbia macho suala hili, sasa Ndugu Mnyika amechangia kwa namna moja au nyingine kupata sikio la mkuu wa kaya....hili ni jambo jema kwa wananchi, hii ndiyo sababu ya kuleta mada so Bravo Ndugu Mnyika na hongera kwa Mhe. Raisi