Quarterpin
JF-Expert Member
- Mar 19, 2013
- 1,253
- 1,084
Huyu ni kiongozi wa nchi na zaidi ya yote ni mzee hivyo ni kama mzazi huwezi kuleta dharau za kifala,ukileta ujinga wajanja wanang'oa jicho.
Huyu si ndiye alisema jk ni dhaifu?
Huyu si ndiye alisema jk ni dhaifu?
Well said mkuu.Elewa kuwa kazi mojawapo ya upinzani ni kuikosoa serikali, kuielekeza, kutoa maoni na kutoa njia mbadala kwa masuala muhimu. Upinzani sio uadui kama wengine wanavyochukulia. Kuna mambo mengi ambayo upinzani umepigania na kutoa maoni na serikali imeyatekeleza. Lengo ni moja, kuleta maendeleo kwa Watanzania, tatizo ni njia gani itumike kuharakisha lengo hili. kwa bahati mbaya sana nchi yetu haina sera za Kitaifa ambapo kila chama cha siasa kinatakiwa kieleze ni kwa namna gani itatekeleza na wananchi wakiikubali njia hiyo basi watakichagua chama husika. Hali ilivyo hivi sasa ni kubeza, matusi, kejeli na chuki ambavyo mwananchi wa kawaida haimsaidii.
Kwa kumalizia Mhe. Mnyika hana sababu ya kumchukia Rais Kikwete, na akiwa karibu nae basi labda atafanikiwa kwa urahisi sana kutimiza ahadi zake kwa wananchi waliomchagua wala sio kusaliti chama chake. Na hivyo ndivyo inavyoelekea hasa kuhusiana na swala la maji. Si lazima kusubiri mpaka chama chake kiingie madarakani.
Wako wabunge ambao badala ya kupigania maendeleo ya wananchi waliowachagua wanapoteza muda kwa maandamano yasiyo na tija. Kwa mfano kwa nini kung"ang"ania kufanya maandamano kuhusu kushuka kwa Elimu badala ya kukaa na wananchi waliowachagua kupanga mikakati ya kuimarisha elimu katika maeneo yao? Sababu za kushuka elimu ni nyingi, na nyingine ziko ndani ya uwezo wa wapigakura waliowachagua kama vile kuondoa utoro, mimba na ndoa za utotoni kwa hayo kuna haja ya kufanya maandamano? Ni bora kutoa maoni kwa vyombo husika au kamati iliyoteuliwa kuliko kupoteza nguvu kazi kwa kufanya maandamano. Wako watu wachache wanaofikiri kushirikiana na chama tawala ni usaliti. Tuondoe fikra hizi.