Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,675
- 40,555
Kwa mara nyingine tunashuhudia nchi yetu ikionyeshwa mchezo mwingine wa mazingaombwe! mchezo wa viini macho. Kitendo cha Rais Kikwete na kampuni kubwa ya madini ya Barrick kupitia tena mkataba ni udhihirishaji wa wazi kuwa mkataba ule wa mwanzo haukuingiwa kukiwa na imani (good faith) kati yao. Kuna mikataba mingine mingi tu ya madini, nishati, umiliki, ugavi n.k ambayo bado inazua maswali mengi.
Hata hivyo, mikataba hiyo haikuingizwa na majini au mapepo!! Walioiingiza serikali kwenye mikataba hiyo ni watanzania wenzetu walio katika nafasi mbalimbali kwenye wizara, idara, na vyombo mbalimbali vya serikali. Watu hawa kwa namna fulani wamenufaika kwa kumegewa sehemu kidogo ya makato wakati wa majadiliano ili mkataba wa aina fulani upite (rejea kesi ya IPTL). Bila ya shaka, tukiwachunguza maafisa wote walioshiriki katika mikataba hii na kulinganisha mali walizonazo (kwa majina yao au ya watoto wao) na kulinganisha vitu hivyo na mapato yao tutaona kuna tofauti kubwa!! Watu hao waitwe kujieleza walivipata vitu hivyo vipi, na ikibidi wapewe kinga ya kutokushitakiwa (siyo kutokutaifishiwa) endapo wataeleza bayana makato na mfuko waliopata toka makampuni makubwa yenye kutaka kuingia mikataba.
Haitoshi kusahihisha mikataba tu wakati walioiingiza serikali kwenye mikataba hiyo bado wana nafasi hizo hizo na bado wanashiriki katika majadiliano ya mikataba mingine. Ninapendekeza yafuatayo:
a. Serikali iweke bayana matakwa yote ya wale wanaoiwakilisha serikali kwenye majadiliano ya mikataba. Kama vile, hawaruhusiwi kupokea pesa, zawadi, au asante yoyote toka kwa kampuni hiyo kwa jina lao au la jirani yao.
b. Mikataba yote inayoingiwa na serikali ina haki ya kupitiwa na Bunge la Tanzania na inaweza kuhojiwa na kamati husika ya Bunge.
c. Endapo mkataba wowote unagundulika kuingiwa kwa kufoji au nje ya kuaminiana (not in good faith) mkataba huo wote (siyo vipengele tu) unakuwa umetanguka na hauna nguvu (null and void)
d. Wale wote ambao wanagundulika kuiingiza serikali kwenye mikataba mibovu huku wao wenyewe wakinufaika, wakamatwe mara moja, washitakiwe kwa sheria ya kuhujumu uchumi ya mwaka 1984??? na wafilisiwe endapo hawako tayari kurudisha mali zote walizojipatia kwa kutumia nafasi zao!
e. Mikataba yote iliyohusisha watu hao na madalali wao lazima ipitiwe upya (yote au vipengele) na endapo kuna kitu cha kusahihishwa, basi kitu hicho kianzie tangu nyuma (retroactive).
Haya yakifanyika basi naweza kuanza kuamini Mhe. Kikwete labda yuko serious.. otherwise.. yote ni mazingaombwe!! Je Mhe. Rais utathubutu kumfunga paka kengele??