Uko sawa kabisa mkuu. Nafikiri wangeruhusiwa kuoa rate ya udhalilishaji wa vijana (watoto wadogo wa kiume) huenda ingekuwa ndogo. Mapadri wengi tu leo wana watoto wengi tuuu mitaani kitu kinachoonyesha unafiki wa hali ya juu kuhusu suala hili. Jamaa hawawezi kukaa hivyo hivyo bila tendo la ndoa kwa sababu wana maisha maisha mazuri ya duniani yakiambata na kula vizuri na hivyo kuufanya mwili uwe kwenye uhitaji mzuri wa kufanya tendo la ndoa. Si mpango wa MUNGU tangu mwanzo mwanaume aishi maisha yake yote bila kuoa. Mbaya zaidi huingilia sana hata ndoa za washirika wao kama vile marehemu askofu Butibubage wa Mwanza alivyovunja ndoa ya Pius Msekwa baada ya kuzaa naye mtoto (watoto). Mhhh! Mbaya kabisa hii. Mapokeo mabaya kabisa haya jamani.
Binafsi siwezi kusema ndoa ndiyo inayoondoa udhalilishaji au kukosa uaminifu katika maisha ya mtu. Ni uamuzi wa mtu mwenyewe kuwa mwaminifu au kutokuwa mwaminifu.
Mbona baadhi ya waliooa wana nyumba ndogo, wanafanya mapenzi hata wanawalawiti watoto wao wa kuzaa au kuwapa mimba wanafunzi? Kitu tusichokielewa kwenye Kanisa ni maisha ya kujitoa sadaka na mara nyingi tunayatafsiri kulingana na tunavyoona sisi wenyewe. Maisha ya useja yalikuwepo hata kabla ya Yesu. Kwani wakati huo Mungu hakuwepo? Kuna njia nyingi za kumtafuta/kumtumikia Mungu.
Ni kweli ndoa imewekwa na Mungu hasa kwa nia ya 'companionship' na 'reproduction'lakini siyo amri kuwa mtu lazima aoe. Maana hata katika kuoa kuna suala la 'choice'. Unaweza ukapenda kuoa na usimpate mwenza anayependezwa na wewe au tabia yako au unaweza kumpenda mwanamke na yeye asikupende.
Kwa hiyo, kama mtu fulani kwa imani yake anaamua kutooa ni uamuzi wake na mwingine akiamua kuoa ni uamuzi wake pia.
Kwani hujui wanandoa ambao wana watoto nje licha ya kwamba wameoa? Na wengine mambo yanajulikana baada ya mume kuaga dunia ndipo mke wa nyumba ndogo anapojitokeza kudai sehemu ya urithi. Kukosa uaminifu ni tatizo letu wote na siyo mapadre tu. Juzijuzi hapa magazeti yaliripoti kuwa mchungaji (ambaye ana mke) alifumaniwa na mke wa mtu. Hata wakati mwingine tunasikia shehe au imamu (ambao wana wake zaidi ya mmoja) kalawiti au kafumaniwa. Je, ni kwa sababu gani?