Mhashamu Methodius Kilaini ahamishiwa Jimbo la Bukoba

Makala

Kikwete amponza Askofu Kilaini

lC.gif
Mwandishi Wetu​
Disemba 9, 2009
rC.jpg

bul2.gif
Kauli ya "Kikwete chaguo la Mungu" bado yamuandama

bul2.gif
Ukabila, umaarufu navyo vyazungumzwa

UHAMISHO wa aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methodius Kilaini, kwenda kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, umehusishwa na mambo mengi ikiwamo siasa za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na sintofahamu kati yake na wenzake ndani ya kanisa hilo, imefahamika.

Habari za ndani ya Kanisa Katoliki, zimethibitisha kuyumba kwa mahusiano kati ya Askofu Kilaini na wenzake ndani ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam kutokana na sababu za kimfumo na kuchochewa zaidi na mahusiano binafsi ya viongozi wakuu ndani ya Kanisa hilo lenye nguvu na wafuasi wengi nchini.

Askofu Kilaini amekuwa kiongozi anayesikika zaidi kutoa matamko kwa niaba ya Kanisa Katoliki nchini, na inaelezwa kuwa hii ni moja ya sababu zilizomuondoa ikidaiwa kwamba baadhi ya matamko aliyotoa hayakuwa na baraka za viongozi wenzake na hiyo imekuwa ikiwakera wenzake ndani ya mfumo wa kanisa hilo.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu Msaidizi kumsaidia Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Kilaini alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), nafasi ambayo ilikuwa ikimpa fursa ya kuwa msemaji wa Baraza la Maaskofu, na kwamba "aliizoea nafasi hiyo hata baada ya kuondoka".

Ukiacha mambo hayo ya ndani, taarifa zinasema Askofu Kilaini atakuwa pia ameponzwa na kauli yake aliyotoa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Akizungumzia matokeo ya uchaguzi huo, baada Jakaya Kikwete kupita kwa kura nyingi, Kilaini alikaririwa akisema Rais Jakaya Kikwete, alikuwa ni "chaguo la Mungu" kwa Watanzania. Kauli hiyo iliwakera baadhi ya viongozi na waumini walioanza kuona kuwa Kanisa linakuwa karibu kabisa na uongozi wa kisiasa.

Hata hivyo, Askofu Kilaini ambaye katika siku za karibuni naye amekuwa haisemi vizuri Serikali ya Kikwete, akijitetea kuhusu kauli yake ile, alisema maandiko yanaainisha kwamba kiongozi yeyote anayechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi walio wengi anakuwa ni "chaguo la Mungu".

Pamoja na utetezi huo wa Kilaini, bado amekuwa akisakamwa kwa kauli yake hiyo ambayo ilihusishwa pia na safari yake ya matibabu India, Septemba 2007, ambayo inaelezwa ya kuwa ilifadhiliwa na Rais Kikwete binafsi. Kauli na safari hii vimekuwa kayi ya vyanzo vya ufa kati yake na viongozi wenzake wa Kanisa, wakimwona kuwa amekwenda kinyume cha mambo kwa kuwa, kwa mfano, Kanisa lisingeshindwa kumlipia matibabu nje, ama hata kama ingebidi, basi angefadhiliwa na Serikali badala ya Rais Kikwete binafsi.

Askofu Kilaini hakuweza kupatikana wiki hii kuzungumzia kuhamishwa kwake, lakini watu wanaomfahamu wamethibitisha kuyumba kwa mahusiano yake na wenzake kutokana na sababu kadhaa, zikiwamo za kiutendaji na sababu nyingine binafsi.

Sababu za kiutendaji zinazotajwa kumponza Askofu Kilaini ni pamoja na wasiwasi wa viongozi wenzake kwamba anaweza "kutumiwa na wanasiasa" katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2010 kutokana na mahusiano yake ya karibu na wanasiasa wengi pamoja na kuwa karibu na vyombo vya habari.

Imeelezwa kwamba sababu binafsi zilizoyumbisha mahusiano yake na wenzake ni pamoja na madai ya kuwapo ukabila katika maamuzi yake mengi ikiwamo kuwaingiza watu kutoka mkoani Kagera katika nafasi nyingi za Kanisa ya Dar es Salaam na watendaji katika asasi kadhaa japo watu wanaomfahamu kwa karibu wameeleza ya kuwa madai hayo yametokana na chuki binafsi walizonazo baadhi ya wenzake.

Ndani ya Kanisa Katoliki kumekuwapo na maswali mengi yanayoulizwa baada ya kutangazwa kwa uhamisho wa Askofu Kilaini ikiwa ni pamoja na wanaohoji kama atateuliwa Askofu Msaidizi mwingine badala yake kumsaidia Pengo.

"Kawaida Askofu Msaidizi anaombwa. Ina maana Pengo, aliomba kuwa na Askofu Msaidizi. Je, sasa ameona hana haja tena kuwa na Askofu Msaidizi? Je, Askofu wa Bukoba ameomba kuwa na askofu Msaidizi? Maana ni lazima aombe!" Alihoji msomaji mmoja wa Raia Mwema lakini ambayo ni miongoni mwa waumini wa Kanisa Katoliki nchini na anayemfahamu vyema Askofu Kilaini.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana Askofu Msaidizi hawezi kuhamishwa kwenda kwingine kama si kupanda daraja na hivyo kwamba kwa kuwa Kilaini alikuwa Askofu Msaidizi Dar es Salaam kuhamishwa kwake kwenda kuwa Askofu Msaidizi wa Bukoba ambako si Jimbo Kuu kama Dar es Salaam ni jambo jipya katika mfumo wa Kanisa Katoliki.

"Hili ni jambo jipya. Maana baada ya kuwa Askofu Msaidizi kwa miaka 10 ilitarajiwa awe Askofu Kamili au awe Askofu Msaidizi Mrithi. Kwa vile ni Askofu Msaidizi, hata akifa Askofu wa Bukoba, si lazima Kilaini awe Askofu wa Jimbo la Bukoba, maana yeye si Askofu Msaidizi Mrithi," anasema muumini huyo.

Lakini baadhi ya watu wa ndani ya Kanisa Katoliki wamekuwa wakiamini kwamba uhamisho huo una nia njema na unalenga kumpandisha ngazi Askofu Kilaini ama pia kumsogeza karibu na nyumbani kwake apate kupumzika kutokana na kuyumba kwa afya yake.

Hoja nyingine inayojadiliwa ni kwamba Askofu Kilaini anaweza kuwa anaandaliwa kuwa Askofu Mkuu wa Mwanza, na kwamba kwenda kwake Kanda ya Ziwa kunamsogeza zaidi karibu na nafasi hiyo kwa kuwa kwa kawaida nafasi ya kwanza ya uteuzi wa Askofu wa Mwanza itatolewa kwa ya mtu mwenye sifa aliyeko Kanda ya Ziwa.
Taarifa ya Kanisa Katoliki iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padre Anthony Makunde ilieleza kwamba Baba Mtakatifu, Benedicto wa 16, amemhamisha Askofu Kilaini, kwenda kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Askofu Kilaini, ambaye amekuwa akimsaidia Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa miaka mingi, ameruhusiwa kuendelea kushika Kiti cha Jimbo la Strumnizza.

Aliteuliwa kushika nafasi ya Askofu Msaidizi Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Baba Mtakatifu, Yohane Paulo wa Pili.

Kilaini amekuwa mmoja wa viongozi wa dini anayesikika sana katika vyombo vya habari na alikuwa mmoja wa wachangiaji wakubwa waliozungumza katika kongamano la Mwalimu Julius Nyerere, lililofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni akiifananisha nchi ilivyo na mtu anayetembea bila nguo.

Miongoni mwa vichwa vya habari vilivyotikisa vikimnukuu
Askofu Kilaini ni pamoja na:

"Askofu Kilaini atoa angalizo uchaguzi mkuu ujao; Askofu Kilaini: 2009 punguzeni pombe; Mafisadi EPA warejeshe riba pia - Askofu Kilaini; Askofu Kilaini, si ufisadi tu, yako mengi; Askofu Kilaini: Kikwete ameelemewa na mafisadi; Askofu Kilaini: Kingunge anajadili hewa."

Kanisa Katoliki limeandaa na kusambaza nyaraka zake maalumu kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa 2010, Askofu Kilaini akiwa mmoja wa washiriki wakuu katika maandalizi na uhamasishaji wa yaliyomo ndani ya nyaraka hizo zilizowakera wanasiasa wengi na kuibua mjadala mkubwa katika jamii.

Source:Raia Mwema

hs3.gif
 
  • Kauli ya "Kikwete chaguo la Mungu" bado yamuandama
  • Ukabila, umaarufu navyo vyazungumzwa

UHAMISHO wa aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methodius Kilaini, kwenda kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, umehusishwa na mambo mengi ikiwamo siasa za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na sintofahamu kati yake na wenzake ndani ya kanisa hilo, imefahamika.

Habari za ndani ya Kanisa Katoliki, zimethibitisha kuyumba kwa mahusiano kati ya Askofu Kilaini na wenzake ndani ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam kutokana na sababu za kimfumo na kuchochewa zaidi na mahusiano binafsi ya viongozi wakuu ndani ya Kanisa hilo lenye nguvu na wafuasi wengi nchini.

Askofu Kilaini amekuwa kiongozi anayesikika zaidi kutoa matamko kwa niaba ya Kanisa Katoliki nchini, na inaelezwa kuwa hii ni moja ya sababu zilizomuondoa ikidaiwa kwamba baadhi ya matamko aliyotoa hayakuwa na baraka za viongozi wenzake na hiyo imekuwa ikiwakera wenzake ndani ya mfumo wa kanisa hilo.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu Msaidizi kumsaidia Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Kilaini alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), nafasi ambayo ilikuwa ikimpa fursa ya kuwa msemaji wa Baraza la Maaskofu, na kwamba “aliizoea nafasi hiyo hata baada ya kuondoka”

Ukiacha mambo hayo ya ndani, taarifa zinasema Askofu Kilaini atakuwa pia ameponzwa na kauli yake aliyotoa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Akizungumzia matokeo ya uchaguzi huo, baada Jakaya Kikwete kupita kwa kura nyingi, Kilaini alikaririwa akisema Rais Jakaya Kikwete, alikuwa ni “chaguo la Mungu” kwa Watanzania. Kauli hiyo iliwakera baadhi ya viongozi na waumini walioanza kuona kuwa Kanisa linakuwa karibu kabisa na uongozi wa kisiasa.

Hata hivyo, Askofu Kilaini ambaye katika siku za karibuni naye amekuwa haisemi vizuri Serikali ya Kikwete, akijitetea kuhusu kauli yake ile, alisema maandiko yanaainisha kwamba kiongozi yeyote anayechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi walio wengi anakuwa ni “chaguo la Mungu”.

Pamoja na utetezi huo wa Kilaini, bado amekuwa akisakamwa kwa kauli yake hiyo ambayo ilihusishwa pia na safari yake ya matibabu India, Septemba 2007, ambayo inaelezwa ya kuwa ilifadhiliwa na Rais Kikwete binafsi. Kauli na safari hii vimekuwa kayi ya vyanzo vya ufa kati yake na viongozi wenzake wa Kanisa, wakimwona kuwa amekwenda kinyume cha mambo kwa kuwa, kwa mfano, Kanisa lisingeshindwa kumlipia matibabu nje, ama hata kama ingebidi, basi angefadhiliwa na Serikali badala ya Rais Kikwete binafsi.

Akofu Kilaini hakuweza kupatikana wiki hii kuzungumzia kuhamishwa kwake, lakini watu wanaomfahamu wamethibitisha kuyumba kwa mahusiano yake na wenzake kutokana na sababu kadhaa, zikiwamo za kiutendaji na sababu nyingine binafsi.

Sababu za kiutendaji zinazotajwa kumponza Askofu Kilaini ni pamoja na wasiwasi wa viongozi wenzake kwamba anaweza “kutumiwa na wanasiasa” katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2010 kutokana na mahusiano yake ya karibu na wanasiasa wengi pamoja na kuwa karibu na vyombo vya habari.

Imeelezwa kwamba sababu binafsi zilizoyumbisha mahusiano yake na wenzake ni pamoja na madai ya kuwapo ukabila katika maamuzi yake mengi ikiwamo kuwaingiza watu kutoka mkoani Kagera katika nafasi nyingi za Kanisa ya Dar es Salaam na watendaji katika asasi kadhaa japo watu wanaomfahamu kwa karibu wameeleza ya kuwa madai hayo yametokana na chuki binafsi walizonazo baadhi ya wenzake.
Ndani ya Kanisa Katoliki kumekuwapo na maswali mengi yanayoulizwa baada ya kutangazwa kwa uhamisho wa Askofu Kilaini ikiwa ni pamoja na wanaohoji kama atateuliwa Askofu Msaidizi mwingine badala yake kumsaidia Pengo.

“Kawaida Askofu Msaidizi anaombwa. Ina maana Pengo, aliomba kuwa na Askofu Msaidizi. Je, sasa ameona hana haja tena kuwa na Askofu Msaidizi? Je, Askofu wa Bukoba ameomba kuwa na askofu Msaidizi? Maana ni lazima aombe!” Alihoji msomaji mmoja wa Raia Mwema lakini ambayo ni miongoni mwa waumini wa Kanisa Katoliki nchini na anayemfahamu vyema Askofu Kilaini.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana Askofu Msaidizi hawezi kuhamishwa kwenda kwingine kama si kupanda daraja na hivyo kwamba kwa kuwa Kilaini alikuwa Askofu Msaidizi Dar es Salaam kuhamishwa kwake kwenda kuwa Askofu Msaidizi wa Bukoba ambako si Jimbo Kuu kama Dar es Salaam ni jambo jipya katika mfumo wa Kanisa Katoliki.
“Hili ni jambo jipya. Maana baada ya kuwa Askofu Msaidizi kwa miaka 10 ilitarajiwa awe Askofu Kamili au awe Askofu Msaidizi Mrithi. Kwa vile ni Askofu Msaidizi, hata akifa Askofu wa Bukoba, si lazima Kilaini awe Askofu wa Jimbo la Bukoba, maana yeye si Askofu Msaidizi Mrithi,” anasema muumini huyo.
Lakini baadhi ya watu wa ndani ya Kanisa Katoliki wamekuwa wakiamini kwamba uhamisho huo una nia njema na unalenga kumpandisha ngazi Askofu Kilaini ama pia kumsogeza karibu na nyumbani kwake apate kupumzika kutokana na kuyumba kwa afya yake.
Hoja nyingine inayojadiliwa ni kwamba Askofu Kilaini anaweza kuwa anaandaliwa kuwa Askofu Mkuu wa Mwanza, na kwamba kwenda kwake Kanda ya Ziwa kunamsogeza zaidi karibu na nafasi hiyo kwa kuwa kwa kawaida nafasi ya kwanza ya uteuzi wa Askofu wa Mwanza itatolewa kwa ya mtu mwenye sifa aliyeko Kanda ya Ziwa. Taarifa ya Kanisa Katoliki iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padre Anthony Makunde ilieleza kwamba Baba Mtakatifu, Benedicto wa 16, amemhamisha Askofu Kilaini, kwenda kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Askofu Kilaini, ambaye amekuwa akimsaidia Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa miaka mingi, ameruhusiwa kuendelea kushika Kiti cha Jimbo la Strumnizza.
Aliteuliwa kushika nafasi ya Askofu Msaidizi Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Baba Mtakatifu, Yohane Paulo wa Pili.

Kilaini amekuwa mmoja wa viongozi wa dini anayesikika sana katika vyombo vya habari na alikuwa mmoja wa wachangiaji wakubwa waliozungumza katika kongamano la Mwalimu Julius Nyerere, lililofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni akiifananisha nchi ilivyo na mtu anayetembea bila nguo.
Miongoni mwa vichwa vya habari vilivyotikisa vikimnukuu Askofu Kilaini ni pamoja na:
“Askofu Kilaini atoa angalizo uchaguzi mkuu ujao; Askofu Kilaini: 2009 punguzeni pombe; Mafisadi EPA warejeshe riba pia - Askofu Kilaini; Askofu Kilaini, si ufisadi tu, yako mengi; Askofu Kilaini: Kikwete ameelemewa na mafisadi; Askofu Kilaini: Kingunge anajadili hewa.” Kanisa Katoliki limeandaa na kusambaza nyaraka zake maalumu kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa 2010, Askofu Kilaini akiwa mmoja wa washiriki wakuu katika maandalizi na uhamasishaji wa yaliyomo ndani ya nyaraka hizo zilizowakera wanasiasa wengi na kuibua mjadala mkubwa katika jamii.
Source: Raia Mwema
My take: ni rahisi wakristo kuabudu mtu
 
Kikwete amponza Askofu Kilaini

Mwandishi Wetu

Raia Mwema
Disemba 9, 2009

bul2.gif
Kauli ya "Kikwete chaguo la Mungu" bado yamuandama

bul2.gif
Ukabila, umaarufu navyo vyazungumzwa

UHAMISHO wa aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methodius Kilaini, kwenda kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, umehusishwa na mambo mengi ikiwamo siasa za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na sintofahamu kati yake na wenzake ndani ya kanisa hilo, imefahamika.

Habari za ndani ya Kanisa Katoliki, zimethibitisha kuyumba kwa mahusiano kati ya Askofu Kilaini na wenzake ndani ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam kutokana na sababu za kimfumo na kuchochewa zaidi na mahusiano binafsi ya viongozi wakuu ndani ya Kanisa hilo lenye nguvu na wafuasi wengi nchini.

Askofu Kilaini amekuwa kiongozi anayesikika zaidi kutoa matamko kwa niaba ya Kanisa Katoliki nchini, na inaelezwa kuwa hii ni moja ya sababu zilizomuondoa ikidaiwa kwamba baadhi ya matamko aliyotoa hayakuwa na baraka za viongozi wenzake na hiyo imekuwa ikiwakera wenzake ndani ya mfumo wa kanisa hilo.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu Msaidizi kumsaidia Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Kilaini alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), nafasi ambayo ilikuwa ikimpa fursa ya kuwa msemaji wa Baraza la Maaskofu, na kwamba "aliizoea nafasi hiyo hata baada ya kuondoka".

Ukiacha mambo hayo ya ndani, taarifa zinasema Askofu Kilaini atakuwa pia ameponzwa na kauli yake aliyotoa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Akizungumzia matokeo ya uchaguzi huo, baada Jakaya Kikwete kupita kwa kura nyingi, Kilaini alikaririwa akisema Rais Jakaya Kikwete, alikuwa ni "chaguo la Mungu" kwa Watanzania. Kauli hiyo iliwakera baadhi ya viongozi na waumini walioanza kuona kuwa Kanisa linakuwa karibu kabisa na uongozi wa kisiasa.
Hata hivyo, Askofu Kilaini ambaye katika siku za karibuni naye amekuwa haisemi vizuri Serikali ya Kikwete, akijitetea kuhusu kauli yake ile, alisema maandiko yanaainisha kwamba kiongozi yeyote anayechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi walio wengi anakuwa ni "chaguo la Mungu".

Pamoja na utetezi huo wa Kilaini, bado amekuwa akisakamwa kwa kauli yake hiyo ambayo ilihusishwa pia na safari yake ya matibabu India, Septemba 2007, ambayo inaelezwa ya kuwa ilifadhiliwa na Rais Kikwete binafsi. Kauli na safari hii vimekuwa kayi ya vyanzo vya ufa kati yake na viongozi wenzake wa Kanisa, wakimwona kuwa amekwenda kinyume cha mambo kwa kuwa, kwa mfano, Kanisa lisingeshindwa kumlipia matibabu nje, ama hata kama ingebidi, basi angefadhiliwa na Serikali badala ya Rais Kikwete binafsi.

Akofu Kilaini hakuweza kupatikana wiki hii kuzungumzia kuhamishwa kwake, lakini watu wanaomfahamu wamethibitisha kuyumba kwa mahusiano yake na wenzake kutokana na sababu kadhaa, zikiwamo za kiutendaji na sababu nyingine binafsi.
Sababu za kiutendaji zinazotajwa kumponza Askofu Kilaini ni pamoja na wasiwasi wa viongozi wenzake kwamba anaweza "kutumiwa na wanasiasa" katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2010 kutokana na mahusiano yake ya karibu na wanasiasa wengi pamoja na kuwa karibu na vyombo vya habari.

Imeelezwa kwamba sababu binafsi zilizoyumbisha mahusiano yake na wenzake ni pamoja na madai ya kuwapo ukabila katika maamuzi yake mengi ikiwamo kuwaingiza watu kutoka mkoani Kagera katika nafasi nyingi za Kanisa ya Dar es Salaam na watendaji katika asasi kadhaa japo watu wanaomfahamu kwa karibu wameeleza ya kuwa madai hayo yametokana na chuki binafsi walizonazo baadhi ya wenzake.

Ndani ya Kanisa Katoliki kumekuwapo na maswali mengi yanayoulizwa baada ya kutangazwa kwa uhamisho wa Askofu Kilaini ikiwa ni pamoja na wanaohoji kama atateuliwa Askofu Msaidizi mwingine badala yake kumsaidia Pengo.
"Kawaida Askofu Msaidizi anaombwa. Ina maana Pengo, aliomba kuwa na Askofu Msaidizi. Je, sasa ameona hana haja tena kuwa na Askofu Msaidizi? Je, Askofu wa Bukoba ameomba kuwa na askofu Msaidizi? Maana ni lazima aombe!" Alihoji msomaji mmoja wa Raia Mwema lakini ambayo ni miongoni mwa waumini wa Kanisa Katoliki nchini na anayemfahamu vyema Askofu Kilaini.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana Askofu Msaidizi hawezi kuhamishwa kwenda kwingine kama si kupanda daraja na hivyo kwamba kwa kuwa Kilaini alikuwa Askofu Msaidizi Dar es Salaam kuhamishwa kwake kwenda kuwa Askofu Msaidizi wa Bukoba ambako si Jimbo Kuu kama Dar es Salaam ni jambo jipya katika mfumo wa Kanisa Katoliki.

"Hili ni jambo jipya. Maana baada ya kuwa Askofu Msaidizi kwa miaka 10 ilitarajiwa awe Askofu Kamili au awe Askofu Msaidizi Mrithi. Kwa vile ni Askofu Msaidizi, hata akifa Askofu wa Bukoba, si lazima Kilaini awe Askofu wa Jimbo la Bukoba, maana yeye si Askofu Msaidizi Mrithi," anasema muumini huyo.

Lakini baadhi ya watu wa ndani ya Kanisa Katoliki wamekuwa wakiamini kwamba uhamisho huo una nia njema na unalenga kumpandisha ngazi Askofu Kilaini ama pia kumsogeza karibu na nyumbani kwake apate kupumzika kutokana na kuyumba kwa afya yake.

Hoja nyingine inayojadiliwa ni kwamba Askofu Kilaini anaweza kuwa anaandaliwa kuwa Askofu Mkuu wa Mwanza, na kwamba kwenda kwake Kanda ya Ziwa kunamsogeza zaidi karibu na nafasi hiyo kwa kuwa kwa kawaida nafasi ya kwanza ya uteuzi wa Askofu wa Mwanza itatolewa kwa ya mtu mwenye sifa aliyeko Kanda ya Ziwa.
Taarifa ya Kanisa Katoliki iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padre Anthony Makunde ilieleza kwamba Baba Mtakatifu, Benedicto wa 16, amemhamisha Askofu Kilaini, kwenda kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Askofu Kilaini, ambaye amekuwa akimsaidia Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa miaka mingi, ameruhusiwa kuendelea kushika Kiti cha Jimbo la Strumnizza.
Aliteuliwa kushika nafasi ya Askofu Msaidizi Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Baba Mtakatifu, Yohane Paulo wa Pili.

Kilaini amekuwa mmoja wa viongozi wa dini anayesikika sana katika vyombo vya habari na alikuwa mmoja wa wachangiaji wakubwa waliozungumza katika kongamano la Mwalimu Julius Nyerere, lililofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni akiifananisha nchi ilivyo na mtu anayetembea bila nguo.
Miongoni mwa vichwa vya habari vilivyotikisa vikimnukuu Askofu Kilaini ni pamoja na:
"Askofu Kilaini atoa angalizo uchaguzi mkuu ujao; Askofu Kilaini: 2009 punguzeni pombe; Mafisadi EPA warejeshe riba pia - Askofu Kilaini; Askofu Kilaini, si ufisadi tu, yako mengi; Askofu Kilaini: Kikwete ameelemewa na mafisadi; Askofu Kilaini: Kingunge anajadili hewa." Kanisa Katoliki limeandaa na kusambaza nyaraka zake maalumu kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa 2010, Askofu Kilaini akiwa mmoja wa washiriki wakuu katika maandalizi na uhamasishaji wa yaliyomo ndani ya nyaraka hizo zilizowakera wanasiasa wengi na kuibua mjadala mkubwa katika jamii.
 
ni horizontal development in his career/lakini naye alikuwa anaongea sana
 
Askofu Nestory Timanywa wa Jimbo la Bukoba sasa hivi amekuwa Mzee sana, nadhani uhamisho wa Kilaini kwenda Bukoba ni kuongeza Nguvu pale. Haya ni maoni yangu.
 
Mengi yamesemwa hapa kuhusu uhamisho wa Askofu msaidizi Kilaini. Nachukua fursa hii kuwashukuru wanachama Paschal Matubi, Magobe T na Kituko kwa michango yao kuhusu huu uhamisho.

Moderators nilivyofuatilia naona bado tunahitaji jukwaa la dini ambalo litatumika kuelimishana katika masuala ya dini. Leo nimepata elimu toka kwa hao niliowataja hapo juu kuhusu baadhi ya taratibu za kanisa katoliki. Kama jukwaa hili lilileta mtafaruku hapo nyuma, basi labda lianzishwe tena halafu kuwe na moderation ya karibu na mwanachama ambaye ataandika hoja potofu au za matusi basi awe anafungiwa mara moja, tena permanent ban kwa ID hiyo. Na kama ataingia na ID nyingine tena basi ni lazima itafika mahali atajirekebisha maana hatafurahia kupoteza michango yake katika ban kila wakati.

Huu ni mtizamo wangu sijui wadau wengine mnaonaje? Asanteni.
 
Haya yote yanaeleweka na ni wewe tu usiyeyaelewa! For your information, mwanzoni mapapa, maaskofu na mapadre walikuwa wanaoa hadi karne ya 12, nadhani.

Kwa muda huo Kanisa lilikuwa katika 'scandals' nyingi za kula mali ya Kanisa, kuwaweka kwenye uongozi - upadre, uaskofu, upapa - watoto wa kiongozi fulani wa juu. Kulikuwa na 'nepotism' ya hali ya juu na pia watu wengi walidai fidia hasa padre, askofu au papa fulani alipoaga dunia... wakidai ni watoto wake na hivyo wanataka sehemu ya urithi wao. Kulikuwa shida kujua ni nani alikuwa sahihi na ni nani hakuwa sahihi.

Papa fulani alipoingia madarakani, akataka kuleta 'radical changes' ili kuondokana na matatizo ya wakati huo na ndipo 'discipline ya celibacy' ilipoanzishwa (na siyo divine law, muda wowote inaweza kubadilishwa).

Of course, Biblia ni neno la Mungu na mstari fulani unaweza kukugusa wewe na mstari mwingine usikuguse ila ukamgusa mtu mwingine. Si unakumbuka pia kwamba hata baadhi ya mitume walikuwa na wake? Siku moja Yesu aliwapa fundisho la kuwagusa kuhusu kuacha familia na kumfuata yeye na Petro akasema: "Tazama sisi tumeacha yote na kukufuata wewe tutapokea nini?"

Yesu akawajibu kuwa "walioacha familia - mke, watoto, wazazi kwa ajili yake - watapokea mara mia zaidi na kuurithi ufalme wa mbinguni." Pia kuna sehemu alifundisha kuhusu kumwacha mke na kumwoa mwingine kuwa ni kuzini dhidi yake na wao wakasema kama ndivyo hivyo hakuna haja ya kuoa kwani hakuna atakayeokoka.

Na yeye akawajibu "si wote wanaoweza kupokea fundisho hili bali wale tu ambao wamefunuliwa". Kwa hiyo, kama mtu mwingine akisoma maneno haya na kuguswa nayo na kujitahidi kuyaishi kiaminifu, who am I to say, he's wrong? Ikitokea pia mtu mwingine akasoma mstari uliou'qoute' na kuguswa nao pia ni sahihi kuishi hivyo.

By the way, unajua 'context' yake? Ilikuwa pia tatizo fulani lilikuwa limeshajitokeza katika viongozi wa Kanisa kuoa wake zaidi ya mmoja.

Nadhani sasa ndiyo imekuwa zaidi, kwani mapadre wanakula sana mali za kanisa wamejenga majumba na kuweka wanawake ambao siyo ndugu zao (Nina hakika ni hawara zao) wanakaa humo na wamenunuliwa magari ya kifahari kwa fedha za kanisa. wanao watoto wengi na wengine mpaka wamefikishwa mahakamani kwa kutembea na wake za watu(Mfano kesi ya Agustino Nyambita Mwanza ambaye alikuwa afisa usalama wa taifa) na padri mmoja ambaye sasa ni Askofu Musoma.

Kwa nini wasioe tu?
 
Hizi kesi za Mapadre kupenda wanawake ni nyingi mno na mpake inafikia kuleta aibu kwani wanapenda ndugu zetu, watoto wetu au jamaa wetu tunaowafahamu, na tena kuishi nao humo humo kwenye conventi zao mpaka kupikiwa na kupakuliwa. Lakini kama alivyopendekeza Member Maane, hapo juu ni kuweka jukwaa hilo yote yaende huko kwani hapa tunajadili uhamisho wa Askofu Kilaini.

Kuna Mambo mengi sana kwenye Ukatoliki huu uhamisho wao kuanzia kwa Mapadre kuna uonevu mkubwa sana mpaka Mapadre wengine wanafikia kuhama nchi kwenda nchi nyingine. Mifano ipo tunaifahamu.

Kuna Maparoko huko vijijini wananyanyasa wakristu utafikiri wenyewe wamerithi jimbo kwani tokea tumezaliwa wapo pale mpaka wanasubiria kufia hapo, hata hawahamishwi. Inashangaza kuona hapa Dar Mapadre wengi wadogo tu wamejaa kila kanisa.

Majaribu ni mengi sana lakini tunamfuata Kristu kusudi tusikwazike.
 
Askofu Nestory Timanywa wa Jimbo la Bukoba sasa hivi amekuwa Mzee sana, nadhani uhamisho wa Kilaini kwenda Bukoba ni kuongeza Nguvu pale. Haya ni maoni yangu.

'Askofu timanywa amekuwa mzee sana' Mzee wa umri gani maana umri wa askofu na kustaafu ni miaka 75 kama sana yako inamfikisha zaidi ya miaka 75 basi anapaswa kustaafu na kuachia kiti, na hii itakuwa maandalizi ya Kilaini kukalia kiti ama kushika kwa muda mapaka atakaekikalia apatikanae
 
Pamoja na uelewa wangu mdogo, niseme tu kile ninachojua:

Mhashamu: Ni neno litumikalo kama tutumiavyo neno 'mheshimiwa' lakini kwa Maaskofu tu. Neno jingine ni 'Mwadhama', hili linatumika kwa makardinali. Mifano inaweza kuwa Mhashamu Baba Askofu Methodius Kilaini, na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Kardinali: Hawa ni maaskofu au mapadre wanaoteuliwa na Baba Mtakatifu (Papa) kama wasaidizi wake wa karibu katika masuala mbalimbali na pia ni washauri wake katika mambo ya uongozi. Makardinari kwa kawaida wanaishi huko Vatican, lakini Makardinari wanaoteliwa wakiwa maaskofu katika majimbo yaliyo katika nchi zao (mf. Kard. Pengo) wanaishi katika nchi zao, wakiendelea na kazi zao za kawaida, na wakati huohuo wanakuwa wasaidizi na washauri wa Papa. Hawa makardinali wana haki zote kama raia wa nchi ya Vatican City (Rais ndiye Papa) na ndio hawa ambao wanapiga kura ya kumchagua Papa, na Papa kwa kawaida anachaguliwa kutoka katika kundi hilo la makardinali.
Kwa kifupi ndio hivyo nijuavyo.

Nitaanza na maana ya Ukardinali: Neno Kardinali linatokana na neno la Kilatini la Cardo ambalo twaweza kusema ni sawa na Bawaba kwa Kiswahili. neno hili limetokana na uhamisho wa watumishi (Mashemas, Mapadri na Maaskofu) wa kanisa kwenda jimbo jingine, ulifananishwa na ule mlango kuhamishiwa ukutani kwa kushikiliwa na bawaba (Cardo). Hivyo zamani waliohamia jimbo lolote waliitwa “Cardinal” neno tunaloliita “Kardinali” .
Katika karne ya 9 haki ya kutambulika kama “Kardinali” ilibaki kwa baadhi ya waliohamishiwa jimbo moja tu la Roma au jimbo la Papa. Padri aliyehamishiwa Roma alipewa kanisa na lililoitwa Titular Church. Padri huyu alijulikana kama Cardinal-Priest (Kardinali-Padri).
Kumbe kutokana na hali hiyo zipo aina tofauti za Kardinali na hiyo Cardinal-Priest ikawa ni aina ya kwanza ya makardinali.
Aina ya pili ya Kardinali ilitokana na baadhi ya mashemasi walioahamishiwa Roma walipewa kazi tofauti ikiwemo vituo vya huduma za kijamii vilivyojulikana kama deaconry. Hawa waliitwa Cardinal-Deacon (Kardinali-Shemasi).
Ofisi ya Papa ilihitaji msaada wa maaskofu hasa wa majimbo madogo jirani na Roma yaliyoitwa “Suburbicarian Diocese”. Kuhitajika Roma kuliwapa maaskofu hawa sifa ya ukardinali, wakajulikana kama Cardinal-Bishop (Kardinali-Askofu) na kuwa aina ya tatu ya makardinali.
Hivyo, aina tatu za makardinali ni Cardinal-Deacon, Cardinal-Priest na Cardinal-Bishop. Sina hakika kama tafsiri yake ni Kardinali-Shemasi, Kardinali-Padri na Kardinali-Askofu.
Mwaka 1150 liliundwa jopo linaloendelea kuitwa College of Cardinals au jopo la makardinali wote. Papa alipenda kuwaita makardinali kwenye vikao vilivyoitwa Consistory hadi leo. Consistory huwa ya makardinali wachache walioko Roma (ordinary consistory) au ya makardinali wote duniani (extraordinary consistory).
Mwaka 1059 ilipitishwa kwamba Papa mpya atakuwa akichaguliwa na jopo la makardinali kwenye mkutano uliopewa jina Conclave linalotumika hadi leo.
Papa Paul VI aliweka umri chini ya miaka 80 uwe sifa ya Kardinali kuhudhuria Conclave. Papa John Paul I ambaye upapa wake ulidumu kwa siku 33 ndiye wa kwanza kuchaguliwa kwa utaratibu huo Agosti 26, 1978.
Nimekumegea kwa msaada wa makala za Joseph Misango ambazo aliziandika T.Daima .
 
Wakuu naomba kuelimishwa,

Mhashamu Kilaini anaweza kuwekwa katika kundi gani kimitizimo kati ya manne hapo chini...

A)Radical, B)Liberal, C)Conservative, D)Extremist?

Je, vipi kuhusu Mwadhama Pengo?

Je kuondoshwa/kuhamishwa kwa Kilaini kunaweza kuwa na athari gani katika suala zima la mahusiano ya kijamii katika nchi yetu ukichukulia kuwa Dar es Salaam ni chungu cha mengi kama siyo yote Tanzania na hali ilivyo sasa?

omarilyas
 
'Askofu timanywa amekuwa mzee sana' Mzee wa umri gani maana umri wa askofu na kustaafu ni miaka 75 kama sana yako inamfikisha zaidi ya miaka 75 basi anapaswa kustaafu na kuachia kiti, na hii itakuwa maandalizi ya Kilaini kukalia kiti ama kushika kwa muda mapaka atakaekikalia apatikanae

Askofu Timanywa alizaliwa 1937
Upadilisho akapata 1966
Uaskofu akaupata 1974
Sasa hivi ana miaka 72

Alipata upadre akiwa na umri mdogo miaka 37.

Kilaini alizailiwa 1948
Sasa hivi ana miaka 61

Askofu yeyote anastaafu kwa kufikisha 75 lakini anaweza kuomba kabla ya hapo. Hayo ndo majibu yangu.
 
Nilisema mapema kabisa hapa kuwa huu uhamisho kuna jambo la ziada si bure tu kwa kiongoozi kama Kilaini kuwa Askofu msaidizi kwa miaka zaidi ya kumi tena wa Cardinal kuhamisha kuendelea na wadhifa wa uaskofu msaidizi tena Bukoba kuna jambo hapa. Sidhani kama anaandaliwa kushika wadhifa wowote bali kafichwa huko ili tumsahau.
 
Magobe T,
Naomba unifafanulie hili la ukabila Maaskofu kuajili watu kutoka makabila yao na kuwaacha mapadre wachapakazi na tena vijana wasomi na kuajiri wazee kwa sababu wanatoka Kabila moja. Mfano ni marehemu Askofu Samba tulipokuwa Makoko Seminary tulizoea kumuita Pum**,alikuwa ni mchaga basi mapadre wote viongozi walikuwa ni wachaga hata ugawaji wa magari aliwapatia mapadre wachaga wakati mapadre wazalendo wa Musoma walikuwa wakitumia pikipiki halafu tena alikuwa na tabia ya kuendeshwa na masista wachaga hakutaka kuajiri dreva kutoka pale Musoma. Alikuwa AKIENDA PALE KWENYE SHIRIKA LA EMACULATE ANACHAGUA VI SISITER VIDOGO VIDOGO VICHAGA NA KUVIFANYA NDIVYO VILEZI NA WAFANYA USAFI WA HEKALU LAKE HUKU AKIWAOA NA KUWABADILISHA KAMA NGUO.
 
Ndio mjue kuwa vyeo vya kanisa siyo kama vya siasa.Ni utumishi na unaweza kupelekwa popote. Mbona hata jimbo la Same liko wazi na hajapelekwa huko.
Huenda uzoefu na umahiri wake unatakikana Bukoba zaidi ya PENGINE.

Wakatoliki nawavulia kofia kwa unpredictability yao. Kuna padri namfahamu alikuwa mwalimu kule Catholic University of Eastern Africa, Nairobi, kipindi hicho ana masters tu. Akapelekwa Rome kufanya PhD, nikajua huyu akirudi atapewa uprofesa kabisa. Nilishangaa mno. Aliporudi alipelekwa eneo fulani la mashenzini kabisa vijijini ndani Karatu huko, eti akaanzishe kigango kipya (wala siyo paroko angalao!). Hawaeleweki hawa jamaa!
 
Ni kweli Mtu B unavyosema. Lakini sio kwamba hawaeleweki in the sense ya kutoeleweka, Nikwamba kwa utaratibu wa kanisa hili, kila padri ni lazima awe tayari kufanya kazi yoyote regardless anaipenda au haipendi, anataka au hataki, hatakama siyo aliyosomea (profession yake ki elimu), provided anaiweza. Nilazima atii mda wote na kanisa pekee ndilo lenye mamlaka ya kumpangia kazi kulingana na mahitaji ya kanisa na kwa wakati husika na siyo matakwa yake binafsi. Hata hivyo anaweza akatoa maombi au mapendekezo lakini silazima akubaliwe.
 
duh! hakika hii ni demotion japo haionekani lakini kwa wachache wanaelewa. upepo wa kisiasa na waraka ule ndio vimepelekea haya ili dini isionekane inachochea ugomvi japo ufisadi unakataliwa na dini. (haya ni kwa jinsi navyoona mm binafsi)
 
basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika mume wa mke mmoja (i timotheo 3:2), kisha mwenye kuisimamia nyumba yake vema,ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu (1 timotheo 3:4)
hizo ni miongoni mwa sifa za askofu kulingana na mkusanyiko wa vitabu(kigiriki biblos,kiingereza bible) sasa hawa maaskofu wasiooa wamepata wapi kifungu kinachowaambia padri au askofu asioe?

yaleyale mapokeo na historia za mababa wa kanisa

Uko sawa kabisa mkuu. Nafikiri wangeruhusiwa kuoa rate ya udhalilishaji wa vijana (watoto wadogo wa kiume) huenda ingekuwa ndogo. Mapadri wengi tu leo wana watoto wengi tuuu mitaani kitu kinachoonyesha unafiki wa hali ya juu kuhusu suala hili. Jamaa hawawezi kukaa hivyo hivyo bila tendo la ndoa kwa sababu wana maisha maisha mazuri ya duniani yakiambata na kula vizuri na hivyo kuufanya mwili uwe kwenye uhitaji mzuri wa kufanya tendo la ndoa. Si mpango wa MUNGU tangu mwanzo mwanaume aishi maisha yake yote bila kuoa. Mbaya zaidi huingilia sana hata ndoa za washirika wao kama vile marehemu askofu Butibubage wa Mwanza alivyovunja ndoa ya Pius Msekwa baada ya kuzaa naye mtoto (watoto). Mhhh! Mbaya kabisa hii. Mapokeo mabaya kabisa haya jamani.
 
Magobe T,
Naomba unifafanulie hili la ukabila Maaskofu kuajili watu kutoka makabila yao na kuwaacha mapadre wachapakazi na tena vijana wasomi na kuajiri wazee kwa sababu wanatoka Kabila moja. Mfano ni marehemu Askofu Samba tulipokuwa Makoko Seminary tulizoea kumuita Pum**,alikuwa ni mchaga basi mapadre wote viongozi walikuwa ni wachaga hata ugawaji wa magari aliwapatia mapadre wachaga wakati mapadre wazalendo wa Musoma walikuwa wakitumia pikipiki halafu tena alikuwa na tabia ya kuendeshwa na masista wachaga hakutaka kuajiri dreva kutoka pale Musoma. Alikuwa AKIENDA PALE KWENYE SHIRIKA LA EMACULATE ANACHAGUA VI SISITER VIDOGO VIDOGO VICHAGA NA KUVIFANYA NDIVYO VILEZI NA WAFANYA USAFI WA HEKALU LAKE HUKU AKIWAOA NA KUWABADILISHA KAMA NGUO.

Mungu anatuita kumtumikia (wewe, mimi na yule) 'in our own skins' (na udhaifu wetu). Kwa hiyo, ni jukumu la kila mmoja wetu kujitahidi kushinda tamaa za mwili pamoja na udhaifu wetu wote. Kuna baadhi ya mapadre na maaskofu siyo waaminifu, ndiyo. lakini kuna 'speculations' nyingi zinasemwa hata kama padre au askofu anaishi wito wake vizuri.

Nilikuwa sehemu fulani na mume mtu alikuwa amefika wiki hiyo kutoka Afrika Kusini anakofanya kazi. Alikuwa na Toyota Corola nyeupe ila yenye number plate nyeupe na namba nyekundu. Nyumba yake haikuwa na fensi na hivyo alikuwa anapaki gari lake nje. Kulikuwa na padre mmoja kijana. Ana gari Toyota Corola pia, ila number plate ilikuwa ya rangi ya njano na namba zake nyeusi.

Wakristo walipoona hilo gari nje na hata usiku lilikuwepo pia, wakapeleka habari kwa askofu kuwa gari la padre yule kijana limeonekana usiku na mchana kwa wiki nzima kwa mke mtu. Kilichomwokoa ni yule mume mtu kusema tangu afike hapo nyumbani hajawahi kutoka na hivyo habari hizo ni za uongo.
Unaona jinsi gani habari zinavyoweza kuenea? Na kama yule jamaa angerudi Afrika Kusini mapema si watu wangeamini kabisa padre alikuwa ana lala pale?

Mara nyingi kitu kinapotokea kunakuwa na 'speculations' nyingi na si rahisi kujua kipi ni kweli na kipi ni uongo. Mfano, tukifuata idadi ya watu, mapadre Wasukuma, Wahaya na Wachaga ni wengi zaidi kuliko, mfano, mapadre Wazinza, Wakara, Wazanaki.

Kwa jinsi hii, inawezekana kabisa katika kila idara ya ngazi za juu za uongozi wa Kanisa awepo padre Mhaya, Mchaga na Msukuma na inawezekana asiwepo kabisa padre Mkara, Mzinza na Mzanaki kwa vile idadi yao ni ndogo. Hii inatokea 'naturally' na siyo ubaguzi au upendeleo. Hivyo, kama Wahaya wengi wako kwenye ngazi za uongozi inatokana zaidi na kuwa na idadi kubwa ya mapadre kuliko ubaguzi.
Mwenye mamlaka ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam ni Kardinali Pengo na hakuwa Methodius Kilaini. Kilaini alikuwa msaidizi. Katika kila jimbo askofu anafanyakazi na mapadre na kukiwa na sababu ya mabadiliko ya 'appointments' askofu anashauriana na hao mapadre baada ya kufanya 'consulatation'. Mfano, kwa Dar es Salaam, Pengo alikuwa anashauriana na Kalaini na baadhi ya mapadre kama kunafanyika mabadiliko fulani.

Kwa upande wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kuna utaratibu wake pia. Huo unahusisha maaskofu na mapadre wengi kidogo. Hivyo, si rahisi askofu afanye upendeleo na kwa kesi ya Kilaini, Pengo asingekubali Kilaini afanye upendeleo wa mapadre kutoka Kagera au Bukoba wakati Pengo ndiye ana uamzi wa mwisho.
Kwa upande wa mapadre wa mashirika, 'appointements' zote zinafanywa kwa kuwahusisha members wote wa mahali na 'consulatation' inafanyika kwa kupiga kura. Ukipiga kura ya ndiyo, hupaswi kutoa maelezo na ukipiga kura ya hapana unapaswa utoe maelezo ili kama kuna sababu za maana zipate kujulikana kuhusu mtu anayepigiwa kura. Na hii inasaidia pia sehemu husika kupima sababu zenyewe kuona kama ni za kweli.
 
Back
Top Bottom